Waislamu wazindua program 2010

Sifa za kiongozi wanaemtaka hawa maashura ni mtu mmoja tu anaweza kuwa nazo. Nae so mwingine bali ni Osama bin Laden....

Mgombea yeyote atakaekua Endorsed na hii shura aandike maumivu, hatashinda ng´ooo
 
Imekua vyema. Basi tusisikie kelele za muongozo wa Wakatoliki. Wao watekeleze programu yao na wawaache Wakatoliki watekeleze mipango yao.
Salute Mkuu. Na kwa msingi huu hatupaswi kusikia tena malumbano... tuachwe tuendelee na mambo mengine
 
Huo wimbo wa "waislamu wanaonewa" sijui utaisha lini. Hayo ni mambo ya kufikirika tu wala hakuna ukweli wowote. Ushauri wangu kwa waislamu ni kwamba waelekeze nguvu katika kusomesha watoto wao kama wanavyoelekeza nguvu kwenye madrasa. Wenzao wakristo wana-invest kwenye masuala yote; dini na elimu. Hivyo, siyo jambo la kushangaza kuona kuwa asilimia kubwa ya waislamu hawajasoma ikilinganishwa na wakristo. Hii siyo siri ni ukweli tu. Hata hao wanaojiita shura ya maimamu ukiwachambua kwa kina utagundua elimu yao imeishia kwenye masuala ya dini tu. Masuala ya kidunia ni patupu! Ukitaka uamini hoja yangu soma hayo maandishi yao ya kurasa 76 hutaona substance yoyote. Jambo la kushukuru ni kwamba hata waislamu wenzao ambao wameelimika kidunia wanawapuuza hao maimamu.
 
I can see clearly a fragmented Tanzania,how can a secural country argue based on religious grounds???nilifikiri tungewajidili wagombea kwa vipaumbele vyao? historia yao,uadilifu wao,uwezo wao katika kujadili na kutatua mambo mbalimbali,maono(vision ) zao, na si ataifanyia nini dini fulani,mtu fulani,kikundi fulani,jamii fulani,hell no!!!!!!!!!!!!
 
mkuu usipate shida kusoma kati ya mistari (btn the lines) aya hii hapa inaeleza lengo lao kwa uwazi.

Lengo ni
(1) kuwa na viongozi Waislam
(2) kulipa kisasi ktk yale wanayohisi walionewa
(3) kuifanya nchi ya kidini (kutambua na kutekeleza sheria za Kiislam)

Ninawasiwasi jamaa wamebanwa mno kule Afghan na Paksistan sasa watatafuta new territory kama ilivyo Somalia.

Nafikiri hapa ndipo ulipokosea na kutia chumvi kwenye chai
 
Wakatoliki itawaudhi hiyo program. lakini nchi ni ya wote . You can fool some people some time But ou can't all the people all the time.

In your dreams! Naona mzigo wa dhambi ushautua sasa uko mbioni kuanza upya! Yetu macho.

Amandla.......
 
Mimi nafikiri ujafatilia kadhia hii.
Awali ya yote Wakatoliki walitoa waraka wao kuhusu uchaguzi. Waraka huo ulileta utata mkubwa sana kwa viongozi wa Serikali na hata wanasiasa. Tunajua wazi kila aliyejaribu kuupinga waraka ule aliandamwa kwa kejeli na matusi ,akubwa. Mfano, Mh Kingunge, na Askofu Kakobe.

Waislam wao baada ya kuona waraka wao wakatoa MWONGOZO kuelekea uchaguzi mkuu. Mwangozo huo ulilaaniwa vikali sana na wakatoliki na wengine.

Sasa waislam wametoa program ya kutekeleza mwongozo wao. Kwa bahati kubwa sana nipo Dar na nmeupata jioni hii hapa kariakoo msikiti wa Mtoro. Nitampa mke wangu aupitie na kuuchambua zaidi.

wazo langu kama wakatoliki mna nia nzuri na TZ basi waacheni waislam na program yao. Au mna wasiwasi kuwa ile 73.4% ya wabunge wote katika bunge la muungano a,bao ni wenu sasa inawezekana ikapungua.

Kutesa kwa zamu.

Mkuu, mpaka uchambuliwe na mkeo!
Mimi naona huu ni mradi tu, mauzo ya waraka hayakukidhi njaa za baadhi za watu kwa hiyo wameona watoe sequel. Wajinga ndiyo waliwao.

Amandla......
 
Fundi Mchundo,

Unafikiri hawa Tumaini na Barubaru hata watanunua?

Kwanza hata wa kwanza hawajasoma. Wao siku nzima wako JF wanahaha na kuhema utafikiri Jogoo limeona paja la Mwanamke. Wanabadili thread moja hadi nyingine kutafuta habari za Dr. Slaa, Uislaam, Nyerere na CHADEMA.

Ukiwachunguza saana utagundua kuwa ni WASOMI wazuri tu na wameletwa hapa kwa kazi fulani ambayo kwa kweli wanaifanya vizuri sana.

Kama ulisoma maelezo ya GT juu ya USALAMA WA TAIFA utaanza kugundua kuwa aliyoyasema yana ukweli. Kama siyo UWT basi nchi ingelikuwa imelipuka zamani sana ila wao wanajua kuuma na kupuliza. Sasa hivi wanatukeep busy na UDINI na wakati huo Mafisadi wanazidi kupeta.

Maelezo ya GT yanaonyesha kuwa hata yeye mwenye GT anaweza kuwa UWT. Mara nyingi anakuwa na hawa akina Tumaini na Barubaru.

Uongozi wa JF inabidi uwamulike hawa jamaa. Ikibidi basi nilishauri JF imeguliwe na kwenye PUMBA basi na dini iwekwe. Jitu likianza kubadilisha mada basi linaliwa Ban. Akianzisha thread za kipuuzi basi inapelekwa kwenye thread ya Majungu/Pumba/Dini nk.
 
Sifa za kiongozi wanaemtaka hawa maashura ni mtu mmoja tu anaweza kuwa nazo. Nae so mwingine bali ni Osama bin Laden....

Mgombea yeyote atakaekua Endorsed na hii shura aandike maumivu, hatashinda ngo.
Kiongozi wanayemtaka hawa Maaskofu ni mtu mmoja tu anaweza kuwa nazo. Naye si Mwingine ila ni "John Garang" ..........
Mgombea yeyote atakekuwa endorsed na Maaskofu na waraka wao aandike maumivu, hatashinda ng'o
 
maneno yako sawia kabisa yaa Alhaj.

Pilipili yaliwa shamba wao yawawashiani.

Program ya waislam basi waacheni na program yao.
Unasahau kuwa hili ni shamba letu sote. Ungekuwa ni mwongozo wa msikitini au jumuiya ya Bakwata ingekuwa pilipili ya shamba. Lakini kuhusu uongozi wa nchi inatuhusu sote.
 
maneno yako sawia kabisa yaa Alhaj.

Pilipili yaliwa shamba wao yawawashiani.

Program ya waislam basi waacheni na program yao.

Waraka wa wakatoliki ulikuwa kwa Taifa na wa kwenu kwa waislamu?btw hiyo signature yako vipi?Ni wazi ukiwa mroho lazima utakuwa mchoyo maana you want it all sasa unaposema ukiwa mchoyo usiwe mroho haueleweki,Tumain ansema mnajadili mambo "Kiwaraka waraka" sasa hapa naona mmekuja na kiislam islam,ama?Hiyo pili pili kwenye shamba lenu bakini nayo,shida iko pale kwenye kujitambulisha kwa dini kwanza kabla ya utaifa,tunataka solutions zenye kutatua matatizo ya kitaifa na si program ziso na kichwa wala miguu.
 
Wakatoliki itawaudhi hiyo program. lakini nchi ni ya wote . You can fool some people some time But ou can't all the people all the time.

Ya alhajj-safari ilikuwaje?

Natumai na sisi ulituombea.

Pia natumai uliwaombea Wakatoliki na Waislamu waje na miongozi yenye manufaa kwa sote.
 
KAMATI ya Siasa ya Shura ya Maimamu jana ilizindua programu ya Elimu ya Uraia yenye lengo la kutekeleza kwa vitendo waraka wake kuhusu uchaguzi mkuu wa mwakani.

Programu hiyo inataja sifa za msingi za chama na mgombea anayepaswa kuchaguliwa, masuala ambayo yalisababisha utata mkubwa baada ya nyaraka hizo za Shura ya Maimamu na Kanisa Katoliki kutolewa.

Mpango huo umo kwenye kitabu cha kurasa 76 na unataka Waislaam kuutekeleza kwa vitendo mwongozo uliozinduliwa na kamati hiyo Agosti 26 mwaka huu.

Programu hiyo ilizinduliwa jana kwenye Msikiti wa Mtoro jijini jijini Dar es Salaam na balozi wa zamani wa Tanzania katika nchi za Ufaransa na Italia, Abbass Sykes. Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, Sykes alisema: "Nchi hii ni ya Watanzania wote, hakuna chama wala mtu mwenye hati miliki ya kutawala nchi hii."

Alisema kila chama na mtu bila ya kujali rangi, dini, kabila au mahali alipotoka, ana haki ya kuomba uongozi ili mradi awe amegombea nafasi ya uongozi kwa kufuata taratibu na sheria zilizopo.

Sifa za mgombea zinatajwa katika mada nambari tano ya kitabu hicho cha 'Elimu ya Uraia' kikitaja bayana sifa za mgombea anayetakiwa kupigiwa kura na Waislamu. "Awe kiongozi mwadilifu, anayejua matatizo makuu ya nchi na wananchi na mjuzi wa kuyatatua.

Matatizo makuu ya nchi ni udini, ubaguzi dhidi ya Waislaam au baadhi ya watu, rushwa, uchafuzi wa mkataba wa Muungano na ukosefu wa maadili kwa viongozi," inasema sehemu hiyo katika ukurasa wa 65.

"Awe kiongozi mwenye utashi wa kuwasaidia wananchi wote bila ya kujali tofauti zao, ajali zaidi maslahi ya umma kuliko ya chama chake, awe tayari kusaidia urejeshaji wa haki za wananchi zilizotaifishwa na serikali ikiwa ni pamoja na shule, ardhi na majengo."

Kitabu hicho kinaeleza kuwa ili mgombea apigiwe kura, anapaswa awe anafahamu haki na dhuruma walizofanyiwa Waislaam kwa kutotendewa haki sawa na dini nyingine na awe tayari kufuta makubaliano baina ya serikali na kanisa.

"Kiongozi huyo lazima awe tayari kutomwaga damu ya Waislaam kama ilivyotokea mara kadhaa katika misikiti, maandamano ya kudai haki au katika mahubiri ya kidini."

Kuhusu chama kinachostahili kuingia madarakani, kitabu hicho kinafafanua kuwa ni kile ambacho serikali yake haitawazuia Waislaam kufuata na kutangaza dini yao kwa uhuru na ambayo haitabadilisha sheria za Waislaam zinazohusu mambo ya mirathi, ndoa na talaka.

Kamati hiyo ya siasa ya Shura ya Maimamu, ilikumbushia migogoro mbalimbali baina ya serikali na Waislaam na kwamba chama kinachofaa ni lazima kiwe tayari kuunda tume huru kuchunguza mauaji ya Waislaam yaliyotokea miaka iliyopita.

"Kiwe chama ambacho serikali yake, itakubali kufanyika kwa uchunguzi wa mauaji ya waislaam katika maandamano ya kutetea Qur-an 1988, mauaji ya msikitini Morogoro 1994, mauaji ya kinyama msikitini Mwembechai 1998, mauaji ya imamu wa msikiti wa Mwembetanga 2001 na mauaji katika maandamano ya Waislaam ya kupinga kufungwa kwa mwenzao aliyesema Yesu si Mungu mwaka 2001," inafafanua sehemu ya kitabu hicho.

"Kiwe chama ambacho serikali yake haitakuwa tayari kupokea maagizo, sheria na misamiati mipya dhidi ya Waislaam kama vile magaidi au siasa kali na kuwasikiliza masheikh na maimamu pamoja na viongozi wengine wa taasisi za kiislaam."

Awali katibu wa kamati ya siasa ya Shura ya Maimamu, Sheikh Ponda Issa Ponda alisema: "Muongozo (wa awali) umefanikiwa sana hasa mikoani, katika mikoa ya kanda ya kusini zaidi ya asilimia 90 ya viongozi walishinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ni Waislaam wanaojielewa."

"Asilimia 75 ya wilaya zote za Tanzania zimefanya warsha na makongamano kuuchambua mwongozo, hotuba za Ijumaa zenye mwelekeo mmoja zimeanza jijini Dar es Salaam, Baraza Kuu la Wanawake wa Kiislaam limetanga kura ya maslahi kuwa ajenda yao kuu 2010 na Taasisi 15 zimesaini makubaliano ya pamoja kuelekea uchaguzi mkuu."

Kwa mujibu wa sheikh Ponda, program mpya ya elimu ya uraia itatekelezwa katika mifumo ya machapisho, warsha, semina, makongamano, mikutano ya hadhara na hotuba kali za Ijumaa zenye mwelekeo mmoja katika miskiti yote nchini.

Source: Mwananchi

Naona mnataka rais muislam kwa ajili ya waislam,hakuna pahala napoweza kusema mnataka rais atakayewashughulikia mafisadi,very sad,uislam na waislam tu basi,everything else doesnt matter....Safari ni ndefu.
 
Wamesema lazima awe mwadilifu, sasa lazima uone neno fisadi ndio uridhike kwamba mwadilifu lazima apige vita ufisadi?

Quran inasema 'Inna llahh la yuhibu Mufsiddin' yaani 'Allah hapendi mafisadi' , hapo je umeridhika? Hata kitabu chao kinatangaza vita dhidi ya ufisadi. Utawaunga mkono sasa baada ya kuona haya ama utatafuta jingine?
 
Wanasema tatizo kubwa ni udini na wana imply kuwa viongozi wakristo ndiyo mafisadi....Soma kwa makini...Ningependelea kuona mwongozo wa kitaifa zaidi.
 
Fundi Mchundo,

Unafikiri hawa Tumaini na Barubaru hata watanunua?

Kwanza hata wa kwanza hawajasoma. Wao siku nzima wako JF wanahaha na kuhema utafikiri Jogoo limeona paja la Mwanamke. Wanabadili thread moja hadi nyingine kutafuta habari za Dr. Slaa, Uislaam, Nyerere na CHADEMA.

Ukiwachunguza saana utagundua kuwa ni WASOMI wazuri tu na wameletwa hapa kwa kazi fulani ambayo kwa kweli wanaifanya vizuri sana.

Kama ulisoma maelezo ya GT juu ya USALAMA WA TAIFA utaanza kugundua kuwa aliyoyasema yana ukweli. Kama siyo UWT basi nchi ingelikuwa imelipuka zamani sana ila wao wanajua kuuma na kupuliza. Sasa hivi wanatukeep busy na UDINI na wakati huo Mafisadi wanazidi kupeta.

Maelezo ya GT yanaonyesha kuwa hata yeye mwenye GT anaweza kuwa UWT. Mara nyingi anakuwa na hawa akina Tumaini na Barubaru.

Uongozi wa JF inabidi uwamulike hawa jamaa. Ikibidi basi nilishauri JF imeguliwe na kwenye PUMBA basi na dini iwekwe. Jitu likianza kubadilisha mada basi linaliwa Ban. Akianzisha thread za kipuuzi basi inapelekwa kwenye thread ya Majungu/Pumba/Dini nk.

Ahali yangu Fundi mchundo.

Hakika mimi nimeununua jana majira ya saa sabaa mchana baada ya swala la Adhuhur pale msikiti wa Mtoro kariakoo kwenye duka la radio Quran.

Nimefurahi sana mwangozo huu umetoka wakati nipo Tanzania. Nitakuwepo mpaka ijumaa na namba ninayotumia ni 0777 420000 ( ya dereva wangu)

Nafikiri kinachokusumbua wewe ni kutaka watu uwaendeshe kama makondoo. Yaani wewe unataka kila mtu aisifie Chadema, Ukatoliki na mengine.

hakika nipo na natumai mwenzangu Tumaini naye yupo huru sana kuchangia kwa mujibu wa mawazo yake na sio kushinikizwa ka kashfa na matusi. Tunaomba utuletee hoja na si kingine.
 
Mkuu, mpaka uchambuliwe na mkeo!
Mimi naona huu ni mradi tu, mauzo ya waraka hayakukidhi njaa za baadhi za watu kwa hiyo wameona watoe sequel. Wajinga ndiyo waliwao.

Amandla......

Mke wangu ana taaluma mbili ya sheria na uandishi. sasa uchambuzi wake utakuwa na msingi mkubwa sana katika kuweka mambo sawa.

Unakumbuka hapahapa katika JF alivyounyambua waraka wa wakatoliki.
Sasa na huu ataudadavua tu usitie shaka
 
Kiongozi wanayemtaka hawa Maaskofu ni mtu mmoja tu anaweza kuwa nazo. Naye si Mwingine ila ni "John Garang" ..........
Mgombea yeyote atakekuwa endorsed na Maaskofu na waraka wao aandike maumivu, hatashinda ng'o
Keli kabisa.
 
Fundi Mchundo,

Unafikiri hawa Tumaini na Barubaru hata watanunua?

Kwanza hata wa kwanza hawajasoma. Wao siku nzima wako JF wanahaha na kuhema utafikiri Jogoo limeona paja la Mwanamke. Wanabadili thread moja hadi nyingine kutafuta habari za Dr. Slaa, Uislaam, Nyerere na CHADEMA.

Ukiwachunguza saana utagundua kuwa ni WASOMI wazuri tu na wameletwa hapa kwa kazi fulani ambayo kwa kweli wanaifanya vizuri sana.

Kama ulisoma maelezo ya GT juu ya USALAMA WA TAIFA utaanza kugundua kuwa aliyoyasema yana ukweli. Kama siyo UWT basi nchi ingelikuwa imelipuka zamani sana ila wao wanajua kuuma na kupuliza. Sasa hivi wanatukeep busy na UDINI na wakati huo Mafisadi wanazidi kupeta.

Maelezo ya GT yanaonyesha kuwa hata yeye mwenye GT anaweza kuwa UWT. Mara nyingi anakuwa na hawa akina Tumaini na Barubaru.

Uongozi wa JF inabidi uwamulike hawa jamaa. Ikibidi basi nilishauri JF imeguliwe na kwenye PUMBA basi na dini iwekwe. Jitu likianza kubadilisha mada basi linaliwa Ban. Akianzisha thread za kipuuzi basi inapelekwa kwenye thread ya Majungu/Pumba/Dini nk.

Hongereni sana Barubaru na Tumain.

Bila shaka hawa ni mayahudi hawa.
 
Mimi nafikiri ujafatilia kadhia hii.
Awali ya yote Wakatoliki walitoa waraka wao kuhusu uchaguzi. Waraka huo ulileta utata mkubwa sana kwa viongozi wa Serikali na hata wanasiasa. Tunajua wazi kila aliyejaribu kuupinga waraka ule aliandamwa kwa kejeli na matusi ,akubwa. Mfano, Mh Kingunge, na Askofu Kakobe.

Waislam wao baada ya kuona waraka wao wakatoa MWONGOZO kuelekea uchaguzi mkuu. Mwangozo huo ulilaaniwa vikali sana na wakatoliki na wengine.

Sasa waislam wametoa program ya kutekeleza mwongozo wao. Kwa bahati kubwa sana nipo Dar na nmeupata jioni hii hapa kariakoo msikiti wa Mtoro. Nitampa mke wangu aupitie na kuuchambua zaidi.

wazo langu kama wakatoliki mna nia nzuri na TZ basi waacheni waislam na program yao. Au mna wasiwasi kuwa ile 73.4% ya wabunge wote katika bunge la muungano a,bao ni wenu sasa inawezekana ikapungua.

Kutesa kwa zamu.

Kwa hiyo, unakubaliana na mimi kwamba Waislamu kuwapinga Wakatoliki ulikuwa unafiki tu hawakuwa na hoja ya maana?
 
Back
Top Bottom