Nyalotsi
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 6,989
- 5,069
Nimekumbuka rafiki yangu mmoja alikuwa yatima analelewa na mzee mmoja maarufu kwa biashara home. Jamaa aliopoa mtoto wa mkurugenzi wa halmashauri na kumwambia yeye ni mtoto wa yule mzee na wanatokea mwanza. Siku moja yule demu katoka kanisani wakapitia madukani kufanya shoping hamadi kakutana na yule jamaa anasomba mizigo dukani aafu wanagonga kiluga cha wakukaya. Demu alivyotoka pale akaenda kuuliza kwa watu jamaa ni wa wapi? Akafichuliwa siri na hao masela, toka siku hiyo akakata mazoea na jamaa ila mzigo alishaliwa. Tulikuwa la sita kipindi hicho na demu alikuwa la saba.