Wakazi wa Dar badilikeni

Wakazi wa Dar badilikeni

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,498
Reaction score
28,723
Naongea haya kwa uchungu mkubwa ,kuhusu wanaume na wakazi wa dar kwa ujumla .

Mnamo mwaka 2013 nilikuja dar kwa mara ya kwanza nikijiunga chuo kikuu UDSM ,
Siku moja majira ya saa 9 mchana nikiwa narudi hosteli za mabibo nilipita maeneo ya SONGAS kwenye mitambo ya umeme, hakika ilikuwa saa 9 kweupe nilikwapuliwa wallet na kunyang'anywa Pesa zangu kiasi cha 50000, nilipiga kelele kuhitaji msaada , lakini wakazi hasa Wanaume wa darisalama waliniangalia tu huku wakinipita na kumuacha yule kibaka akitamba ,..

Iliniuma sana kwani sikuwahi kudhani kwamba Wanaume na wakazi wa dar wapo hivo, nilijiuliza ni uoga au ndio kila mtu na maisha yake, kwamba kila mtu kaja kutafuta.

Niliondoka na kwenda polis kutoa taarifa waje wawakamate wale vibaka . Nilienda kituo cha polis ubungo ndani ya stendi , cha ajabu nao walinipiga dana dana wakitaka hela ndio wakamkamate..

Nikaondoka nikaenda kituo cha polis urafiki

Sikupata msaada.

Nikarudi ubungo mataa nikiwa nimechoka nisielewe tabia za wakazi wa dar.

Bahati nzuri nikakutana na mwanajeshi nikamueleza tukio zima, tukafunga safari hadi kwa hao vibaka , akakamatwa na kunirudishia pesa yangu.

SASA kuna tukio limetokea huko buguruni , kijana mmoja ansjiita Scorpion anachoma watu visu na kupora , mchana kweupe lakini ...wanaume wa dar wanakuacha hawatoi msaada .


Ni juzi amemtoboa mfanyabiashara mmoja macho na kumchoma visu lakini watu walishuhudia na hawakutoa msaada wowote.

Polis wapo siku zote wanajua kuhusu huyu kibaka...

Mpaka vyombo vya habar vimepiga kelele ndio katiwa nguvuni


NINACHOSHANGAA MBONA MIKOANI KUNA USHIRIKIANO TOFAUTI NA HUKU DAR?

HEBU WANAUME NA WAKAZI WA DAR MBADILIKE SOTE NI WATANZANIA
 
Mikoani watu wana akili sana + umoja. huyu Scorpio angekuwa amesha uwawa muda mrefu sana, hawezi kutesa watu bila sababu.
 
Dar masharobaro.

Inatakiwa mtu mnasaidiana na sio kuangaliana. Its a shame.
 
Pole sana kwa kukaribishwa mjini na vibaka.
Watu tunaoishi Dar tumezaliwa mikoani hizi tabia tumezikuta hivyo tunatafuta suluhisho taratibu.
Pole sana.
 
ila wamemfanya mbaya aisee
yeye kumnyofoa mwenzie macho na kumpatia kilema cjha maisha na wote aliowaumiza ni sawa hebu jiweke miguunii kwa huyu aliyepofuliwa macho

mi naona kama adhabu ya huyu shetwaii angekyofolewa na yeye kiungo kimoja baada ya kingine waanze na jicho moja
 
yeye kumnyofoa mwenzie macho na kumpatia kilema cjha maisha na wote aliowaumiza ni sawa hebu jiweke miguunii kwa huyu aliyepofuliwa macho

mi naona kama adhabu ya huyu shetwaii angekyofolewa na yeye kiungo kimoja baada ya kingine waanze na jicho moja
simwonei huruma yani nafurahi jinsi wanaume wa dar wamefanya hadi analia mama,.... nashindwa kuweka aisee
 
nimeona video wmemvunja miguu tayari Scorpio

Unanchanganya
6773a111b18a02f06192959a7b9a9315.jpg
 
Huku daslam watu wake kichefuchefu sana hata mm rafiki yangu alikabwa mchana saa sita kweupe,pembeni walikaa vijana hawakuamka kumsaidia ila baada ya vibaka kuondoka wanajisogeza kumuuliza kulikoni,aliwatia matusi na kuondoka
 
Back
Top Bottom