Wajamani tusaidiane JK ni mchumi kweli au...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wajamani tusaidiane JK ni mchumi kweli au...?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Feb 16, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,564
  Trophy Points: 280
  Jana JK amedai ya kuwa kuna malengo mawili tu ya MDG au Millenium goals ambazo hatuwezi kuzifikia na ni zile zinazogusa "life expectancy" na hivyo kuamaanisha ya kuwa nyingine zote tutazikamilisha...................huu ni uongo wa kutukuka........................

  Katika kupima ubora wa maisha ya mwanadamu yaani "standard of living" kipimo cha "life expectancy" ni cha muhimu sana na vipimo hivyo viwili huwezi kuvitenganisha hata chembe........................

  Kwa kauli ya JK inaashiria ya kuwa MDGs nyinginezo zote tutazikamilisha na hivyo kama ni kweli itakuwa hivyo basi "living standard" itapanda na kama ikipanda kwa nini "life expectancy" ishuke au kubali pale pale ilipo????????????????

  Vifo vya watoto chini ya umri wa miaka 5 na akina mama waja wazito ni dhahiri vitachangia katika kupunguza "life expectancy" na moja kwa moja waathirika hao "living standard" yao ni lazima iwe mbaya vinginevyo wangelikuwa na mazingira ya kukwepa hizo suluba.........................

  Suluba hizo wameshindwa kuzikwepa kwa sababu ni ukweli usiopingika hatuna uwezo wa kufikia hizo MDgs hata mojawapo...................

  Sasa pale ambapo Jk anashindwa kuona uhusiano kati ya "life expectancy" na "living standard" hi huyu ni mchumi wa wapi??????????????????

  Jana hiyo Waziri Ngeleja amesema umeme wa uhakika ni hadi 2033.............sasa hizo MDGs nyinginezo ukiondoa nambari 4 na 5 ambazo JK anatamba zitafikiwa.......kweli zitafikiwa bila ya umeme wa uhakika????????????????

  Is this government speaking in tongues or what........................
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,564
  Trophy Points: 280
  'Malengo 2 ya MDGs hayafikiki'

  Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Kibaha; Tarehe: 15th February 2011 @ 23:56 Imesomwa na watu: 97; Jumla ya maoni: 0
  SERIKALI ya Tanzania bado ina changamoto ya kufikia malengo mawili ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) yanayohusu sekta ya afya.

  Hayo yamesemwa na Rais Jakaya Kikwete akiyataja malengo hayo kuwa ni la nne linalosisitiza kupunguza vifo vya watoto wa umri wa chini ya miaka mitano na la tano linalosisitiza kupunguza vifo vya wazazi ifikapo mwaka 2015.

  Rais Kikwete alikuwa akifungua jana jengo la Afya ya Uzazi na Huduma za Watoto katika Hospitali Maalumu ya Tumbi mjini Kibaha, Pwani lililojengwa kwa msaada wa Serikali ya Korea kwa ushirikiano na klabu ya kimataifa ya Rotary kwa gharama ya Sh bilioni 1.1.

  Alisema kuna mafanikio kiasi katika utekelezaji wa malengo hayo kwa mwaka 2005/10 ambapo vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano vilipungua kutoka 157 kwa hadi 121 kwa watoto 1,000 wakati vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka 95 hadi 76 kwa 1,000.

  Hata hivyo, alisema takwimu za vifo vya uzazi hazijapungua kiasi cha kuridhisha ambapo inaonesha kupungua kwa wastani wa 578 hadi 454 kwa 100,000 mwaka jana, hali ambayo bado inatia shaka.

  "Nina shaka kama 2015 tutaweza kufikia lengo hili la tano kwa kuwa idadi ya akinamama wanaokufa kwa uzazi bado ni kubwa, angalau kwenye lengo la nne kuna unafuu," alisema Rais Kikwete.

  Alisema katika kukabiliana na changamoto, Serikali imeweka kipaumbele katika kupambana na vifo hivyo kupitia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi, ambao katika utekelezaji wake, zinajengwa zahanati kwa kila kijiji na vituo vya afya na kupandisha hadhi hospitali za mikoa, ili kuboresha huduma za ngazi ya pili na ya tatu.

  "Mwananchi asitembee zaidi ya kilometa tano kufuata huduma za afya na hospitali za rufani ziweze kutoka huduma kwa kiwango cha juu na kwa wakati unaotakiwa," alisema na kuongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wataalamu na vifaa katika kila ngazi vinakuwapo vya kutosha, ili wananchi wapate huduma bora zaidi.

  Rais Kikwete takwimu zinaonesha kwamba kwa Tanzania, uwiano wa daktari na wagonjwa ni 1:30,000 wakati Korea ni 1:500.

  Alitaka wataalamu wa afya kutunza vifaa na majengo hayo ili viweze kudumu na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa ya kuokoa maisha ya watu.

  "Itakuwa aibu baada ya muda mfupi kusikia vifaa mmehamishia katika hospitali zenu au za rafiki zenu au vimeharibika," alisema Rais Kikwete.

  Mwenyekiti wa taasisi ya Community Chest ya Korea, Dk Lee Dong-Kurn na Balozi wa Korea nchini, Kim Young, walisema kupunguza vifo vya watoto ni kampeni ya kimataifa na Umoja wa Mataifa umeelekeza jitihada zifanyike.

  Kiongozi wa Rotary, Andy Chande alisema msaada huo ulipangwa kupelekwa Dar es Salaam, lakini Rais Kikwete alitaka jengo hilo lijengwe nje ya mji.

  Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Amina Said, alisema wafadhili wamekubali kutoa msaada wa dola 120,000 za Marekani kwa ajili ya ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika kituo cha afya mkoani Pwani ili kupunguza msongamano Tumbi.


   
 3. amanindoyella

  amanindoyella Senior Member

  #3
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mimi nina mgojwa Tumbi, manesi waliacha kuwahudumia wagonjwa ili wapate fursa ya kumsikilizi kikwete awakabidhi jengo jipya. Karibu kila dawa sharti ununue hati mabomba ya sindano!
   
 4. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,569
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Jamani huyu bwana ni mchumi, ila tuu mambo mengi yanamchanganya!
   
 5. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kama kikwete ni mchumi basi neno UCHUMI silielewi vizuri. Halafu ningependa kuwapa hint tu wachangiaji wa thread nii kwamba kikwete alipata gentleman degree ya pale UDSM. Ndiyo maana alienda kwenye kichaka cha siasa kwenye chama.
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  siyo mchumi.

  ni luteni kanali
   
 7. m

  mzambia JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mi namfahamu sana kikwete ni mchumi mzuri sana ila alikuwa akidesa sana hajawahi kufanya pepa ye ka yeye kwa waliosoma mlimani wanajua neno loop. Alikuwa mtaalam wa kutengeneza loop kwa hiyo hakuna anachokijua zaidi ya kudesa sidhani kama anajua hata logarithm maana ni mtaalam sana wa kudesa na ndio maana maamuzi magumu anashindwa kuyachukua kwa sababu hana desa.
   
 8. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Aiseeeeeee, kuuuumbeeee, basi ndiyo maana hawezi kazi. Kazoea madesa tu. Hata mke wake mama salma nasikiai ni kilaza kwelikweli! Sasa sijui watoto wa shuke (ya msingi) walikuwa wanaishije na mwailimu kilaza!!??
   
 9. g

  geophysics JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Haya twende ndugu zangu... Hayo ndio maisha bora kwa kila mtanzania... Wana CCM waliita Hari mpya, nguvu mpya na kasi mpya.... Poleni walalahoi wenzangu
   
 10. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
   
 11. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Fisadi kikwete hiyo shahada ya Uchumi naona ameipatia kwenye uchakachuaji pia, mchumi gani asiyejua hata umaskini wa nchi yetu. hana lolote huyu fisadi bora apate kiharusi nchi iwe salama:coffee:
   
 12. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  NINI SABABU YA TANZANIA KUWA MASKINI HADI SASA?
  HATA MIMI SIFAHAMU SABABU!!!!!
  huyo ndiyo mchumi unayemsema .................. ukimuuliza hilo swali kijana anayesoma form six sababu za umaskini atakutajia pasipo hata kutafakari. leo unayemuita mchumi hajui ..............
  KIfupi wasomi wengi waliomaliza mlimani si uchumi tu bali hata shahada zingine ni vilaza. Wamesoma kwa kukaririshwa si kuelewa mambo. na sababu kuu ya kukaririshwa ni walimu wao/professors kuwa na wivu wa kuona wanafunzi wao wanafaulu!!. Mwanafunzi aliyemaliza mzumbe au DIT ni mzuri kuliko yule wa Mlimani!!!
   
 13. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  He's not and neva was!
   
 14. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 802
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Mchumi wa kuchumia mafioso!!
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Ni mchumi wa kusomea mkuu, but kunatofauti kubwa kusomea kitu na kukitekeleza hasa kama ulifeli. Playboy kama huyo sups zilikuwa kubao tu!
   
 16. s

  seniorita JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Millennium goals in a reverse gear....that is what it is...
   
 17. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Greater Thinkers

  Jamani nimeona threads zenu humu nikagundua wengi wenu humu hamfahamu hata hizo MDGs.
  FYI below are MDGs
  GOAL 1. Eradicate extreme poverty and hunger
  GOAL 2. Achieve Universal Primary education
  GOAL 3. Promote Gender Equality and Empower women
  GOAL 4. Reduce Child Mortality
  GOAL 5. Improve Maternal Health
  GOAL 6. Combat HIV/AIDS, Malaria and Other Diseases
  GOAL 7. Ensure Environmental sustainability
  GOAL 8. Develop a Global Partnership for Development

  My Take ni kwamba sione hata goal moja tukii achieve, I stand to be corrected
   
 18. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  kwani JK ni mchumi ?au ni mchumi wa siasa?
  Huyu bwana amesomea mambo ya siasa za uchumi and not economic at all.
  Hivi ni vitu tofauti sana.
  Angekuwa ni mchumi anagekuwa aniongoza nchi hivyo?
  hata kipofu akipewa anaweza kuiongoza kwa sababu yeye ameakaa na kuna watu wanaoongoza nchi...agghhhhhhhhh mchumi?? nani???:clap2:
   
 19. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  yapi?
   
 20. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  ahsante kwa kuliellewa hilo
  hakuna mchumi hapo labda kama ni mchumaji
   
Loading...