Wakaniambia, 'Shemeji piga mzigo…'!

Wakaniambia, 'Shemeji piga mzigo…'!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
Cherating-Beach5_Lunch-friends_gyscha-rendy-used-with-permission.jpg

Walikuwa wawili na mzungu mmoja...............

Nilikutana na binti huyu mwaka 1990 wakati huo nikikaa na kaka yangu maeneo ya Mwenge. Siku hiyo nilikuwa nimetumwa maeneo ya Ubungo na nilikuwa naendesha gari la kaka yangu aina ya Toyota Mark II ambayo ilikuwa bado ina hali nzuri na mziki mnene. Nilikuwa nimepiga T-shirti na Jinzi na miwani ya jua. Niliamua kupitia barabara ya Chuo Kikuu lengo langu likiwa ni kujaribu bahati yangu kama nitakutana na binti yeyote anayesubiri usafiri nimpe lifti na kujaribu kutupia nyavu.

Ilikuwa ni kawaida yangu kila nikitumwa na kaka na kupewa gari napitia barabara ya Chuo Kikuu lengo langu likiwa ni hilo la kuopoa vimwana na mara nyingi nilikuwa sikosi kimwana wa kumpa lifti na kumtongoza. Wapo niliokuwa nikiwapata na wale niliokuwa nikiwaona washamba nilikuwa nawapotezea.

Siku hiyo nilibahatika kumpata binti mmoja. Alikuwa ni mzuri hasa kwa sura na umbo na weupe unaoashiria kuwa mambo yake ni mazuri. Nilisimama na kumtupia salaam, na yeye bila kusita aliniitikia na ndipo nikamwambia kama anaelekea Ubungo nimsogeze. Awali alisita lakini baada ya kumsisitiza alikubali kupanda nikaondoka naye. Njiani nilianza kumsomesha, hakuonekana kuwa mgumu, ingawa nilijishtukia kutokana na binti huyo kuonekana ni wa matawi.

Aliponiuliza ninaishi wapi na ninachofanya, nilimwambia ninaishi kwa kaka yangu ambaye ni mwanajeshi na nikamdanganya kwamba, ndio nimemaliza chuo kikuu mwaka uliopita na kwa sasa ninafanya kazi kama mwanadiplomasia pale wizara ya mambo ya nchi za nje. Nilimwambia kuwa, huwa nasafiri mara kwa mara nje ya nchi kwa shughuli za kikazi na kuonekana kwangu nchini ni mara chache sana. Aliponiliza kama huwa nasafiri nchi gani, nilimwambia, huwa natembelea zaidi nchi za Maziwa makuu. Hata hivyo nilimwambia kwamba, ndio ninajipanga nitafute nyumba ili nihame kwa kaka yangu kwa kuwa ndio nimeanza kazi nilikuwa bado najipanga ingawa kaka yangu hataki nihame hapo kwake.

Kwa upande wake alinijulisha kwamba na yeye amesoma nchini Uingereza na anafanya kazi katika ubalozi fulani wa mojawapo ya nchi za Scandinavia (naomba nisiutaje huo ubalozi) na anaishi na wazazi wake ambapo baba yake ni mhadhiri hapo Chuo kikuu. Alianza kunipigisha mastori yanayohusiana na mambo ya kidiplomasia ikabidi nimpotezee na kubadilisha stori ili asije akanishtukia.

Baada ya kumpa soma alikubali na kuniahidi nimtembelee hapo nyumbani kwao wiki ijayo mwishoni mwa juma ili tutoke out kwa ajili ya kufahamiana zaidi. Kwa kuwa simu za mkononi zilikuwa bado hazijaingia nchini alinipa namba ya simu ya nyumbani kwao. Tulipofika Ubungo aliteremka na kushika hamsini zake akiniacha na mimi nikifanya shughuli iliyonipeleka hapo Ubungo. Kwa muda mfupi nilioongea na yule binti alionekana kunipenda sana kwani hata wakati anashuka kwenye gari alinisisitiza sana tuonane hiyo wiki ijayo.

Ukweli ni kwamba nilikuwa sina kazi, na nilikuwa ndio nimemaliza kidato cha nne na kuangukia pua, yaani kwa kupata divisheni ya ziro. Wiki iliyofuata tangu nikutane na yule binti nilipata kazi ya kutembeza vitu na kuuza, maarufu kama promosheni. Siku hiyo nikiwa na furushi langu la vyombo na mwenzangu mmoja, yule binti aliniona. Alinikuta maeneo ya Kijitonyama akiwa kwenye gari. Mimi sikumwona, na alinipigia honi na alipoona sisikii alishuka. Alinikimbilia huku akiniita jina. Niligeuka na kugundua kuwa ni yule mpenzi wangu wa Chuo Kikuu niliyempa lifti na kumpiga fix.

Nilibabaika sana kwa kweli. Ilibidi hata kabla hajanisemesha, nimwambie Yule mwenzangu, ‘au labda ni nyumba hii hapa, maana nimechoka sana.' Yule binti akiwa ameshikwa na butwaa aliniuliza mbona niko kule na furushi kubwa. Nilimwambia, ‘ninamsindikiza huyu boy shamba wetu kwao. Ameacha kazi nyumbani nataka nimkabidhi kwa kaka yake. Ndio anajaribu kunionyesha nyumba, lakini naona kama naye kapasahau.' Nilimjibu nikiwa nimebabaika sana.
‘Oh, Nilishangaa kukuona na hilo furushi. Je nikupeni lifti ili tutafute hiyo nyumba yenyewe?' aliniuliza. Nilimwambia asisumbuke, tutatafuta hiyo nyumba na tutaipata tu. Aliniaga akionyesha kutoridhishwa na maelezo yangu.

Baada ya tukio lile niliona kazi ile haifai na nikaamua kuiacha. Nilipata kazi kwenye mghahawa mmoja uliopo mjini karibu na posta. Nilianza kazi pale kama mhudumu yaani waiter. Siku moja nikiwa nachukua order ya chakula waliingia wateja, sikuwatazama vizuri kwa sababu ya kashkash ya kazi mchana huo. Nilikwenda katika meza yao ili kuchukua order yao. Nilipofika pale walipokaa hao wateja nilikutana uso kwa uso na yule mpenzi wangu wa Chuo Kikuu. Niliishiwa pozi. Niligeuka haraka na kutaka kuondoka. Nilikuwa nataka kukimbilia jikoni. Lakini nilikuwa nimechelewa. Kwani aliniita kwa jina na kusema, ‘usijali, najua kinachoendelea. Ndio maana nimeamua kuja kula hapa. Chukua order yetu ya chakula na kuwa tu huru, kwani tangu wakati wa promosheni ya vyombo, nilikuwa najua….'

Aliposema hivyo aliwatazama wale wenzake. Mmoja wao aliniambia, ‘shem usijali piga mzigo, mapenzi kitu kingine na kazi zetu kitu kingine.' Nilienda jikoni, lakini sikurudi tena. Yaani ilikuwa ni kashfa kubwa ambayo sitakuja kuisahau mpaka leo hii niko na mama Ngina. Hadi leo sijui yule binti yuko wapi. Maana niliacha kazi na kwenda kusoma mkoani Arusha. Nashukuru hakujua ninaishi wapi pale Mwenge. Hata hivyo nilijifunza mengi, lakini kubwa zaidi nilijifunza kujiamini na ndio maana hadi leo mtu akiniliza nakaa wapi na ninafanya kazi gani ninamwambia ukweli kwamba ninaishi Mwanayamala kwa Kopa na ninafanyakazi ya Kuuza kahawa mjini.


nivea, Lisa, lara 1, King'asti, na mwaJ, ole wenu mtoe comment kwenye hii maneno....................LOL
 
mimi tu naruhusiwa kutoa comment enh!
ahahahahhah King'asti enh sisi hatujatajwa bana tusomngeshe kama kadawia!
we mzeee ni nouuuumer!
 
mimi tu naruhusiwa kutoa comment enh!
ahahahahhah King'asti enh sisi hatujatajwa bana tusomngeshe kama kadawia!
we mzeee ni nouuuumer!
Acha umbea, kwanza hii stori hainihusu kabisa, nilisimuliwa na afki yangu wa ukwee ninayeishi naye huku kwetu uswazi.....
 
kumbe umetajwa?best basi we usiongee kitu manake babako leo ana hasira kama nin!
ila nafkir BADILI TABIA hajatajwa
so hebu kuja huku uone shost huyu mzee alivo na baraaaaaaaaaaa!
 
Last edited by a moderator:
kumbe umetajwa?best basi we usiongee kitu manake babako leo ana hasira kama nin!
ila nafkir BADILI TABIA hajatajwa
so hebu kuja huku uone shost huyu mzee alivo na baraaaaaaaaaaa!
Sasa ndio unapigishia upatu?
Binti una nongwa wewe, hebu acha ushakunaku mweh...............!
 
mkuu mi nikajua umepiga ule mzigo wenyewe haswaaaa!

yani srii some ehn?ahahahhahhahaha anaweza ikawa huyu mzee hafai hata kulumangia huyu!we muulize tu vizuri hata kwa pm atakupa mkanda mzima ulikuwaje!
 
Sasa ndio unapigishia upatu?
Binti una nongwa wewe, hebu acha ushakunaku mweh...............!

ushakunaku muhimu babe wee!kusutwa sunna!
na unisute kwanza una huo ubavu!
jeshi langu si walijua lakini!
tulikuwa martenity leave tumerudi mazima!oh!
 
Lols...here we go again!.. mzee wa ununio ndani ya nyumba....ebwana nimecheka kwa sauti!
Kama kuna dhambi wanaume itatupeleka motoni ni kudanganya kazi tunazofanya wakati wa kuomba kikojoleo!
Pole sana bro Mtambuzi ..nimeyaona machungu yako.............Ila kumbuka saa zingine kuna zali la Mentali..............
 
Last edited by a moderator:
Lols...here we go again!.. mzee wa ununio ndani ya nyumba....ebwana nimecheka kwa sauti!
Kama kuna dhambi wanaume itatupeleka motoni ni kudanganya kazi tunazofanya wakati wa kuomba kikojoleo!
Pole sana bro Mtambuzi ..nimeyaona machungu yako.............Ila kumbuka saa zingine kuna zali la Mentali..............
Yaani SnowBall ilikuwa ni noumer mbaya, maana kimwana alikuwa ni mrembo hasa nikajua bila kutumia gia kubwa sitoweza kumpata, duh, sikujua kwamba mrembo ana exposure, nikaangukia pua..............
 
Last edited by a moderator:
mkuu nimecheka sana hasa hapa 'ninamsindikiza huyu boy shamba wetu kwao. Ameacha kazi nyumbani nataka nimkabidhi kwa kaka yake. Ndio anajaribu kunionyesha nyumba, lakini naona kama naye kapasahau.' unamsindikiza kwa miguu kiatu vumbu jasho ndembe ndembe,Nilikuwa nataka kukimbilia jikoni kwani we mpishi useme ulikuwa unaunguza?? pole sana mkuu
hata ukijiamini bila kuwa mkweli toka mwanzo bado tatizo linaweza kuwa pale pale ndio maana Mungu alisema kabisa usiseme wala kushuhudia uongo,

kw mazingira hayo mkuu ukweli peke yake ndio ungekuokoa (
The Truth will set you free)
 
Ha ha ha ha ha...mkuu hizi zimetukuta sana enzi zile tunasoma..wakati tukiwa o-level, mfano tukienda Weruweru kwa akina gfsonwin kuruka debe...full kujisifia kuwa tunasoma PCB (enzi hizo bonge la combination)...Mara unachanganyia like ila Commerce inazingua na Book Keeping ndo kabisa hatuna walimu wa kutosha..sasa binti akijiuliza PCB yenye Commerce na Book keeping ni ipi?..ebwana wee lazima akukimbize tu..anajua wewe bado njuka...........

Yaani SnowBall ilikuwa ni noumer mbaya, maana kimwana alikuwa ni mrembo hasa nikajua bila kutumia gia kubwa sitoweza kumpata, duh, sikujua kwamba mrembo ana exposure, nikaangukia pua..............
 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka kuna gazeti lilikuwa linaitwa Jitambue lilikuwa linaandika habari za saikolojia, kipengele kimojawapo kilikuwa ni jinsi NILIVYOFEDHEHEKA. Story kama yako zilikua nyingi. Good story, umenikumbusha mbali sana.
 
Ha ha ha ha ha...mkuu hizi zimetukuta sana enzi zile tunasoma..wakati tukiwa o-level, mfano tukienda Weruweru kwa akina gfsonwin kuruka debe...full kujisifia kuwa tunasoma PCB (enzi hizo bonge la combination)...Mara unachanganyia like ila Commerce inazingua na Book Keeping ndo kabisa hatuna walimu wa kutosha..sasa binti akijiuliza PCB yenye Commerce na Book keeping ni ipi?..ebwana wee lazima akukimbize tu..anajua wewe bado njuka...........
umenikumbusha mbali sana yaani khaaa!
 
kondoo anajileta mwenyewe halafu wewe simba unamwachia aende zake!!! :nimekataa kwenye miti __________. naomba unitumie namba yake
 
Dah hakika nimecheka na kujifunza kuwa mkweli na kujiamini.
Kuna mtu ongo
 
mkuu nimecheka sana hasa hapa 'ninamsindikiza huyu boy shamba wetu kwao. Ameacha kazi nyumbani nataka nimkabidhi kwa kaka yake. Ndio anajaribu kunionyesha nyumba, lakini naona kama naye kapasahau.' unamsindikiza kwa miguu kiatu vumbu jasho ndembe ndembe,Nilikuwa nataka kukimbilia jikonikwani we mpishi useme ulikuwa unaunguza?? pole sana mkuu
hata ukijiamini bila kuwa mkweli toka mwanzo bado tatizo linaweza kuwa pale pale ndio maana Mungu alisema kabisa usiseme wala kushuhudia uongo,

kw mazingira hayo mkuu ukweli peke yake ndio ungekuokoa (
The Truth will set you free)
Eh, bwana Jiwe Linaloishi, mie enzi zangu nilikuwa mzee wa seleka kwa kuwania vibinti, yaani nilikuwa hodari wa kutega mitego balaa na ikipachuka nahama kambi.

Nilikuwa nacheza na maeneo ya Chuo Kikuu, Mikocheni na Kawe kwa wazungu, na mzee mzima nina Mark II ya Mjeda mbona vimwana wa geti kali walinikomaje...........

Acheni tu nipumzike kwa sasa maana nimeona mengi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom