Bodi ya Utalii Tanzania: Hatujamtuma Mwijaku Kutangaza Utalii Mitaani Ujerumani

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,114
49,840
Bodi ya Utalii imemkana Mwijaku 😂😂😂

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesema haijamtumia wala kumtuma mtangazaji na mwigizaji, Mwemba Burtony maarufu kama Mwijaku nchini Ufaransa kutangaza utalii mitaani, akiwa balozi wa utalii kwa niaba au kwa gharama za Serikali.

Katika taarifa iliyotolewa na TTB, imesema mwaka huu TTB ilishirikiana na Sekta Binafsi kwenye maonyesho ya utalii ya Ufaransa ambayo yalifanyika kuanzia Oktoba 03 hadi 05, 2023 na ilikwenda na kampuni 12 ikiwemo kampuni ya Asha Tours EK ambayo ndiyo ilimgharamia Mwijaku kwenda kufanya utangazaji wa kampuni yake inayofanya biashara ya utalii yenye makao makuu Hamburg, Ujerumani.

1696874125175.png

Mwijaku

“TTB inakanusha kumtumia Mwijaku na inatoa tamko kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote asiye na dhamana ya kutangaza wala kuhamasisha utalii kwa mujibu wa sheria za Tanzania na taratibu zilizowekwa.” imesema taarifa.

Aidha, Bodi ya Utalii imewataka watu wote kuzingatia sheria kwenye utoaji wa taarifa au utangazaji na uhamasisha wa utalii ndani na nje ya nchi.

Mwijaku.jpg


Swali.
Kwani mtu akiamua kutangaza Utalii ni lazima atumwe na Bodi ya Utalii? Akili za Kijima ni tatizo jingine kubwa Tanzania.
 
Ninachoona wanaweka ambo sawa kwakua mwijaku hakawii kusema kagharamiwa na serikali kwahyo na wao wanajitetea. Kwenye swala la kutangaza utalii sio lazima awe mwijaku yeye akifanya ni kwa kupenda kwake.
 
Hakuna haja ya salamu.

Nimesoma hii barua. Nikauliza Bwijaku ni nani nikaambiwa ni mtangazaji anatangaza Utalii ufaransa. Bodi ya Utalii yasema haijamtuma. Nikajiuliza sikupata majibu.
Screenshot_2023-10-09-19-29-27-664_com.instagram.android~2.jpg
 
Back
Top Bottom