Wakati tunatekeleza majukumu yetu tukumbuke kuwa nasisi ni binadamu

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
16,054
11,557
Nilitembelea kituo cha wazee cha Kalwande Bukumbi mwaka jana ukweli wale wazee wanaishi maisha ya shida mno, sio hilo tu hata watumishi wao nao vilevile hali ni ya kukatisha tamaa. Nashukuru Mama JPM kwa msaada wa CRDB alienda angalau kuwajulia hali. Wengi wa wazee walioko pale wamefika pale kutokana na dhahama mbalimbali zikiwemo kufurumushwa kwa tuhuma za uchawi na wengine kuporwa mashamba yao na kutishiwa maisha hivyo kuamua kukimbilia au kuletwa kuhifadhiwa hapo. Tatizo haliko Bukumbu tu lipo Nungwi na kwingineko.

Alikuwepo mzee maarufu na rafiki yangu mkubwa Mzee Matonya, siku moja alifurumushwa na mkuu wa mkoa Yusufu Makamba alibebwa mzobemzobe hadi Dodoma, yule mzee hakukaa muda alifariki. Nilisikitika sana kwani nilizoea kutaniana nae hasa saa za jioni.

Wapo ombaomba hasa watoto wengi wanamakwao na hawaombi kuwa wanashida ni utundu tu na kutaka kusanifu watu, wapo kweli wanaomba wapate riziki, hawa ni vipofu wakoma viwete walemavu na wazee, hawa hawana namna ya kuishi zaidi ya kusaidiwa na jamii.

Binadamu tunaamini unapowasaidia wahitaji basi unapata thawabu na unapata baraka, siku za ijumaa wafanyabishara wengi hasa waislam hutoa misaada kwa wahitaji utakutana na msururu mrefu wa vipofu na wakoma wakiwa katika maduka ya wahindi na wapemba wakipewa misaada.

Nasikia kuna amri ya kuwafurumusha omba omba wote kisa kusafisha mji, kama ndio hivyo tunakosea sana, wengine wapo Dar kwa zaidi ya miaka thelathini unataka aende wapi? wengine walikuwa hukohuko Gezaulole na Nungwi njaa zimewakimbiza huko wakaja azikiwe na mnazi mmoja kutafuta riziki, hebu tuliangalie hili jambo kwa umakini tena umakini mkubwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom