Kwanini watanzania hasa waliosomea Lugha wanashindwa kuchangamkia fursa za kazi za ualimu wa Kiswahili, Kiingereza na utafsiri wa lugha nchini Japan

Parabora

JF-Expert Member
Jul 6, 2019
1,504
2,179
wakuu bado lock-down inaendelea japo kuna mwanga unaanza kuonekana baada ya hotuba ya leo ya waziri wa uchumi wa hapa switzerland bwana Guy Parmelin kuonesha matumaini ya kulegezwa kwa masharti katika phase ijayo ya kupambana na huu ugonjwa.

Turudi kwenye tafakuri ya leo kama heading inavyoeleza, walimu wa fani ya lugha wanaomaliza huko nchini kwenye vyuo vya nyumbani wanashindwa nini kuchangamkia fursa za kimataifa na ikiwa ukweli ni kwamba wana uwanja mpana wa fursa huku?

Nimekaa Japan nchi ina uhitaji mkubwa wa walimu wa kiingereza, kiswahili na watafsiri wa lugha(Interpreter/Translator) na si Japan tu hata mataifa ya karibu na japan kama china na korea kusini nako wanahitajika sana, nini hasa kinawakwamisha vijana wenzangu wahitimu wa hizi fani kuzichangamkia hizi fursa za kimataifa? Ukiwa nchini Japan unakutana na wakenya wengi wanafundisha kiswahili lakini huwezi kukutana na mbongo anafundisha kiswahili na wakati wahitimu wapo wengi wa hizi fani na pia hii ni lugha yetu toka kuzaliwa.

kwa Japan hawa watu ni kati ya watu wanaolipwa vizuri nimeshuhudia watu wa mataifa ya uganda hata kiswahili hawajui vizuri wanafanya kazi za part time za kufundisha kiswahili na wanalipwa 300,000Yen kwa mwezi, na rafiki yangu mkenya yeye alikuwa analipwa 4,500,000m Yen anafundisha kiswahili na ni mkalimali pia sisi ndio lugha yetu lakini tukamwa hata kuifundisha kimataifa pamoja na kuwa tunahitajika, tatizo ni nini?

Kwa wahitimu wa fani hii, fani yenu haina changamoto kimataifa kabisa kama walivyo wa fani za Engineering, IT &Telecomunication Engineering ama manufacture/Industrial engineering ambazo nchi zilizoendelea haziwezi kutilia maanani elimu hizi zilizotoka baadhi ya nchi za kiafrica kufanya kazi kwenye taasisi zao japo zinahitajika kwa wingi.

Hivi mnashindwa hata kusoma Certification za CELTA,TELF na TESOL/TESL au ESL kwa miezi kadhaa ili muweze kuwa wa kimataifa kidogo, British Council hawa wapo kila nchi matawi yao nadhani hata tanzania wapo, mnashindwa kusoma hizi programme kwa miezi michache then mkachangamkia fursa kimataifa? AMKENI VIJANA MSITEGEMEE SOKO LA AJIRA LA NDANI TU MNAHITAJIKA SANA HUKU DUNIANI

N:B
CELTA - Certifacte in English Language Teaching to Adult
TEFL - Teach English as a Foregn Language Certificate
TESOL - Teach English to Speaker of Other Language Certificate
TESL - Teaching English as a Second Language Certificate
ESL - English as a second language Certificate

Kati ya hizo certificate CELTA ni nzuri kwa nchi kama Japan kulingana na mahitaji yake

Parabora
Geneva - Switzerland

chukua hatua stahiki, Corona ipo na ni hatari
 
Hili unalosema ni kweli lakini bado narudia elimu yetu inampumbaza mtoto zaidi kuliko kumtengeneza ajiamini katika kupambana, ni kweli kiswahili kwa sasa kina demand kubwa huko nje lakini wanaongoza kuchangamkia fursa hiyo ni wakenya na waganda ingawaje hawakijui vizuri kama sisi.

watoto wetu wakimaliza wanachosubiri ni kuajiriwa na serikali na wakikosa hawana maono mengine ya kuwawezesha kujikwamua.

kuna umuhimu wa elimu hii kupitiwa upya
 
Hivi vijamaa vyenye macho madogo ni vichumia tumbo havikupi dili kabisa badala yake vinakuja kukusanya coins zetu milioni 200
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom