Wajinga huchanganya english na IQ

RoadLofa

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
1,347
2,957
Huwa na shangaa sana napokutana na watu wakimsifia mtu anayeongea kiingereza na kumheshimu kisha kumdharau asiyejua kuongea hiyo lugha.

Wanashindwa kuelewa kwamba kiingereza ni lugha tu kama lugha nyingine japo ni international language kama kiswahili tu africa mashariki. Kwa utafiti wangu nimegundua wengi wanaoamini ivyo ni hawajitambui pia wengi wao hawaijui iyo lugha.
 
Nani anaechanganya IQ na english?
Korea, japan na china english hawajui hata kuongea ni shida ila wastani wa iq zao ni zaidi 100
 
Katika aina za IQ, kuna type inaitwa Language Intelligent.

So inategemea umeLook from which angle.
 
Ki ukweli mimi Kingereza ni hakuna kabisa sio cha kuongea au cha kuandika Ila uwezo wangu wa kufikiri hasa kwenye Hisabati uko tofauti kwa kila darasa ambalo nimewahi kuwa nalo au shule au umri nlo nao ..
Nafadhahikaga sana sehemu nafika napewa kisogo kisa sikifaham vizuri kingereza.
Kusoma nakuelewa ni mwepesi sana tatizo kujibu na hata kukumbuka herufi za neno kwa ufasaha(kingereza).

Hii imenifanya kucharaza mwandiko ili mtu asione herufi za neno nilivyoandika akagundua hayo makosa maana binadam tunasoma neno na si herufi moja moja. Na ndo njia nlotumia hadi nikahitimu chuo.
 
Huwa na shangaa sana napokutana na watu wakimsifia mtu anayeongea kiingereza na kumheshimu kisha kumdharau asiyejua kuongea hiyo lugha.

Wanashindwa kuelewa kwamba kiingereza ni lugha tu kama lugha nyingine japo ni international language kama kiswahili tu africa mashariki. Kwa utafiti wangu nimegundua wengi wanaoamini ivyo ni hawajitambui pia wengi wao hawaijui iyo lugha.
Unakwama wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom