KERO Isamilo, Mwanza: Wakazi wa mtaa wa Maendeleo tunasumbuliwa na wanaoegesha malori kwenye mageti yetu

KERO Isamilo, Mwanza: Wakazi wa mtaa wa Maendeleo tunasumbuliwa na wanaoegesha malori kwenye mageti yetu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
photo_2026-05-28_17-33-23.jpg
Sisi wakazi wa Isamilo, Mtaa wa Maendeleo, tunawasilisha rasmi malalamiko yetu kuhusu kero kubwa inayotukabili katika eneo letu la makazi.

Kuanzia mwezi Aprili, 2026, jirani yetu mmoja amefungua gereji isiyo rasmi (garage bubu) ndani ya mtaa huu wa makazi, na ameigeuza kuwa sehemu ya kupakia na kushushia mizigo ya malori makubwa. Kutokana na hali hiyo, malori hayo yamekuwa yakipaki nje ya mageti ya nyumba zetu, jambo linalosababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi.
photo_2026-05-28_17-37-35.jpg
Hali hii imeleta athari zifuatazo:Kuzuia njia za kuingia na kutoka majumbani kwetu, Kuweka hatarini usalama wa wakazi, hasa watoto, Kelele na usumbufu mkubwa mchana na usiku, Uharibifu wa mazingira ya makazi ambayo siyo ya kibiashara.

Tulifika kwa Mwenyekiti wa Mtaa ili kupata ufumbuzi, lakini hadi sasa hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa. Inasemekana kuwa ameshapewa ushawishi usio rasmi, hali inayozua wasiwasi juu ya uwajibikaji wake. Pia tulitoa taarifa kwa TARURA, lakini hatujapata ushirikiano wowote hadi sasa.

Kutokana na hali hiyo, tunaomba mamlaka husika ziingilie kati haraka iwezekanavyo ili: Kusitisha matumizi ya eneo hilo kama kituo cha malori, Kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mhusika, Kulinda usalama na haki za wakazi wa eneo hili.

Tunaamini mamlaka itachukua hatua stahiki ili kurejesha utulivu na usalama katika mtaa wetu.
 
Back
Top Bottom