dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,496
- 3,461
Leo Jumatatu Desemba 23, 2019 Kampuni ya Vodacom Tanzania imetangaza kujiuzulu kwa wakurugenzi wawili Andries Delport na Till Streichert kuanzia Mei na Juni 2020.
Wakurugenzi wawili wa bodi ya kampuni ya Vodacom Tanzania; Andries Delport na Till Streichert wametangaza kujiuzulu.
Tangazo lililotolewa na kampuni hiyo leo Jumatatu, Desemba 23, 2019 imesema Delport atajiuzulu Mei 14, 2020 wakati Sreichert akitarajiwa kujiuzulu Juni 30, 2020 au muda wowote kabla ya tarehe hiyo.
Kabla ya kuingia Vodacom Novemba 2017, Till alikuwa mjumbe wa bodi ya kampuni ya Safaricom ya Kenya kuanzia Agosti 2017.
Wakurugenzi hao wote walikuwa wafanyakazi wa Vodacom Group ya Afrika Kusini. Wakati Till akiwa ofisa mkuu fedha wa kampuni hiyo kuanzia Februari 2014 Delport alikuwa mkuu wa kitengo cha teknolojia.
Akiwashukuru kwa mchango walioutoa kwa muda waliohudumu, katibu wa Vodacom Tanzania, Caroline Mduma amesema: “Bodi inawashukuru na kuwatakia mafanikio mema katika shughuli zao.”
Wajumbe hao wametangaza kujiuzulu ikiwa ni miezi mitano tangu aliyekuwa mwenyekiti wao, marehemu Ali Mufuruki kufanya hivyo.
Chanzo: Mwananchi