Waimbaji wa Nyimbo za Injili Mrudieni Mungu

jnuswe

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,270
549
Kichwa hicho hapo juu kinafaa sina namna ninavyoweza kueleza kwa kinachoendelea , watu wamejisahau wameshindwa kujua nguvu na siri kubwa ya Kimungu iliyoko kwenye uimbaji wa nyimbo za Injili. Wameamua kujichanganya na ulimwengu kabisa. Inasikitisha sana

Najua sio wote waliharibika lakini ninachoweza kusema asilimia kubwa wameharibika. Sijaelewa kabisa kinachoendelea , eti kuna umoja/shirikisho la wanamuziki Tanzania, ambapo waimbaji wa nyimbo za Injili na zile za dunia wanakutana pamoja kujadili muziki na uimbaji, Ole wa dunia. Nimesikitishwa na kitendo hiki sana na zaidi tuombeane Mungu aweze kudhihirika, Uwezi ukachanganya nuru na giza kamwe haitakuja kutokea na ikakubalika

Ni nyakati za Mwisho, Mungu atupe macho ya kuliona hili
 
Hata mm nakuunga mkono sijui jambo hili linatoka wapi, kama umoja wao wenyewe wameshindwa itakuwa huo wa mchanganyiko? Na siku hizi wanajipa vyeo eti Malkia wa uimbaji namba moja, mulemule jamani waimbaji wa Injili someni neno
 
Umeongea kweli tupu. Hawa waimbaji wetu wa injili waendako siko wanapotea kabisa.
 
Sema waimbaji wa ilInjili wa kilokole huwezi kuwakuta SDA na RC kwenye hivyo vyama vyao na wanamuziki wa kidunia.
 
we nawe ile si kazi kama kazi nyingine wapi ilipoandikwa kuwa mtu ataenda peponi kwa kuimba na si matendo yake wacha wapige hela wavae wanavyotaka tumieni fulsa twen'zetu
 
Sijaona ubaya hapo...Kwani lengo lao la kukutana ni nini..???? Wote wanauza kazi zao kwa jamii hii hii...

Kazi za wasanii zinaibiwa haijalishi ni Wanjili au Wakidunia...Wamekutana ili kujadili jinsi ya kuzuia uibaji wa kazi zao..
 
Nilishapiga stop kutoa pesa yangu et nanunua nyimbo za injiri za kazi gani? za hawa wasani? si kama ni wokuvu bora nibaki na biblia yangu

Washaisha hivyo,walianza wanajipodoa watu walivyosema wakasema vipodozi si ishu sasa wanashindana kukaa uchi na wanaandaa vikao na shetani eti kuongelea muziki ..My God!!
 
Hawa wote ni wasanii,tofauti ni aina ya usanii tu. wameungana ili kudhibiti wizi wa kazi zao na sio katika uimbaji..
 
Moto na Jehunam inawangoja wote wanaotoza watu mahubir na matamasha yao ni upagani mkubwa wamrudie MUNGU.
 
Yani umeongea kweli kabisaaa kwa kweli nyimbo za injili za sikuhiz mm zinanikwaza sana kwanza zimekosa utukufu unakuta eti mtu anaimba kwa kutumia melody za taarabu au ndombolo mara wanarap yani imefikia sasahv nyimbo za dunia na za Mungu hazina tofauti huo uvaaji na uchezaji loh, no wonder sikuhz zinapigwa hadi kwenye ma bar me nafikir waimba injili wamebak wachache wengi ni wasanii tu wanatafuta rizki na wamesoma nyakati manake nyakat za sasa hzo nyimbo za injili zina soko sana
 
Kichwa hicho hapo juu kinafaa sina namna ninavyoweza kueleza kwa kinachoendelea , watu wamejisahau wameshindwa kujua nguvu na siri kubwa ya Kimungu iliyoko kwenye uimbaji wa nyimbo za Injili. Wameamua kujichanganya na ulimwengu kabisa. Inasikitisha sana

Najua sio wote waliharibika lakini ninachoweza kusema asilimia kubwa wameharibika. Sijaelewa kabisa kinachoendelea , eti kuna umoja/shirikisho la wanamuziki Tanzania, ambapo waimbaji wa nyimbo za Injili na zile za dunia wanakutana pamoja kujadili muziki na uimbaji, Ole wa dunia. Nimesikitishwa na kitendo hiki sana na zaidi tuombeane Mungu aweze kudhihirika, Uwezi ukachanganya nuru na giza kamwe haitakuja kutokea na ikakubalika

Ni nyakati za Mwisho, Mungu atupe macho ya kuliona hili

Hivi Yesu alikuja kwa kina nani?
 
Kwani wanaimba injili? Rose Mhando,flora mbasha na wenye miziki kama hiyo wote ni sawa na El saadat na Ali choki.
 
Back
Top Bottom