Waislam nijibuni hili

Hata gharama ya hospitali ikiwa ndogo mara mia kuliko ya msikiti, katika sehemu yenye misikiti mia na isiyo na hospitali.

Mtu akiamua, kwa hela zake, kujenga msikiti wa mia moja na moja, wakati hajaamua kujenga hospitali. Ni haki yake.

Ukiona kakosea. Usimseme.

Tafuta hela yako, jenga hospitali.

Onesha kakosea kwa matendo. Kwa hela yako.

Usimpangie mtu cha kufanya kwa hela yake mwenyewe.

Kwa sababu, hata wewe unayeona hospitali ni muhimu kuliko msikiti sehemu hiyo, ukiamua kujenga hospitali, kwa hela yako, halafu mtu mwingine akakupangia ujenge msikiti, kitu unachoona hakihitajiki na si matakwa yako, hutafurahi.

Kila mtu ajenge anachotaka, kwa hela yake, bila kubugudhiwa.

Kama unaona shule ni muhimu, hujakatazwa kujenga shule. Jenga.

Kama unaona hospitali ni muhimu, hujakatazwa kujenga hospitali. Jenga.

Kama unaona msikiti ni muhimu, hujakatazwa, jenga.

Kama unaona kanisa ni muhimu, hujakatazwa, jenga.

Hata ukitaka kujengea spaceship la kwenda sayari nyingine, jenga.

Sasa ya nini kumshupalia mtu anayetumia hela yake kujenga anachotaka yeye?

Unajuaje hiyo shule au hospitali ni muhimu kwake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya
 
Hamna cha amali. Mtu ajenge misikiti hata kujaza dunia lakini akawa na mambo ya ajabu ajabu adhabu yake iko pale pale.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ndie unaehukumu au yupo anaehukumu?
Je unaijua nafsi ya mtu ? Je kama atatubia?
Mbona nyie mnakwenda kutubu kila jumapili?
Mnasema yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zenu iweje bado mna dhambi?

Cᵃʳᵉᵉᵐ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿD
 
Moja ya sababu kubwa ya umasikini ni tabia ya kupenda wengine wakufanyie unachotaka wewe bila ya wewe mwenyewe kufanya hicho specific unachotaka kifanyike.

Tabia hii inaendana na kutaka watu wengine watumie hela zao kufanya unachotaka wewe kifanyike. Kama kumtaka mtu baki ajenge shule au hospitali unayotaka wewe, badala ya msikiti anaotaka yeye.

Ni umasikini wa mawazo, ni ufukara wa fikira, ni kilema cha akili.

Action speaks louder than words.

Show. Don't tell.


When you have to shoot, shoot. Don't talk.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Indonesia ndio nchi yenye idadi kubwa ya waislamu duniani,kuna vita?au Brunei amani IPO au haipo, nchi ambayo serikali yake ni tajiri inamlipia kila mwanaume safari ya kwenda hijja.uwe una acha kudanganya hadharani.
Acha Ujinga huko unakosema ni Mashariki ya kati???Elewa nimesema Mashariki ya kati nakupa tena nafasi taja nchi yoyote ya Mashariki yenye amani kama Tanzania!!!!
 
Nadhani wengi wakikuelewa vizuri hii ndo ingekua conclusion. Hizi dini tumeletewa tukazikumbatia. Waliotuletea wakatuacha tunazihusudu na kupigana kwa sababu ya hizo dini, wao wakaendelea kusogea mbele (Tumekua kama mmbwa aliyetupiwa mfupa akabaki ameng'ang'ana nao mwizi akaendelea kuiba.

Ndugu zangu waislamu acheni kufuata msichojua kikoje. Walioleta uislamu kwenye nchi zao wanafanya biashara kubwa kubwa na kujenga viwanda kila kukicha. Huku mmeaminishwa kujikita kwenye elim akhera na kusababisha wengi kukosa ufaham wa dunia inavyokwenda.

C kwenu tu. Hata kwa wakristo tunaibiwa sana kwa sababu tu ya kukosa kunyenyekea dini huku ukweli ukiwa unajulikana.

Fungukeni wapendwa. Achaneni na mapokeo. Najua yapo yenye maana ila inabidi kufungua akili ili uweze kuyachuja
Sent using Jamii Forums mobile app
 
KCMC Hospital na nyingine nyingi.

Mueleweshe huyu ndugu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nn wasikupe msaada wa shule, kiwanda, hospitali, n.k. Kwa nn misikiti tu. Utasema kukujenge misikiti wanajenga akhera yao. Sawa

Sasa, kwa nn wasijenge kule kwao wewe wakusukumie kuabudu wao wajivutie biashara na maendeleo.

Funguka akili
Nahisi una uvimbe kichwani. Hayo ya kwao lakini misaada wanayotoa inalenga kujenga akhera zao. Una jipya?!

Cᵃʳᵉᵉᵐ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿD

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatzo mnaoelewa haya mambo ni wachache sana. Wengi wamebase kwenye isue ya KUTENGENEZA AKHERA. Waneshindwa kuwa na ufahamu ulio nao wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani hasa nyie mnawashwa na nini sisi tukijengewa miskiti?? Si muwaambie na nyie watu wenu wawajengee makanisa!

Cᵃʳᵉᵉᵐ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿD
 
Kwani hasa nyie mnawashwa na nini sisi tukijengewa miskiti?? Si muwaambie na nyie watu wenu wawajengee makanisa!

Cᵃʳᵉᵉᵐ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿD
Mtu baki anaposhindwa kufanya unachoona kinatakiwa kufanyika, kitu cha maana kabisa hapo ni wewe unayeona hajafanya kinachotakiwa kufanyika ukifanye, halafu yeye aone kwa mfano.

Sio kuleta maneno mengi hajafanya hiki au kile.

Ukileta maneno sana hapo utaonekana inawezekana una propaganda zako na ajenda binafsi ambayo huisemi.

Wanaoona kuna haja ya shule kujengwa, wajenge shule. Hawajakatazwa.

Wanaoona kuna haja ya hospitali kujengwa, wajenge hospitali. Hawajakatazwa.

Wanaoona kuna haja ya misikiti kujengwa, wajenge misikiti. Hawajakatazwa.

Wanaotaka kuchezea kamari hela zao, wachezee kamari, hawajakatazwa.

Ili mradi wanatumia hela zao na hawamuingilii mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo hata mkijenga shule
Au vyuo hamjengi vya elimu ya kawaida...kwa shule utakuta shule inakuwa maarufu kwaajili ya elimu ya dini na maadili au kubanwa kwa wanafunzi wala sio ufaulu...na upande wa vyuo vingi utakuta vyuo vya dini,,,hii inapelekea hata wazazi kutopeleka watoto wao kwa wingi huko...
Hili nalo linahitaji marekebisho
Maendeleo hayana dini
 
Wanaolalamika waache walalamike.

Kulalamika ni sehemu ya haki za kikatiba za Watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muhammad alianzisha shule au hospitali???
Uislam haukukua kwa diplomacy ndugu bali fuatilia historia ya vita vya Ridda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…