Wakati wa mimi kusema umefika

Pasco umemaliza kila kitu. Watu sio kuwa wanamzuia kusema bali hizi tabia za tisha toto zinaonyesha anachotaka kusema (tena kwa wakati huu) kina malengo maalum. Hapa hajasema kitu tayari tafsiri zimekuwa nyingi kwa kadri kila mtu anavyotamani iwe. Hata kama hata sema tayari kuna damage fulani hivi ambayo ishatokea. Huyu bwana akija hapa na kusema " yale yote niliyosema mahakamani ndio ukweli wenyewe na MUNGU ni shahidi yangu kuna watu watasema kesha tishwa ndio maana kasema hivi.
Aliloonyesha Deus naungana nawe ni tabia za kike kabisa.



Sent from my iPad using JamiiForums

Watu mnamtukana Mama zenu na Dada zenu na wake zenu kwa kudhani kuwa Mnamtukana Deus F Mallya. Poleni sana
 
Last edited by a moderator:
nimesoma nimekuelewa ndugu mallya
lakini ni lini utasema? Pia kinachonitia mashaka ya unachotaka kusema ni kujitokeza kundi linalopinga wewe kusema. Hili kundi ni la nani? Liko chini ya nani? Wanataka unyamaze kwa faida za nani?

wewe deusi,fahamu kuwa hata kama utatumia 'id'ya kichina utafahamika tu mdogo wangu!
-jaribu kuzifikiria pesa wakati huo jipime future yako itakuwaje baadae,maana siamini kwamba mwanzo wakati upo dodoma mahakamani ulikuwa na ugonjwa wa akili eti sasa ndiyo umepona unataka kujisahihisha!
"jiulize katika ile ajali kuna siku wanachadema waliwahi kukutuhumu kuwa unahusika na kifo cha wangwe?,
maana hawa wanachadema ambao unataka kuwachafua na tuhumu za kupandwa kama hizo.
Wao ndio walio kuwa mstari wa mbele kuku tetea na kweli wengi tulikuamini pale ulipo jieleza.
Japo yawezekana kuna wengine hawakukuamini na hasa wana c.c.m,na zaidi ni wale makada wa chama ambao naamini walikuwa wanajua kila hatua ya movie dhidi ya wangwe kwa uhusika wao.
 
Ni aibu, kama kuna namna tuliyomalizwa ni namna tuliyofanyiwa vijana wetu wote wakawa mataahira. Aliyetufanyi hivi katuweza, sijui alitumia vyakula vya watoto au alitumia dawa za chanjo mimi sijui.

Kama Taifa sasa ni lazima tufanye kila namna kujua kinachowafanya vijana wetu kuwa mataahira, hasa wanaojitokeza kuingia katika siasa. Aina hii ya vijana ni hatari kwa usalama wetu na nchni yetu,kwa namna hii kuna kila dalili Taifa hili litamezwa huko mbeleni. Kuna wale wa kike ambao mimi nilidhani ni tabia za umalaya hasa zinazosababiwa na tamaduni na tamaa za badhii ya makabila yetu, sasa hawa wa kiume ambao hawawezi kuona na kujadili matatizo yetu ya kijamii na kiuchumi wao kila wakati ni kujadili watu na kujenga chuki miongoni mwetu?
 
Salaam!

Kwa muda Mrefu nimekuwa nikipata msukumo unaonitaka kuzungumzia maneno yaliyosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari hivi karibuni kutoka kwa ndugu ma makundi mbali mbali.

Kimsingi sintajibu wanayotaka kwa sababu nimeendelea kupokea jumbe za Matusi na kejeli hata kuvamiwa na wanaodai ni wafuasi wa CHADEMA wakitaka niendelee kuwa Kimya!. Wapo walioamua kujitaja majina yao ili nijue ni kiasi gani wako 'Serious' kwenye kile wasemacho!.

Japo nilishatoa taarifa Polisi, kwa sasa nimechoka kuishi maisha ya kuwindwa ndani ya Nchi yangu. Nimechoka. Nitakachofanya ni KUONGEA na si KUJIBU kilichosemwa na yeyote kuhusu Mimi na 'Ajali ya Pandambili'

Naamini kwa Mungu siku zote
Naamini nikifa ni kwa Mpango wake
Nikifa ukweli Utaishi hadi vizazi vijavyo.

Deus Mallya
Dar es Salaam.
Kuelekea uchaguzi tutasikia mengi sana. Tutaambiwa yooote yaliyo hovyo na ambayo hayasitahili kusemwa. Wewe mahakamani ulishindwa KUJITETEA na siri kila siku zinavuja unavyotumika vibaya kama dodoki. Wewe sema tu yote usitishie humu,maana wenzako walitengeneza Mkanda wa ugaidi ukweli ukajulikana. Na wewe sema ukweli tu.
 
mbona mnahangaika sana? Kwani mmeshajua anachotaka kusema?

kijana hatuja jua ndiyo lakini kutoka na uzi fulani hapa jukwaani uliokuwa unahusu yeye deusi mallya na antoni diallo kupanga kutumia ajali ya wangwe kama sehemu ya mapambano ya harakati za kisiasa dhidi ya chadema,hapo ndipo tunaunganisha hoja nakupata jibu la moja kwa moja kuwa.yawezekana ni kweli deusi atakuwa amehongwa vijisenti ili achafue viongozi wa chadema kwa kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa chama.
"ila sitaki kuamini kuwa wewe deusi mallya umekuwa mtu wa kuhongwa na kukubali kutumika na mafisadi wa c.c.m kiasi hiki!"
 
Mkuu Deus Mallya, kwanza asante kwa kuamua kutaka kusema!.

Moja ya tabia za kiume kwa mwanamume ni kuwa na msimamo thabiti, msimamo imara, akiamua kitu, ameamua na anasimama nacho mpaka mwisho wake, na ikibidi kufa, anakufa na msimamo wake huku akiitwa shujaa!. Sasa wewe kama ni mwanamume na unazo tabia za kiume, ulipoamua kukaa kimya na kunyamaza, ni lazima uendelee kukaa kimya na kunyamaza mpaka mwisho!.

Hii imeenda mbali zaidi!


Hili tishio la oh mara ntasema, au wakati wa kusema umefika!, hizi ni tabia za kike!, mwanamume akiamua kusema, hasemi ntasema bali husema!. Mwanamke ndio huamua kutishia aseme au asiseme, na hata akitong..zwa anajijua kabisa amekubali, atajifanya hataki ili uonyeshe kuhangaika kumpata!.

Mkuu Pasco unajua hapa umewagusa wengi !
Najua unaweza kuweka list inayoeleweka na hasa ya Waheshimiwa.Naomba kukumbusha kuwa Jamii ya Wanafiki ndiyo yenye kuishi maisha ya Kiujanja kama hayo ya Kutishia ili kutikisa kibiriti kwa malengo fulani.
Unajua hata Mkuu wa Kaya alisema;


"Sizungumzi kwa utani nayajua ninayoyasema. Nilichoweka akiba ni kuwataja watu kwa majina. Wasidhani nikienda wizarani nikasema watu hawa wanakula rushwa wasidhani siwajui kwa majina, ninawajua; bali kwa sasa ninatoa muda kwa watu hao wajisahihishe. Mwenye masikio nadhani atakuwa amesikia," alisisitiza.



Raia Mwema - Mikwara hii ya Kikwete kwa wahalifu haisaidii


Hii ya wewe kutishia kuwa utasema, its as if ulilipwa kiasi fulani hapo mwanzo ili unyamaze, na ukanyamaza, sasa umeishiwa, unataka kuendelea kulipwa siku zote kwa kukaa kimya!, yaani ukimwa wako ndio ajira yako, ili uendelee kulipwa, unatishia kusema ili watishike na kukulipa tena ili usiseme, ukae kimya!.

Suala linaloumiza vichwa vya watu na kuendelea kwa Jamii kuhoja tukio ni kwa sababu ya hilo ulilolidokeza.
Kwa mtu anayefikiri Kauli ya kuweka akiba kwenye kuweka wazi Jambo linazua Maswali yasiyo na Majibu.

Tuchukue mfano Mdogo wa kipenzi Chako Edo- yeye aliweka wazi kuwa Tatizo lilikuwa Uwazi Mkuu wake.
Na hilo kwa watu wanaofirikiwa mpaka sasa watakuwa wamekwisha pata Majibu.

Mwakeyembe -Waziri
S.Siita usiseme!
na team mzima ........
Utaona kuwa pamoja na Kazi nzuri lakini nyuma ya Pazia kulikuwa jambo jingine!


Nakushauri, kama umeamua kweli kusema, amua moja na useme sasa!, hukupaswa kusema utasema, ulipaswa useme tuu tujue moja, kitendo cha kutishia nyau kuwa utasema, kinaweza kupelekea wale waliokulipa siku zote kukaa kimya, wakakuona you are not an asset, you are a liability which needs disposal kabla haijawa too risky or threat, hivyo ukanyamazishwa jumla!.

Ni ushauri tuu.

Asante.

Mkuu Pasco mara nyingi watu wanaoshiriki kazi haramu wako tayari kwa kila jambo.
 
Wewe pia una matatizo makubwa, pengine kuliko huyu mgonjwa wa akili.

Hapo hatuongelei fasihi tunaongelea kosa la jinai. Kosa la jinai huthibitika kwa kauli yenye ushahidi usio na shaka. Hivi nikikuuliza maswali haya hapa chini una jibu la maana?
1) Una uhakika gani kuwa ni kweli Malya kuna watu wanamtishia maisha
2) Kuna ugumu gani kusema kuwa ametishiwa na mwanachama wa CCM au CHADEMA?
3) Hao wanachama wa CHADEMA waliomtishia kwa nini hawataji majina yao?
4) Polisi walimhoji kabla ya kupelekwa mahakamani, kwa nini hizo siri asizitoe huko polisi kama aliwaogopa watuhumiwa?
5) Kesi ya jinai huwa haina mwisho, kwa maana ya muda. Kama kuna chochote kilimfanya wakati akihojiwa kwa mara ya kwanza ashindwe kuwataja watuhumiwa, na sasa yupo tayari kuwataja, kwa nini asipeleke taarifa hizo polisi ili kesi ianze upya?

NB: Ukishabikia maneno ya kijinga toka kwa mwendawazimu ni dhahiri nawe ni mwendawazimu.
Hiyo ni hatua ya pili ya kimahakama lakini ya hatua ya kwanza ni umma kuelewa andiko lake Deus Mallya kwanza kwa ufafanuzi wa kifasihi kama ilivyoonyesha na iwapo siyo kweli yeye yupo hapa jukwaani atakuja kukanusha.
 
- HA! HA1 HA! HA! HA! mbona mnaaanza kutoka mapovu kabla mwananchi hjasema lililotokea mnajua kumbe kilichotokea ha! ha!

Le Mutuz

Watu huwa wanasema mchawi akionekana wakati analoga/anawanga, basi huo uchawi wake hautofanya kazi. Na kwa mlinganisho huo basi, si huyu huyu malya last time kuna post imewekwa hapa kuwa wanatengeneza issue na dialo itoke kama ushahidi wa kuihusisha CDM na kifo cha Chacha Wangwe? Kama iligundulika na ikaletwa hapa, sasa anataka kusema nini tena na walishabainika? Sana sana ningemshauri atafute njia ya kumrudishia dialo hela yake, dili imebumburuka
 
Mkuu unaandika humu JF kututishia au? Mbona JF sio mahali pake? Usisemee humu JF. Nenda kwa DPP au kwa IGP au kwa Werema, au Jaji Mkuu. Hao ndo watakusaidia. Watayapima maneno yako, wakiona yanafaa kwa lolote watayachukulia hatua.
Kutishiwa mbona jambo la kawaida tu. Hata kuuawa, mbona jambo la kawaida tu. Hujasikia binti aliyefanyiwa unyama wa kutisha wiki ilopita halafu bado wakauchukua na uhai wake, na kumweka uchi mtaroni?
Usiogope, sema lakini semea mahali stahiki, na ni kwa hao nlokuambia. Kama ulifungwa kwa kuonewa, nenda kwa walio tofauti na serekali. Tafuta msaada, Haki za Binadamu. Usitishie watu na weye kuwa unajua kuchonga. Amka asubuhi, chonga sana ila chongea penyewe wala usipotee njia mchongo wako ukapotea tena.

Umempa live bila chenga,wanataka kuleta uwongo wao hapa JF kwa mpango wa Dialo!
 
Hivi jamani,,ndugu yangu Ben Saanane yuko wapi..,mbona simuoni akitokwa mapovu kwenye thread kama hizi...yaani Mzee wake anakaribia kupelekwa lupango na yeye amekaa kimya kama hayamuhusu..njoo uwaambie umma wa JF kuwa hatuhusiki na atakachosema Mallya ni uzushi.

Hurufu mbaya
 
Ulikua wapi siku zote?, tuiite nini hii? maana ni zaidi ya njaa na unafiki uliokubuhu,
Nyie mnaoekti uana siasa ni washenzi sana......

Anataka kuushangaz ulimwengu huyu kijana....
Hayo anayotaka "kuyaongea" sijui nitofauti nayale aliyoyatoa polisi kipindi kile ama!

Kuna kila dalili ya mtu kutumiwa hapa sio bure
 
Deus Mallya bora useme tu ukweli.. Chadema wamekutukana sana..Sasa hivi wanataka kukuua
 
Miaka mitatu jela baada ya wiki mbili msamaha kutoka kwa rais(taasisi) unayo mazito sana. Tulia. Usitumike. Ongea ukweli.
 
Huna lolote wewe mbwiga, ni njaa tu inayokusumbua.
Ni wazi kuna wanaokuona wewe ndo mtu sahihi kufanikisha malengo ya kisiasa katika kipindi hiki, na hasa kule tuendako 2015. Jihadhari nao sana ndugu yangu, kwa maana hao watu kama wanaweza kukutumia uende kinyume na kile ulichowahi kukieleza polisi na baadaye mahakamani ktk ile kesi, kesho hawatasita kukuundia zengwe ili wakufute kabisa kama lengo lao la kisiasa hutalitafanikiwa.

Heshimu utu wako, waheshimu wale wote waliopigana pamoja nawe wakati wa kesi yako.Linda hata heshima ya hakimu/jaji aliyesikiliza shauri lako na hatimaye kutoa hukumu aliyoitoa.

Usikubali kutumika kirahisi namna hiyo ndugu....Ebu tazama waliopata kutumiwa na hao walikupa wewe deal, leo hii wko wapi...wamwpata nini cha maana, baada ya kumaliza mission zao.
 
Back
Top Bottom