Wakazi wa Dar badilikeni

Wakazi wa Dar badilikeni

Wenye tabia kama za scorpio wapo wengi hasa kwenye uporaji, ujambazi na ubakaji. Ni vyema kuripoti ktk jeshi la polisi. Wananchi kujichukulia maamuzi mikononi kwa kuwachoma moto au kuwakata viungo sio sahihi.
Kuna watakaokosa haki zao, wanaweza kutumika kuzalisha wakiwa jela
 
Kwakweli maana huu ni udhalilishaji

Wanaume wa dar wako busy kushindana na dada zao kupaka poda na kuvaa heleni
Tatizo lenu uko mikoani mnaogopa wanyonya damu,mnadhani kila dakika mkiona jambo mpige kelele ili kuwaua wanyonge? Nawewe ulieleta hii thread ulipokabwa kwanini haukupambana au na wewe ulikuwa tayari wa Dar?onyesha unapambana utapatiwa msaada sio unakuwa lege lege hapa mjini.
 
Ni kweli kabisa wanaume wa dar mabishoo muno. Potelea mbali mkinishambulia ukweli utabaki pale pale.
Vibaka wanaoiba taa na vifaa vingine vya magari huwaibia wakiona na hakuna kusaidiana, halafu utashangaa karibu kila gari analoendesha mwanamume huwa na panga au kisu lakini ni cha ubishoo tuu. Ukweli dar hakuna umoja wao wanadhani umoja ni kushindana kutongoza na kupiga facial scrub!

Haya njooni mtoe mapovu sasa..
 
Ni kweli kabisa wanaume wa dar mabishoo muno. Potelea mbali mkinishambulia ukweli utabaki pale pale.
Vibaka wanaoiba taa na vifaa vingine vya magari huwaibia wakiona na hakuna kusaidiana, halafu utashangaa karibu kila gari analoendesha mwanamume huwa na panga au kisu lakini ni cha ubishoo tuu. Ukweli dar hakuna umoja wao wanadhani umoja ni kushindana kutongoza na kupiga facial scrub!

Haya njooni mtoe mapovu sasa..
Sijaona chochote ulichoandika,Dar ni tofauti kubwa sana na mikoani hilo lazima ujue,wewe umekalili tu dar watu hawasaidiani sio kweli tatizo unaweza kumsaidia mwizi ukifanya mchezo,wewe unaeibiwa jaribu kuonyesha unapambana uone kama watu watakuacha peke yako
 
Sijaona chochote ulichoandika,Dar ni tofauti kubwa sana na mikoani hilo lazima ujue,wewe umekalili tu dar watu hawasaidiani sio kweli tatizo unaweza kumsaidia mwizi ukifanya mchezo,wewe unaeibiwa jaribu kuonyesha unapambana uone kama watu watakuacha peke yako
Umekalili=umekariri....mmmh wanaume wa dar!!
 
Na pia usisahau kua wanaume wa Dar 70% wana vitambi, na vijana wa kiume wa Dar ni ngumu kuwatofautisha kwakua woote hujiremba na kujipamba kama Mashoga.
Eti na "panya road" wanawashinda!!! tatizo wanakula mahindi kwa chunvi na ndimu!

Cjui wanapiga gym za nin sasa! Kutunisha miili tu, au nn?
 
Nyie wavulana wa mikoani mna shida sana alafu mnakuwaga na kashfa sana mkisha rudigi makwenu wakati mkija huku mnataka wenyeji wenu waache shughuli zao wa wazungushe jiji zima.Mara mkapige pic kwenye sanamu la askari,mara mpelekwe coco beach..tena wangine mnafikaga mbali mnataka mpelekwe mpaka state house.We dar gani iyo uibiwe mchana kweupe alaf upige kelele wadau tusichukue hatua zozote..huyo mfanyabiashara alitobolewa macho usiku co mchana kweupe kama media zinavyotangaza
 
Hili sio dar tu hata mbeya nako hakufai mke wangu kaporwa saa mbili asubuhi kweupe pale uyole hata kusaidia hakuna Watz hatusaidiani siku hizi unaibiwa watu wanakutolea mimacho tu
Badala ya kukusaidia wanakurekodi video kwenye smartphone ...tena wanaombea kibaka aendelee kukukaba ili wafike warekodi video!!
 
naomba nipite taaaratibu, bila kumbugudhi mtu
 
Hahahahahaha ni kazi sana kumtofautisha mwanaume wa Dar na mwanamke.
 
hizo nguvu za kusaidiana zinatoka wapi chips, juisi na maji ya kiroba?

Ndugu yangu ulipotaja VIROBA umegusa point sana.

Sasa hivi Dar watu wanakunywa VIROBA kama maji. Unakuta mtu ananuka KIROBA na amechoka. Tena yupo kwenye public service.

Sijui serikali inatazama vipi swala la Viroba mijini.
 
Naongea haya kwa uchungu mkubwa ,kuhusu wanaume na wakazi wa dar kwa ujumla .

Mnamo mwaka 2013 nilikuja dar kwa mara ya kwanza nikijiunga chuo kikuu UDSM ,
Siku moja majira ya saa 9 mchana nikiwa narudi hosteli za mabibo nilipita maeneo ya SONGAS kwenye mitambo ya umeme, hakika ilikuwa saa 9 kweupe nilikwapuliwa wallet na kunyang'anywa Pesa zangu kiasi cha 50000, nilipiga kelele kuhitaji msaada , lakini wakazi hasa Wanaume wa darisalama waliniangalia tu huku wakinipita na kumuacha yule kibaka akitamba ,..

Iliniuma sana kwani sikuwahi kudhani kwamba Wanaume na wakazi wa dar wapo hivo, nilijiuliza ni uoga au ndio kila mtu na maisha yake, kwamba kila mtu kaja kutafuta.

Niliondoka na kwenda polis kutoa taarifa waje wawakamate wale vibaka . Nilienda kituo cha polis ubungo ndani ya stendi , cha ajabu nao walinipiga dana dana wakitaka hela ndio wakamkamate..

Nikaondoka nikaenda kituo cha polis urafiki

Sikupata msaada.

Nikarudi ubungo mataa nikiwa nimechoka nisielewe tabia za wakazi wa dar.

Bahati nzuri nikakutana na mwanajeshi nikamueleza tukio zima, tukafunga safari hadi kwa hao vibaka , akakamatwa na kunirudishia pesa yangu.

SASA kuna tukio limetokea huko buguruni , kijana mmoja ansjiita Scorpion anachoma watu visu na kupora , mchana kweupe lakini ...wanaume wa dar wanakuacha hawatoi msaada .


Ni juzi amemtoboa mfanyabiashara mmoja macho na kumchoma visu lakini watu walishuhudia na hawakutoa msaada wowote.

Polis wapo siku zote wanajua kuhusu huyu kibaka...

Mpaka vyombo vya habar vimepiga kelele ndio katiwa nguvuni


NINACHOSHANGAA MBONA MIKOANI KUNA USHIRIKIANO TOFAUTI NA HUKU DAR?

HEBU WANAUME NA WAKAZI WA DAR MBADILIKE SOTE NI WATANZANIA
Kwa hiyo unalalamikia wanaume wa dar au wakazi wote maana naona unazungumzia sana sana wanaume wa dar
 
Katika jambo lililonisikitisha ni pamoja na hilo watu wamekaa wanaangalia mwenzio anacharangwa na visu na wao wamesimama hivi wauza kuku si wanakuwaga na visu? Saa NNE usiku buguruni ni kama mchana watu wanakuwa wengi tu ni katika maeneo ambayo watu hawaishag pale hata usiku wa manane imekuaje mtu anatobolewa macho na wao wanaangalia? Et wengine wanasingizia kuwa anapiga karate watu mko 100 karate zitafua dafu? Tuwe tunasaidiana
 
Back
Top Bottom