Waislamu wazindua program 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waislamu wazindua program 2010

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by HM Hafif, Dec 7, 2009.

 1. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  KAMATI ya Siasa ya Shura ya Maimamu jana ilizindua programu ya Elimu ya Uraia yenye lengo la kutekeleza kwa vitendo waraka wake kuhusu uchaguzi mkuu wa mwakani.

  Programu hiyo inataja sifa za msingi za chama na mgombea anayepaswa kuchaguliwa, masuala ambayo yalisababisha utata mkubwa baada ya nyaraka hizo za Shura ya Maimamu na Kanisa Katoliki kutolewa.

  Mpango huo umo kwenye kitabu cha kurasa 76 na unataka Waislaam kuutekeleza kwa vitendo mwongozo uliozinduliwa na kamati hiyo Agosti 26 mwaka huu.

  Programu hiyo ilizinduliwa jana kwenye Msikiti wa Mtoro jijini jijini Dar es Salaam na balozi wa zamani wa Tanzania katika nchi za Ufaransa na Italia, Abbass Sykes. Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, Sykes alisema: "Nchi hii ni ya Watanzania wote, hakuna chama wala mtu mwenye hati miliki ya kutawala nchi hii."

  Alisema kila chama na mtu bila ya kujali rangi, dini, kabila au mahali alipotoka, ana haki ya kuomba uongozi ili mradi awe amegombea nafasi ya uongozi kwa kufuata taratibu na sheria zilizopo.

  Sifa za mgombea zinatajwa katika mada nambari tano ya kitabu hicho cha 'Elimu ya Uraia' kikitaja bayana sifa za mgombea anayetakiwa kupigiwa kura na Waislamu. "Awe kiongozi mwadilifu, anayejua matatizo makuu ya nchi na wananchi na mjuzi wa kuyatatua.

  Matatizo makuu ya nchi ni udini, ubaguzi dhidi ya Waislaam au baadhi ya watu, rushwa, uchafuzi wa mkataba wa Muungano na ukosefu wa maadili kwa viongozi," inasema sehemu hiyo katika ukurasa wa 65.

  "Awe kiongozi mwenye utashi wa kuwasaidia wananchi wote bila ya kujali tofauti zao, ajali zaidi maslahi ya umma kuliko ya chama chake, awe tayari kusaidia urejeshaji wa haki za wananchi zilizotaifishwa na serikali ikiwa ni pamoja na shule, ardhi na majengo."

  Kitabu hicho kinaeleza kuwa ili mgombea apigiwe kura, anapaswa awe anafahamu haki na dhuruma walizofanyiwa Waislaam kwa kutotendewa haki sawa na dini nyingine na awe tayari kufuta makubaliano baina ya serikali na kanisa.

  "Kiongozi huyo lazima awe tayari kutomwaga damu ya Waislaam kama ilivyotokea mara kadhaa katika misikiti, maandamano ya kudai haki au katika mahubiri ya kidini."

  Kuhusu chama kinachostahili kuingia madarakani, kitabu hicho kinafafanua kuwa ni kile ambacho serikali yake haitawazuia Waislaam kufuata na kutangaza dini yao kwa uhuru na ambayo haitabadilisha sheria za Waislaam zinazohusu mambo ya mirathi, ndoa na talaka.

  Kamati hiyo ya siasa ya Shura ya Maimamu, ilikumbushia migogoro mbalimbali baina ya serikali na Waislaam na kwamba chama kinachofaa ni lazima kiwe tayari kuunda tume huru kuchunguza mauaji ya Waislaam yaliyotokea miaka iliyopita.

  "Kiwe chama ambacho serikali yake, itakubali kufanyika kwa uchunguzi wa mauaji ya waislaam katika maandamano ya kutetea Qur-an 1988, mauaji ya msikitini Morogoro 1994, mauaji ya kinyama msikitini Mwembechai 1998, mauaji ya imamu wa msikiti wa Mwembetanga 2001 na mauaji katika maandamano ya Waislaam ya kupinga kufungwa kwa mwenzao aliyesema Yesu si Mungu mwaka 2001," inafafanua sehemu ya kitabu hicho.

  "Kiwe chama ambacho serikali yake haitakuwa tayari kupokea maagizo, sheria na misamiati mipya dhidi ya Waislaam kama vile magaidi au siasa kali na kuwasikiliza masheikh na maimamu pamoja na viongozi wengine wa taasisi za kiislaam."

  Awali katibu wa kamati ya siasa ya Shura ya Maimamu, Sheikh Ponda Issa Ponda alisema: "Muongozo (wa awali) umefanikiwa sana hasa mikoani, katika mikoa ya kanda ya kusini zaidi ya asilimia 90 ya viongozi walishinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ni Waislaam wanaojielewa."

  "Asilimia 75 ya wilaya zote za Tanzania zimefanya warsha na makongamano kuuchambua mwongozo, hotuba za Ijumaa zenye mwelekeo mmoja zimeanza jijini Dar es Salaam, Baraza Kuu la Wanawake wa Kiislaam limetanga kura ya maslahi kuwa ajenda yao kuu 2010 na Taasisi 15 zimesaini makubaliano ya pamoja kuelekea uchaguzi mkuu."

  Kwa mujibu wa sheikh Ponda, program mpya ya elimu ya uraia itatekelezwa katika mifumo ya machapisho, warsha, semina, makongamano, mikutano ya hadhara na hotuba kali za Ijumaa zenye mwelekeo mmoja katika miskiti yote nchini.

  Source: Mwananchi
   
 2. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakatoliki itawaudhi hiyo program. lakini nchi ni ya wote . You can fool some people some time But ou can't all the people all the time.
   
 3. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Jamani, si hawa watu walisema kutoa waraka ni kuchanganya siasa na dini, sasa wao wanafanya nini? Nashindwa kuwaelewa. Mara nyingi ni 'reactionaries', rarely wanakuwa 'constructive'.
   
 4. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nafikiri imekupita kidogo. Waislam walitoa mwongozo kuelekea uchaguzi mkuu. Sasa hiyo ni program ya mwongozo huo.
   
 5. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,073
  Likes Received: 4,001
  Trophy Points: 280
  Tujiulize kati ya hao masheikh wanaopigania haki ya Waislam ni wangapi hata wana diploma kujua haki ya kataba ya nchi kutobadilishwa?
   
 6. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Exactly, wao walipinga progarmme na waraka wa Wakatoliki wakisema ni kuchanganya dini na siasa. Na walisema mambo mengi sana 'negative' kuhusu Wakatoliki na Wakristo kwa ujumla.

  Hao hao leo wanakuja na similar issue na hawaoni kama walichowafanyia Wakatoliki wao wenyewe. Huo ni unafiki mkubwa. "Sisi hatufanyi hivi..." kumbe na wao wanafanya. Si wanadai Qur'an inajitoshereza haihitaji waraka wala mwongozo. Sasa mwongozo na programme ni vya nini, kama siyo fix tu.

  Kwenye psychology kuna 'expression' inaitwa 'split personality'. Ni mtu kusema kitu fulani na baadaye kusema hajasema hivyo. Au kupinga kitu na baadaye kukifanya kitu kilekile ulichokipinga.

  Mimi hainiingii akilini, unless waseme walichokuwa wanapinga ilikuwa geresha tu. Umenielewa? Nilitegemea wao wasingezindua mwongozo wala progarmme ili wawe mfano kwa wote. Lakini kumbe hawana jipya ni kuji'contradict' tu. What a shame!
   
 7. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  KAMATI ya Siasa ya Shura ya Maimamu jana ilizindua programu ya Elimu ya Uraia yenye lengo la kutekeleza kwa vitendo waraka wake kuhusu uchaguzi mkuu wa mwakani.

  Programu hiyo inataja sifa za msingi za chama na mgombea anayepaswa kuchaguliwa, masuala ambayo yalisababisha utata mkubwa baada ya nyaraka hizo za Shura ya Maimamu na Kanisa Katoliki kutolewa.

  Mpango huo umo kwenye kitabu cha kurasa 76 na unataka Waislaam kuutekeleza kwa vitendo mwongozo uliozinduliwa na kamati hiyo Agosti 26 mwaka huu.

  Programu hiyo ilizinduliwa jana kwenye Msikiti wa Mtoro jijini jijini Dar es Salaam na balozi wa zamani wa Tanzania katika nchi za Ufaransa na Italia, Abbass Sykes. Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, Sykes alisema: "Nchi hii ni ya Watanzania wote, hakuna chama wala mtu mwenye hati miliki ya kutawala nchi hii."

  Alisema kila chama na mtu bila ya kujali rangi, dini, kabila au mahali alipotoka, ana haki ya kuomba uongozi ili mradi awe amegombea nafasi ya uongozi kwa kufuata taratibu na sheria zilizopo.

  Sifa za mgombea zinatajwa katika mada nambari tano ya kitabu hicho cha 'Elimu ya Uraia' kikitaja bayana sifa za mgombea anayetakiwa kupigiwa kura na Waislamu. "Awe kiongozi mwadilifu, anayejua matatizo makuu ya nchi na wananchi na mjuzi wa kuyatatua.

  Matatizo makuu ya nchi ni udini, ubaguzi dhidi ya Waislaam au baadhi ya watu, rushwa, uchafuzi wa mkataba wa Muungano na ukosefu wa maadili kwa viongozi," inasema sehemu hiyo katika ukurasa wa 65.

  "Awe kiongozi mwenye utashi wa kuwasaidia wananchi wote bila ya kujali tofauti zao, ajali zaidi maslahi ya umma kuliko ya chama chake, awe tayari kusaidia urejeshaji wa haki za wananchi zilizotaifishwa na serikali ikiwa ni pamoja na shule, ardhi na majengo."

  Kitabu hicho kinaeleza kuwa ili mgombea apigiwe kura, anapaswa awe anafahamu haki na dhuruma walizofanyiwa Waislaam kwa kutotendewa haki sawa na dini nyingine na awe tayari kufuta makubaliano baina ya serikali na kanisa.

  "Kiongozi huyo lazima awe tayari kutomwaga damu ya Waislaam kama ilivyotokea mara kadhaa katika misikiti, maandamano ya kudai haki au katika mahubiri ya kidini."

  Kuhusu chama kinachostahili kuingia madarakani, kitabu hicho kinafafanua kuwa ni kile ambacho serikali yake haitawazuia Waislaam kufuata na kutangaza dini yao kwa uhuru na ambayo haitabadilisha sheria za Waislaam zinazohusu mambo ya mirathi, ndoa na talaka.

  Kamati hiyo ya siasa ya Shura ya Maimamu, ilikumbushia migogoro mbalimbali baina ya serikali na Waislaam na kwamba chama kinachofaa ni lazima kiwe tayari kuunda tume huru kuchunguza mauaji ya Waislaam yaliyotokea miaka iliyopita.

  "Kiwe chama ambacho serikali yake, itakubali kufanyika kwa uchunguzi wa mauaji ya waislaam katika maandamano ya kutetea Qur-an 1988, mauaji ya msikitini Morogoro 1994, mauaji ya kinyama msikitini Mwembechai 1998, mauaji ya imamu wa msikiti wa Mwembetanga 2001 na mauaji katika maandamano ya Waislaam ya kupinga kufungwa kwa mwenzao aliyesema Yesu si Mungu mwaka 2001," inafafanua sehemu ya kitabu hicho.

  "Kiwe chama ambacho serikali yake haitakuwa tayari kupokea maagizo, sheria na misamiati mipya dhidi ya Waislaam kama vile magaidi au siasa kali na kuwasikiliza masheikh na maimamu pamoja na viongozi wengine wa taasisi za kiislaam."

  Awali katibu wa kamati ya siasa ya Shura ya Maimamu, Sheikh Ponda Issa Ponda alisema: "Muongozo (wa awali) umefanikiwa sana hasa mikoani, katika mikoa ya kanda ya kusini zaidi ya asilimia 90 ya viongozi walishinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ni Waislaam wanaojielewa."

  "Asilimia 75 ya wilaya zote za Tanzania zimefanya warsha na makongamano kuuchambua mwongozo, hotuba za Ijumaa zenye mwelekeo mmoja zimeanza jijini Dar es Salaam, Baraza Kuu la Wanawake wa Kiislaam limetanga kura ya maslahi kuwa ajenda yao kuu 2010 na Taasisi 15 zimesaini makubaliano ya pamoja kuelekea uchaguzi mkuu."

  Kwa mujibu wa sheikh Ponda, program mpya ya elimu ya uraia itatekelezwa katika mifumo ya machapisho, warsha, semina, makongamano, mikutano ya hadhara na hotuba kali za Ijumaa zenye mwelekeo mmoja katika miskiti yote nchini.

  Source: Mwananchi
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Dec 7, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kama sifa ndio hizo za mgombea katika uchaguzi Mkuu wa mwakani basi sifa hizo za kidini hazifai kabisa kwa upande wa watu wasio waislamu. Hebu tuangalie sifa za kiongozi huyo anayetakiwa na Waislamu:

  1. "Awe kiongozi mwadilifu, anayejua matatizo makuu ya nchi na wananchi na mjuzi wa kuyatatua. Matatizo makuu ya nchi ni udini, ubaguzi dhidi ya Waislaam au baadhi ya watu, rushwa, uchafuzi wa mkataba wa Muungano na ukosefu wa maadili kwa viongozi."
  Hapa inaonekana kama vile sifa zilizotajwa ni general lakini kwa nini wamezungumzia kuhusu ubaguzi dhidhi ya waislamu (wametajwa kwa jina) halafu "na watu wengine." Hapa emphasis ni kiongozi anayelinda maslahi ya waislamu, hayo mengine ni geresha tu!

  2. ili mgombea apigiwe kura, anapaswa awe anafahamu haki na dhuruma walizofanyiwa Waislaam kwa kutotendewa haki sawa na dini nyingine na awe tayari kufuta makubaliano baina ya serikali na kanisa. Hapa anayezungumziwa ni kiongozi wa kitaifa au wa BAKWATA?

  3. "Kiongozi huyo lazima awe tayari kutomwaga damu ya Waislaam kama ilivyotokea mara kadhaa katika misikiti, maandamano ya kudai haki au katika mahubiri ya kidini." Kwa hiyo watu wa dini nyinginezo damu zao zinatakiwa zimwagwe? Na vilevile waislamu wakifanya fujo waachwe tu waendelee na fujo zao, eti kwa sababu ni waislamu?

  4. "Kiwe chama ambacho serikali yake, itakubali kufanyika kwa uchunguzi wa mauaji ya waislaam katika maandamano ya kutetea Qur-an 1988, mauaji ya msikitini Morogoro 1994, mauaji ya kinyama msikitini Mwembechai 1998, mauaji ya imamu wa msikiti wa Mwembetanga 2001 na mauaji katika maandamano ya Waislaam ya kupinga kufungwa kwa mwenzao aliyesema Yesu si Mungu mwaka 2001," inafafanua sehemu ya kitabu hicho. Mbona hawazungumzii juu ya uchunguzi wa uchomaji wa Kanisa huko Zanzibar?

  5. "Kiwe chama ambacho serikali yake haitakuwa tayari kupokea maagizo, sheria na misamiati mipya dhidi ya Waislaam kama vile magaidi au siasa kali na kuwasikiliza masheikh na maimamu pamoja na viongozi wengine wa taasisi za kiislaam." Kwa hiyo tuvumilie tu mabomu ya akina Osam bin Laden na magaidi mengine ya Kiislamu na kuyaita hiyo ni neema kutoka kwa Allah (aka Muhammad)?

  Jamani ukiangalia sifa za kiongozi anayetakiwa na Shura ya Maimamu, kwa kusoma between the lines, Kiongozi huyo lazima atakuwa ni Mwislamu. Sasa kama wenyewe wanapinga udini halafu wanaufagilia udini huo kwa mlango wa nyuma, huo sio unafiki ulioenda shule? Hatudanyanyiki!
   
 9. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,836
  Likes Received: 1,090
  Trophy Points: 280
  mkuu usipate shida kusoma kati ya mistari (btn the lines) aya hii hapa inaeleza lengo lao kwa uwazi.

  Lengo ni
  (1) kuwa na viongozi Waislam
  (2) kulipa kisasi ktk yale wanayohisi walionewa
  (3) kuifanya nchi ya kidini (kutambua na kutekeleza sheria za Kiislam)

  Ninawasiwasi jamaa wamebanwa mno kule Afghan na Paksistan sasa watatafuta new territory kama ilivyo Somalia.
   
 10. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mbona unaweka tafsiri yako mwenyewe wala siyo ya shura ya maimamu? nikupe ufafanuzi kwa ufupi wa maswali yako 1-5
  1. Muadilifu hawezi kuwa Mdini

  2. Anatakiwa awe anafahamu historia ya ubaguzi Tanzania hapo kuna tatizo gani? au wewe unapenda sana kupendelewa pasipo haki? ulishaona kupendelewa ni haki siyo?

  3.Tume huru inatakiwa kudhibitisha kama waislamu walianza kufanya fujo au walifanyiwa fujo kwa maagizo kutoka kwa watu wenye nia mbaya na nchi hii ambao wanaweza kukimbia nchi na kujificha huko wanakoficha waovu?? hapo kuna tatizo gani? kufanya uchunguzi ili jamii iridhike

  4. Uchunguzi wa kanisa kuchomwe ulishafanyika na wenye kanisa wameridhika na hatua zilizochukuliwa ndio maana hakuna malalamiko yeyote kutoka kwao lakini uchunguzi kwa upande wa waislamu haukufanyika na hawataki kufanya hivyo, shura inataka mtu ambaye hafichi uchafu huo awe mkristo au muislamu??

  5. kumzuia Osama bin laden na kazi yake chafu haina maana kuwanyima haki zao waislamu na kuwakandimizi kwa kutumia external forces..je wewe utafurahia kwasababu LRA wanafanya fujo uganda wakristo wote wa Tanzania watungiwe sheria mbaya?

  "Si kweli kwamba sifa ya kiongozi wa shura ya waislamu lazima awe muislamu ila ni Mtanzania mwenye kudhamini utu wa watu wote wakiwemo waislamu" hatundanganyiki na propanda zako...
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Lakini kilichonishangaza ni kuona mzee Abbas Sykes, mzalendo ninayemheshimu, kujihusisha naye na waraka huu.
   
 12. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Huu si waraka ila ni Mwongozo,

  Wazalendo ndio wanatakiwa washiriki zaidi kwakuwa una manufaa kwa jamii yetu yote.
   
 13. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri ujafatilia kadhia hii.
  Awali ya yote Wakatoliki walitoa waraka wao kuhusu uchaguzi. Waraka huo ulileta utata mkubwa sana kwa viongozi wa Serikali na hata wanasiasa. Tunajua wazi kila aliyejaribu kuupinga waraka ule aliandamwa kwa kejeli na matusi ,akubwa. Mfano, Mh Kingunge, na Askofu Kakobe.

  Waislam wao baada ya kuona waraka wao wakatoa MWONGOZO kuelekea uchaguzi mkuu. Mwangozo huo ulilaaniwa vikali sana na wakatoliki na wengine.

  Sasa waislam wametoa program ya kutekeleza mwongozo wao. Kwa bahati kubwa sana nipo Dar na nmeupata jioni hii hapa kariakoo msikiti wa Mtoro. Nitampa mke wangu aupitie na kuuchambua zaidi.

  wazo langu kama wakatoliki mna nia nzuri na TZ basi waacheni waislam na program yao. Au mna wasiwasi kuwa ile 73.4% ya wabunge wote katika bunge la muungano a,bao ni wenu sasa inawezekana ikapungua.

  Kutesa kwa zamu.
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  Dec 7, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Imekua vyema. Basi tusisikie kelele za muongozo wa Wakatoliki. Wao watekeleze programu yao na wawaache Wakatoliki watekeleze mipango yao.
   
 15. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0

  Kujihusisha kwake sio dhambi na wala sio kuvunja katiba.

  Kuzindua program hii ya mwongozo kunataka zaidi watu wenye nia nzuri na Tanzania. Kwani kwa kufata program ya mwongozo huu nafikiri Bunge lijalo litapunguza idadi ya mafisadi na wanafiki.
   
 16. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #16
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ni bora wawe hawana Diploma kuliko kuwa na zile za St.. St,, ambazo zinakubeba toka Certificate mpaka PhD.
   
 17. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #17
  Dec 7, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Haihitaji kwenda shule kuelewa kuwa Waraka wa Shura ya Maimamu unahimiza kuchaguliwa kwa Kiongozi mwislamu atakayevumilia mabomu ya magaidi Waislamu akina Osama bin Laden na washirika wake! Kama wanahitaji Kiongozi wa Waislamu si wangemchagua huko BAKWATA ili awaongoze Waislamu?
   
 18. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #18
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  maneno yako sawia kabisa yaa Alhaj.

  Pilipili yaliwa shamba wao yawawashiani.

  Program ya waislam basi waacheni na program yao.
   
 19. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #19
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Waislamu wazindua programu kutekeleza mwongozo wao 2010
  Salim Said

  KAMATI ya Siasa ya Shura ya Maimamu jana ilizindua programu ya Elimu ya Uraia yenye lengo la kutekeleza kwa vitendo waraka wake kuhusu uchaguzi mkuu wa mwakani.

  Programu hiyo inataja sifa za msingi za chama na mgombea anayepaswa kuchaguliwa, masuala ambayo yalisababisha utata mkubwa baada ya nyaraka hizo za Shura ya Maimamu na Kanisa Katoliki kutolewa.

  Mpango huo umo kwenye kitabu cha kurasa 76 na unataka Waislaam kuutekeleza kwa vitendo mwongozo uliozinduliwa na kamati hiyo Agosti 26 mwaka huu.

  Programu hiyo ilizinduliwa jana kwenye Msikiti wa Mtoro jijini jijini Dar es Salaam na balozi wa zamani wa Tanzania katika nchi za Ufaransa na Italia, Abbass Sykes. Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, Sykes alisema: "Nchi hii ni ya Watanzania wote, hakuna chama wala mtu mwenye hati miliki ya kutawala nchi hii."

  Alisema kila chama na mtu bila ya kujali rangi, dini, kabila au mahali alipotoka, ana haki ya kuomba uongozi ili mradi awe amegombea nafasi ya uongozi kwa kufuata taratibu na sheria zilizopo.

  Sifa za mgombea zinatajwa katika mada nambari tano ya kitabu hicho cha 'Elimu ya Uraia' kikitaja bayana sifa za mgombea anayetakiwa kupigiwa kura na Waislamu. "Awe kiongozi mwadilifu, anayejua matatizo makuu ya nchi na wananchi na mjuzi wa kuyatatua.

  Matatizo makuu ya nchi ni udini, ubaguzi dhidi ya Waislaam au baadhi ya watu, rushwa, uchafuzi wa mkataba wa Muungano na ukosefu wa maadili kwa viongozi," inasema sehemu hiyo katika ukurasa wa 65.

  "Awe kiongozi mwenye utashi wa kuwasaidia wananchi wote bila ya kujali tofauti zao, ajali zaidi maslahi ya umma kuliko ya chama chake, awe tayari kusaidia urejeshaji wa haki za wananchi zilizotaifishwa na serikali ikiwa ni pamoja na shule, ardhi na majengo."

  Kitabu hicho kinaeleza kuwa ili mgombea apigiwe kura, anapaswa awe anafahamu haki na dhuruma walizofanyiwa Waislaam kwa kutotendewa haki sawa na dini nyingine na awe tayari kufuta makubaliano baina ya serikali na kanisa.

  "Kiongozi huyo lazima awe tayari kutomwaga damu ya Waislaam kama ilivyotokea mara kadhaa katika misikiti, maandamano ya kudai haki au katika mahubiri ya kidini."

  Kuhusu chama kinachostahili kuingia madarakani, kitabu hicho kinafafanua kuwa ni kile ambacho serikali yake haitawazuia Waislaam kufuata na kutangaza dini yao kwa uhuru na ambayo haitabadilisha sheria za Waislaam zinazohusu mambo ya mirathi, ndoa na talaka.

  Kamati hiyo ya siasa ya Shura ya Maimamu, ilikumbushia migogoro mbalimbali baina ya serikali na Waislaam na kwamba chama kinachofaa ni lazima kiwe tayari kuunda tume huru kuchunguza mauaji ya Waislaam yaliyotokea miaka iliyopita.

  "Kiwe chama ambacho serikali yake, itakubali kufanyika kwa uchunguzi wa mauaji ya waislaam katika maandamano ya kutetea Qur-an 1988, mauaji ya msikitini Morogoro 1994, mauaji ya kinyama msikitini Mwembechai 1998, mauaji ya imamu wa msikiti wa Mwembetanga 2001 na mauaji katika maandamano ya Waislaam ya kupinga kufungwa kwa mwenzao aliyesema Yesu si Mungu mwaka 2001," inafafanua sehemu ya kitabu hicho.

  "Kiwe chama ambacho serikali yake haitakuwa tayari kupokea maagizo, sheria na misamiati mipya dhidi ya Waislaam kama vile magaidi au siasa kali na kuwasikiliza masheikh na maimamu pamoja na viongozi wengine wa taasisi za kiislaam."

  Awali katibu wa kamati ya siasa ya Shura ya Maimamu, Sheikh Ponda Issa Ponda alisema: "Muongozo (wa awali) umefanikiwa sana hasa mikoani, katika mikoa ya kanda ya kusini zaidi ya asilimia 90 ya viongozi walishinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ni Waislaam wanaojielewa."

  "Asilimia 75 ya wilaya zote za Tanzania zimefanya warsha na makongamano kuuchambua mwongozo, hotuba za Ijumaa zenye mwelekeo mmoja zimeanza jijini Dar es Salaam, Baraza Kuu la Wanawake wa Kiislaam limetanga kura ya maslahi kuwa ajenda yao kuu 2010 na Taasisi 15 zimesaini makubaliano ya pamoja kuelekea uchaguzi mkuu."

  Kwa mujibu wa sheikh Ponda, program mpya ya elimu ya uraia itatekelezwa katika mifumo ya machapisho, warsha, semina, makongamano, mikutano ya hadhara na hotuba kali za Ijumaa zenye mwelekeo mmoja katika miskiti yote nchini.
   
 20. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #20
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  imeshindwa kujibu hoja unakuja kutisha watu hapa..hatudanganyiki!

  shura inataka kiongozi wa kitaifa, muadilifu mwenye kufahamu historia sahihi ya Tanzania, mwenye kujua kwamba ubaguzi ni aibu taifa...na ustawi wake...what is bakwata bana toa hoja ndugu??
   
Loading...