Kwenu Waislam mnaopenda kusikiliza nyimbo za Injili

Mr sule

JF-Expert Member
Oct 14, 2021
607
1,097
Naomba kujua.

Unapokuwa muislam alafu unapenda kusikiliza nyimbo za injili, hii huwa ina maana gani katika Imani?

Nimekutana na waislam wengi wanapenda sana kusikiliza nyimbo za injili, na kufurahia maneno ya kumtukuza Mungu katika Imani ya Krsito.

Naomba kujua hiyo yafsiri yake ni nini?
 
Nyimbo za injili za hasa za siku hizi zimekaa kibongo fleva hiyo mtu unakuta anapenda kusikia mdundo wa nyimbo na sio maneno yanayo ibwa, mfano mm ni mpenzi mkubwa wa nyimbo za kilingala lakini kinacho imbagwa mule sikielewagi.
 
Naomba kujua.

Unapokuwa muislam alafu unapenda kusikiliza nyimbo za injili, hii huwa ina maana gani katika Imani?.

Nimekutana na waislam wengi wanapenda sana kusikiliza nyimbo za injili, na kufurahia maneno ya kumtukuza Mungu katika Imani ya Krsito.

Naomba kujua hiyo yafsiri yake ni nini?
Tafsiri yake ni Upendo kwa wote wamchao Mungu!
 
Mungu hana upendeleo, Kwenye imani ya kikristo Mungu ni pendo apenda wote na hakuna ubaguzi kuamini hivyo. Shangaa muislam anaweza kuingia kanisani na akajumuika na waumini huko kwa upendo mkubwa na asipate misukosuko walau kubadilishwa dini bila ridhaa yake.

Huwezi kuingia msikitini kirahisi ukaribishwe kwa furaha lazima utapata misukosuko uliingia kufanya nini na huku kuswali sala zao hujui. Utasilimishwa kwa lazima utake usitake. Kanisani kuna kipindi cha kukaribisha wageni unataja jina lako wapi unatoka na wapi unasali. Baada ya ibada kama kuna muda wa kutosha mchungaji mwenyeji atataka kufahamiana zaidi na wageni walienda pale, je wanahamia au wanapita
 
Umenikumbusha sekondari, kuna jamaa alikua muislamu, ila alikua anaupenda ukatoliki sana, alikua hadi anatumikia kwenye misa, anasoma bibilia mwenyewe, anasali rosari, ila kitimoto alikua hali. Alikua mtu wa ajabu sana.
Yaani hao wa kitimoto ninao kibao ijumaa akitoka msikitini jioni tupo tunakula kitimoto,

Nipo na mshkaji wangu mzanzibar yeye anaishi znz kila ikifika kipindi cha mwezi ramadhani cha kufunga anakuja huku bara kwa dada yake, anakuambia sahivi kula kitimoto kule ni shida sana😂.
 
Naomba kujua.

Unapokuwa muislam alafu unapenda kusikiliza nyimbo za injili, hii huwa ina maana gani katika Imani?.

Nimekutana na waislam wengi wanapenda sana kusikiliza nyimbo za injili, na kufurahia maneno ya kumtukuza Mungu katika Imani ya Krsito.

Naomba kujua hiyo yafsiri yake ni nini?

Nafikiri wanasikiliza tu kama vile mtu anavyoweza kusikiliza nyimbo za kilingala, kihindi nk na akaburudika.

Lakini pia nyimbo za kuabudu nyingi zina ujumbe murua wa kutukuza ukuu wa Mungu japo pale baadhi ya kwaya wanapoimba kuwa; Yesu ni mwana wa Mungu au Yesu ni Mungu, hapo ndipo Waislam huzidelete kwani ni kinyume kabisa na imani yao.

Waislamu humtambua Yesu kama Mtume wa Mungu (aliyekuja kufikisha ujumbe wa Mungu) na alikuwa anafanya miujiza konki kwa uwezo wa Mungu.

Nyongeza; Historia ya Yesu ipo kwa kirefu zaidi kwa Waislam ambapo unaweza kusoma maisha ya Yesu katika hatua mbalimbali tangia utotoni na miujiza aliyofanya katika hatua tofauti tofauti hadi alipokua; wakati kwenye Biblia unasoma Yesu alipozaliwa, unakuja kukutana naye tena akihubiri.
 
Naomba kujua.

Unapokuwa muislam alafu unapenda kusikiliza nyimbo za injili, hii huwa ina maana gani katika Imani?.

Nimekutana na waislam wengi wanapenda sana kusikiliza nyimbo za injili, na kufurahia maneno ya kumtukuza Mungu katika Imani ya Krsito.

Naomba kujua hiyo yafsiri yake ni nini?
Huko Zambia na Malawi,ngoma za rose muhando zinagongwa club na baa,siku za nyuma ngoma za makoma hazikua na tofauti na za Koffi Olomide,tulibang bila kujua Kama ni injili,Sasa goma Kama 'matendo' utaachaje kulisikiliza,wanafuata vibe
 
Back
Top Bottom