Wakaniambia, 'Shemeji piga mzigo…'!

Wakaniambia, 'Shemeji piga mzigo…'!

Kama kawaida mkuu wa kazi napenda sana story zako hakika yafaa uwe muandishi wa vitabu au novel,una mastory
cherating-beach5_lunch-friends_gyscha-rendy-used-with-permission.jpg

walikuwa wawili na mzungu mmoja...............

nilikutana na binti huyu mwaka 1990 wakati huo nikikaa na kaka yangu maeneo ya mwenge. Siku hiyo nilikuwa nimetumwa maeneo ya ubungo na nilikuwa naendesha gari la kaka yangu aina ya toyota mark ii ambayo ilikuwa bado ina hali nzuri na mziki mnene. Nilikuwa nimepiga t-shirti na jinzi na miwani ya jua. Niliamua kupitia barabara ya chuo kikuu lengo langu likiwa ni kujaribu bahati yangu kama nitakutana na binti yeyote anayesubiri usafiri nimpe lifti na kujaribu kutupia nyavu.

Ilikuwa ni kawaida yangu kila nikitumwa na kaka na kupewa gari napitia barabara ya chuo kikuu lengo langu likiwa ni hilo la kuopoa vimwana na mara nyingi nilikuwa sikosi kimwana wa kumpa lifti na kumtongoza. Wapo niliokuwa nikiwapata na wale niliokuwa nikiwaona washamba nilikuwa nawapotezea.

Siku hiyo nilibahatika kumpata binti mmoja. Alikuwa ni mzuri hasa kwa sura na umbo na weupe unaoashiria kuwa mambo yake ni mazuri. Nilisimama na kumtupia salaam, na yeye bila kusita aliniitikia na ndipo nikamwambia kama anaelekea ubungo nimsogeze. Awali alisita lakini baada ya kumsisitiza alikubali kupanda nikaondoka naye. Njiani nilianza kumsomesha, hakuonekana kuwa mgumu, ingawa nilijishtukia kutokana na binti huyo kuonekana ni wa matawi.

Aliponiuliza ninaishi wapi na ninachofanya, nilimwambia ninaishi kwa kaka yangu ambaye ni mwanajeshi na nikamdanganya kwamba, ndio nimemaliza chuo kikuu mwaka uliopita na kwa sasa ninafanya kazi kama mwanadiplomasia pale wizara ya mambo ya nchi za nje. Nilimwambia kuwa, huwa nasafiri mara kwa mara nje ya nchi kwa shughuli za kikazi na kuonekana kwangu nchini ni mara chache sana. Aliponiliza kama huwa nasafiri nchi gani, nilimwambia, huwa natembelea zaidi nchi za maziwa makuu. Hata hivyo nilimwambia kwamba, ndio ninajipanga nitafute nyumba ili nihame kwa kaka yangu kwa kuwa ndio nimeanza kazi nilikuwa bado najipanga ingawa kaka yangu hataki nihame hapo kwake.

Kwa upande wake alinijulisha kwamba na yeye amesoma nchini uingereza na anafanya kazi katika ubalozi fulani wa mojawapo ya nchi za scandinavia (naomba nisiutaje huo ubalozi) na anaishi na wazazi wake ambapo baba yake ni mhadhiri hapo chuo kikuu. Alianza kunipigisha mastori yanayohusiana na mambo ya kidiplomasia ikabidi nimpotezee na kubadilisha stori ili asije akanishtukia.

Baada ya kumpa soma alikubali na kuniahidi nimtembelee hapo nyumbani kwao wiki ijayo mwishoni mwa juma ili tutoke out kwa ajili ya kufahamiana zaidi. Kwa kuwa simu za mkononi zilikuwa bado hazijaingia nchini alinipa namba ya simu ya nyumbani kwao. Tulipofika ubungo aliteremka na kushika hamsini zake akiniacha na mimi nikifanya shughuli iliyonipeleka hapo ubungo. Kwa muda mfupi nilioongea na yule binti alionekana kunipenda sana kwani hata wakati anashuka kwenye gari alinisisitiza sana tuonane hiyo wiki ijayo.

Ukweli ni kwamba nilikuwa sina kazi, na nilikuwa ndio nimemaliza kidato cha nne na kuangukia pua, yaani kwa kupata divisheni ya ziro. Wiki iliyofuata tangu nikutane na yule binti nilipata kazi ya kutembeza vitu na kuuza, maarufu kama promosheni. Siku hiyo nikiwa na furushi langu la vyombo na mwenzangu mmoja, yule binti aliniona. Alinikuta maeneo ya kijitonyama akiwa kwenye gari. Mimi sikumwona, na alinipigia honi na alipoona sisikii alishuka. Alinikimbilia huku akiniita jina. Niligeuka na kugundua kuwa ni yule mpenzi wangu wa chuo kikuu niliyempa lifti na kumpiga fix.

Nilibabaika sana kwa kweli. Ilibidi hata kabla hajanisemesha, nimwambie yule mwenzangu, ‘au labda ni nyumba hii hapa, maana nimechoka sana.’ yule binti akiwa ameshikwa na butwaa aliniuliza mbona niko kule na furushi kubwa. Nilimwambia, ‘ninamsindikiza huyu boy shamba wetu kwao. Ameacha kazi nyumbani nataka nimkabidhi kwa kaka yake. Ndio anajaribu kunionyesha nyumba, lakini naona kama naye kapasahau.’ nilimjibu nikiwa nimebabaika sana.
‘oh, nilishangaa kukuona na hilo furushi. Je nikupeni lifti ili tutafute hiyo nyumba yenyewe?’ aliniuliza. Nilimwambia asisumbuke, tutatafuta hiyo nyumba na tutaipata tu. Aliniaga akionyesha kutoridhishwa na maelezo yangu.

Baada ya tukio lile niliona kazi ile haifai na nikaamua kuiacha. Nilipata kazi kwenye mghahawa mmoja uliopo mjini karibu na posta. Nilianza kazi pale kama mhudumu yaani waiter. Siku moja nikiwa nachukua order ya chakula waliingia wateja, sikuwatazama vizuri kwa sababu ya kashkash ya kazi mchana huo. Nilikwenda katika meza yao ili kuchukua order yao. Nilipofika pale walipokaa hao wateja nilikutana uso kwa uso na yule mpenzi wangu wa chuo kikuu. Niliishiwa pozi. Niligeuka haraka na kutaka kuondoka. Nilikuwa nataka kukimbilia jikoni. Lakini nilikuwa nimechelewa. Kwani aliniita kwa jina na kusema, ‘usijali, najua kinachoendelea. Ndio maana nimeamua kuja kula hapa. Chukua order yetu ya chakula na kuwa tu huru, kwani tangu wakati wa promosheni ya vyombo, nilikuwa najua….’

aliposema hivyo aliwatazama wale wenzake. Mmoja wao aliniambia, ‘shem usijali piga mzigo, mapenzi kitu kingine na kazi zetu kitu kingine.’ nilienda jikoni, lakini sikurudi tena. Yaani ilikuwa ni kashfa kubwa ambayo sitakuja kuisahau mpaka leo hii niko na mama ngina. Hadi leo sijui yule binti yuko wapi. Maana niliacha kazi na kwenda kusoma mkoani arusha. Nashukuru hakujua ninaishi wapi pale mwenge. Hata hivyo nilijifunza mengi, lakini kubwa zaidi nilijifunza kujiamini na ndio maana hadi leo mtu akiniliza nakaa wapi na ninafanya kazi gani ninamwambia ukweli kwamba ninaishi mwanayamala kwa kopa na ninafanyakazi ya kuuza kahawa mjini.

nivea, lisa, lara 1, king'asti, na mwaj, ole wenu mtoe comment kwenye hii maneno....................lol
 
Heheheheeh! Ila kwa Kibosho na Machame geloz mlikuwa hamtuambii kitu. Ni kama tulikuwa tumewawowa asee........ Dah umenikumbusha ile mibweni kama wodi LOL

Jamani hata Watu wa Moshi tech ..wanajisifu kwa bata....Moshi tech ya mwaka gani? Maana tuliosoma ukanda huo tunawajuwa Moshi Tech..kama washamba tu ...wakulima ...mafundi mchundo ....manjemba! Wao walikuwa wanajuwa Zaidi hesabu !

Miaka ya mwisho ya 80 shule lilikuwa inaongoza kwa wajanja na vipanga Moshi ni ...

Old Moshi Secondary.........barua zetu za kuomba debe zolikuwa hazikataliwi...Weru Weru ,Machame,Masama,Mawenzi na majengo ( disco la mchana ) ,Kibosho Girls,Ashira,Kiraeni ,Namfua,Marangu Sec....hawa watoto walikuwa ni watamu Sana.....Leo hii tukikutana nao wamekuwa wamama wa enzi zetu wengine ma professor,makatibu wakuu ,wabunge etc....wengine wapo diaspora tunaonana nao

Rekodi ya old Moshi ilikuwa kwa karibu inafuatiwa na ILBORU....,UMBWE...,LYAMUNGO..,...labda ndio MOshi Tech kwa mbali......na shule Kama KOLILA, KILI BOYS .....

kIBOHEHE walikuwa wazee wa vurugu!!!
 
Umeonaeeeh...sasaivi tushakuwa mafisadi..full mavitambi...blues lenyewe halichezeki..kiduku ndo hata kusimamia unyayo hakiendi...sana sana ingegongwa twist ya nguvu.........

hahahahhahhhh! sasa hivi ndo mwendo wa zilipendwa kwa kwenda mbele. dah ila nimemkumbuka mama Tungaraza na yule mwl wenu wa Kimbulu mbaba hivi alikuwaga mzee nyumba yake ilikuwa hapa mwisho kabisa karibu na njia ya kuendea rau alikuwa ana watoto wengi utafikiri mkewe kila j1 alikuwa anaenda labour.
 
Mi nimesoma Moshi Technical bana. Wazee wa maovaroli. Kibosho geloz ndo walikuwaga wake zetu.:becky::becky::becky:
jamani jamani moshi tech huko walikuwa wanasoma wasukuma watu wa bondo harage!!
hawa hata mvuto hatukuwa nao manake walikuwa wazee wa vyuma. unakumbuka ule utani wetu enzi hizo eti mvulana wa mosh tech akikutongozo utamsikia anasema

''dahdah nimekudohndhokhea!!''!
 
Wewe mwanamke umenikumbusha mbali saana..maana...mmhh!..ngoja mengine nimezee najua mzee wa Umbwe Asprin anasubiri kusikia ilikuwaje....

lkn twende pm kwanza uniambie yule handsome wenu social yuko wapi siku hizi?? ama kesha vuta manake alikuwa kazaliwa jamani acheni mama yake apewe hongera lol!
 
Acha umbea, kwanza hii stori hainihusu kabisa, nilisimuliwa na afki yangu wa ukwee ninayeishi naye huku kwetu uswazi.....
Mkuu mbona hii kitu inakuja kwenye mazingira yako siyo mjengoni hapo mkuu??
 
Ukiwa mwanaume kabwela hakika utaendelea kula kwa macho tu...mla nyama ni yule aliyechonga meno!!
 
aah wapppy!!
enzi zile kule kukumbatiwa tu na kumlalia mvulana kifuani ilitosha kabisa kumfanya mschana aridhike kabisa tena mkitoka hapo mabarua, post cards na card za kawaida zinafuata za i love you, iss you best wishes etc.

Kabisa tulikuwa tunacheza music tukimaliza , tayari amekuwa mpenzi wako, lakini tulikuwa hatufanyi kitu kinaitwa mapenzi, lakini watoto wa miaka hii , wanazaa wadogo sana, hasa kule anakoka kaka Mtambuzi, mwananyamala kwa kopa , ni hatari unakuta mtoto kabeba mtoto, utadhani ni mdogo wake, kumbe mwanae Loh!
 
Hahahahahahaha! kaka Mtambuzi umenifanya nicheke mbaya, maana ulipokutwa pale getini ulitambani ardhi ipasuke, nadhani hata underware ilikubana kwa aibu.
Na ni kawaida kwa mwanamke usipomdanganya kidogo humpati Ng'o, lazima useme uongo kiasi, wewe unafikiri ungemwambia umeangukia pua, halafu upo upo tu, angekukubali/ tena angekuangalia juu mpk chini halafu angeondoka zake. Na siku zote mwanaume kuwa na kitu ni security kubwa sana kwake, inamfanya ajiamini sana, na anakuwa na uwezo wa kuamua jambo, lakini akiwa hana Loh, hata umtie singi hakujibu, ananyweaaaaaaaaaaaaaaa!!!
 
Nimecheka sana bada ya kusoma huu uzi kwani inanikumbusha kitu kama hiki ambacho kilimkuta mshikaji wangu wa karibu sana ambae kwa sasa ni DJ katika moja ya redio zinazobamba hapa mjini. Enzi hizo tukiwa pangu pakavu, alijifanya kumtokea dada mmoja hivi ambae ni wa matawi anaishi mitaa ya Masaki. Jamaa yangu akamwambia yule dada kwamba anaishi Upanga na anafanya kazi nzuri tu mjini Dar. Yule dada akamuamini mshkaji na wakapeana contact kwa ajili ya kupanga kuonana zaidi. Jamaa ana shangazi yake anaishi Sinza. Huyu Shangazi mtu alivyoona mwanae (mshkaji wangu) kwamba hana kazi, ili aweze kupatia hela kidogo za kusukuma maisha akamuomba aende Sinza akamsaidie kupaka rangi nyumbani kwake ndani. Jamaa akiwa hana hili wala lile, akafika siku hiyo na kuvaa maguo ya kazi na kuanza kazi na Shangazi mtu akamuaga kwamba anatoka na atarudi mida ya mchana hivyo aendelee tu na kazi. Jamaa akaanza kuchapa kazi, nguo na mpaka mwili ukawa umejaa marangi rangi na alivuja jasho haswa. Mchana ukafika, Shangazi akarudi na mgeni ambae ni rafiki na huyo Shangazi katika biashara zao huko. Shangazi kaingia ndani jamaa yupo bize na kazi, Shangazi akamwambia mgeni wake kwamba kuna ka-ujenzi kanaendelea hapo nyumbani, so akipenda wakaucheki wote. Basi yule rafiki mtu akakubali. Jamaa(mshaki wangu) alikuwa amewapa mgongo walivyoingia, akaitwa ageuke ili waonane na mgeni watambulishe, hamadi si ndo kukutana uso kwa uso na yule dada aliyemuongopea na kujikweza....jamaa aliona aibu na hakumtafuta tena yule dada na wala hakutaka kusikia habari zake.
Sasa hii yako Mtambuzi imenikumbusha hii stori ya jamaa yangu na nimecheka sana kwa kweli. Thanks for making my day
 
Last edited by a moderator:

chwechinyong kule kwetu Mwananyamala kwa Kopa tunaita SELEKA ZA WALAMI, nakumbuka tulikuwa tunatoka Mwananyamala kwa Kopa na kuingia viunga vya Regency Estate pale Viktoria kuwania vibinti vya geti kali kwa kujifanya watoto wa Masaki........

Duh, kweli old is gold aisee..........
 
Last edited by a moderator:
Kabisa tulikuwa tunacheza music tukimaliza , tayari amekuwa mpenzi wako, lakini tulikuwa hatufanyi kitu kinaitwa mapenzi, lakini watoto wa miaka hii , wanazaa wadogo sana, hasa kule anakoka kaka Mtambuzi, mwananyamala kwa kopa , ni hatari unakuta mtoto kabeba mtoto, utadhani ni mdogo wake, kumbe mwanae Loh!
khaaaa! wakikusikia wenyewe wa mwananyamala utakoma.

ukweli uliowazi ni kwamba watoto wa siku hizi hawajui kula raha kabisaa. miaka yetu ilikuwa unakuwa na rafiki wa kalam basi mnaandikiana hadi unaona raha, tena mkitumiana makadi na post cards unapata ujiko n wala hutamani kuwa nae karibu ili uzidi kupata makadi na mabarua.

ukimaliza shule mnabaki kuwa marafiki wa kutembeleana na kwenda outing tena harushan maji wala nn, utakomaa na kuiba kidogo kidogo kwa umakini ili umalize chuo. na hapo ukimaliza utataka urudi mtani upange kwanza geto lako mwenyewe ule bata full kujiachia kwa raha, si outin s uhuru si kuvaa hadi mtu unachoka ndo unasema sasa niolewe. so unaolewa tayari ushakula life sana tu, ukiingia ndani huadithiwi sasa hawa wa siku hizi hata miraha ya uish peke yao hawaijui.
 
Kuna rafiki yangu mwengine alimpata binti flani wa matawi sana na babaake anamiliki hoteli moja kubwa kwa enzi hizo jijini Dar. Jamaa alikutana na binti kwenye harusi ya ndugu yake, wakakubaliana na jamaa alimzimia mbaya yule binti. Basi jamaa ilikuwa karibia kila siku anatoka maeneo ya kwako migomigo na kwenda mpaka Mbezi beach kumsubiria binti atoke kwao ndani ili amuone tu, enzi hizo ni simu za ndani tu zinatumika no simu za mkononi, so jamaa alikuwa anakula glue mpaka basi..mwishowe walinzi wa ile mitaa wakamzoea maana mwanzo walikuwa na wasiwasi. Mwisho wa yote, tunasema mbuzi wa masikini hazai na hata akizaa basi atazaa tasa, yule binti alisafiri kwenda Uganda na ndo ikawa mwanzo na mwisho wa kuonana na mshkaji ingawa kwa siku za mwanzo ambazo yule binti alisema angekaa huko zilipoisha jamaa alienda kutega mingo zake but with no fruitful outcomes...

Kiukweli, old is gold Mtambuzi
 
Yaaaaaaaaaaaaani! umenikumbusha mbali sana ya kupanga geto, mnashindana kuweka vitu vya thamani ndani, nakumbuka frige yangu ya kwanza nilinunuliwa hapo AC GOMES kwenye jengo la Ali hasan mwinyi, sijui sasa hivi linaitwajwe, liko mkabala na mahakama ya kisutu, na kabati languo . nilikuwa nakaaa mitaa ya sinza karibu na flat za BOT, we acha tu, nilikuwa najiona ile mbaya, nikapata kibarua Tanesco , unanitaka. hahahahaah, Loh.
 
Kuna rafiki yangu mwengine alimpata binti flani wa matawi sana na babaake anamiliki hoteli moja kubwa kwa enzi hizo jijini Dar. Jamaa alikutana na binti kwenye harusi ya ndugu yake, wakakubaliana na jamaa alimzimia mbaya yule binti. Basi jamaa ilikuwa karibia kila siku anatoka maeneo ya kwako migomigo na kwenda mpaka Mbezi beach kumsubiria binti atoke kwao ndani ili amuone tu, enzi hizo ni simu za ndani tu zinatumika no simu za mkononi, so jamaa alikuwa anakula glue mpaka basi..mwishowe walinzi wa ile mitaa wakamzoea maana mwanzo walikuwa na wasiwasi. Mwisho wa yote, tunasema mbuzi wa masikini hazai na hata akizaa basi atazaa tasa, yule binti alisafiri kwenda Uganda na ndo ikawa mwanzo na mwisho wa kuonana na mshkaji ingawa kwa siku za mwanzo ambazo yule binti alisema angekaa huko zilipoisha jamaa alienda kutega mingo zake but with no fruitful outcomes...

Kiukweli, old is gold Mtambuzi
chwechinyong, mie hizo za kucomeshwa mahindi nishachomeshwa sana.
Nakumbuka enzi hizo mwaka 1988 niliwahi kuchomeshwa mahindi na shori mmoja wa mitaa ya mikocheni mpaka basi, sitamsahau mwanaizaya yule, maana nilisaga lami kumfuatilia nikaishia kula kipondo kutoka kwa kaka zake...........
 
Last edited by a moderator:
Dah Bro ulitia huruma sana hapo mwishoni...... Ila Kaka yako alikukatia uhondo wa gari mapema...... Ila imegeuka na kuwa historia tamu, raha kukumbuka tu..... Halafu ulivyofika Arusha ukaenda kuzua kasheshe jingine hahahaha we umeshindikana kweli
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom