Kinyungu,
Mimi jana nilisema mara nyingi Kikwete alikuwa anababaika kujibu, hapa Godon alimuuliza swali la msingi "Nowadays IT technology and education is moving faster, how quick can move education forwad in Africa" Nafikiri Kikwete hakulitegemea swali hili akaanza kwa kujikanyaga kanyaga namnukuru "Yes ofcource we....first let me say about infrastructure......." hadi mwisho hakujibu swali la msingi akaishia kusema Afrika haina idadi kubwa ya magari.
Mimi nafikiri tuna tatizo kubwa rais wetu hana uwezo wa kuchambua mambo seriously kama kwa mfano PM wa Ethiopia Zenawi alivyokuwa anachambua. Ndio maana wazungu wamemsoma IQ yake wakagundua hana vision yeyote ya kuiletea maendeleo nchi yake, na wao wamegundua kumbe lengo lake lilikuwa kupata urais tu. Kwa hiyo kama wamegundua na wanatusaidia kumkosoa tusiwalaumu kwa vile bakuli tunalotembeza linajazwa kwa kodi zao.
Hayo ndo madhara ya kuchagua viongozi kwa ZAMU,eti safari hii zamu ya waislamu, cjui akristo, wapagani nk nk, mara jinsia..! na hayuko peke yake wako wengi sana ccm, spika, pm..ongeza orodha!