Wakati Chato tunaendelea, basi tuiboreshe na Tanganyika - Tanga

4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
5,979
6,782
Wana jf heshima zenu zote nilishamkabidhi mungu bila kujali, dini, chama au umri.

Mheza kama waenda Tanga mjini ipo sehemu yaitwa TANGANYIKA kabla ya kufika MKANYAGENI, na kabla ya kufika BAGAMOYO, KILAPULA, PONGWE, MAWENI, KANGWE then kwa MINCHI to TANGA MJINI.

Sikuwahi jua chanzo cha jina TANGANYIKA, ila wenda pamebeba tafasiri kubwa kama sehemu ya Tanzania kuliko Chato, na jina tu lazima mashule wapeleke wanafunzi kujua historia ya sehemu husika,hivyo ni utalii tosha.

KWA nia njema Mh JPM tufanye Jambo muhim pale mfano

1. Ijengwe shule matata from form one to six
2. Ijengwe hospitali ya wilaya matata, maana Muheza haina hospitali ya wilaya tofauti na Tehule hospital
3. Wananchi wa pale Serikali toeni msahada wa kujengewa nyumba bora maana pale ni sehem ndogo sana na watu ni wachache
4. Bolesheni chuo cha utafiti pale mkanyageni maana kipo karibu na Tanganyika, na vyote mtakavyofanya hapo tumieni jina Tanganyika.

Mwisho, tafuta historia ya jina hili hapo maana patapata watalii wengi kwamba kabla ya kwenda AMBONI wataanzia hapo.

Chato na Tanganyika twende kwa pamoja
 
Tanga mbona miradi kibao

MUONKEANO WA DAMPO LA KISASA, NA STENDI MPYA YA MABUS TANGA​


 
Mkuu unaonaje hayo uliyoyasema yaanzie kule wilayani TANGANYIKA mkoani Rukwa kabla ya kuanzia kwenye hako kaTANGANYIKA kadogo ka hapo wilayani Muheza?

Au hii ni janja janja ya wanaMuheza kuomba maendeleo kwa bwana mkubwa ?

Kule wilayani Mkinga (barabara ya Tanga Horohoro) kuna sehemu panaitwa Zanzibar, nadhani na wao watakuja na hoja kama yako kuomba miradi ya maendeleo ielekezwe huko.

Nimependa ubunifu wa wana Tanga katika hili.

Kila la heri kwenu.
 
Mkuu unaonaje hayo uliyoyasema yaanzie kule wilayani TANGANYIKA mkoani Rukwa kabla ya kuanzia kwenye hako kaTANGANYIKA kadogo ka hapo wilayani Muheza?....
Mkuu sio janja janja inawezafanyika utafiti, wapi ni chimbuko la TANGANYIKA, maana zipo sehem huiga majina,na zingine ni chimbuko halisi so Sina shida na wazi lako
 
Tanganyika ilishaungana na Zanzibar ikazaliwa Tanzania, na leo rais wa Zanzibar yupo Tanzania kwa ziara ya siku 2.

Hatuwezi kurudi nyuma kuindeleza Tanganyika ambayo haipo.

Hicho hapo Mkanyageni kwa Bastola ni ukumbusho tuu.

Tanzania ni moja! Maendereo hayana vyama, uwe CCM uwe CUF au CHADEMA 😂
 
Tanganyika ilishaungana na Zanzibar ikazaliwa Tanzania, na leo rais wa Zanzibar yupo Tanzania kwa ziara ya siku 2....
Sawa Tanzania moja ila jua mkuu histolia haifutiki that kila mwaka twaenzi mapinduzi ya Zanzibar,muungano, nyerere day,japo hakuna karume day
 
Back
Top Bottom