Waholanzi Watengeneza Virusi Vya Kuua Wanadamu

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Waholanzi Watengeneza Virusi Vya Kuua Wanadamu

Wataalamu wa Uholanzi wametengeneza virusi vinavyotishia maisha ya nusu ya watu wote duniani. Habari hiyo imefichuliwa na gazeti la Corriere della Sera la Italia ambalo limetangaza kuwa wahakiki wa Kituo cha Tiba cha Erasmus nchini Uholanzi wametengeneza virusi vya kuambukiza vinavyoweza kuua nusu ya watu wote duniani.

Gazeti hilo limeandika kuwa virusi hivyo ni aina ya virusi vya mafua ya ndege vya H5N1 na kwamba vina uwezo wa kuambukizwa kwa kasi kubwa kwa mamilioni ya watu na kuenea haraka kote duniani.

Mtaalamu wa Kituo cha Tiba cha Erasmus nchini Uholanzi Ron Fouchier amesema kuwa kirusi hicho kimepatikana kwa kufanya mabadiliko ya kijeni katika kirusi cha H5N1. Ameongeza kuwa kirusi hicho ni miongoni mwa virusi hatari mno ambavyo vimekwishatengenezwa hadi sasa duniani.

Utengenezaji wa kirusi hicho hatari kwa maisha ya mwanadamu umezusha wasiwasi mkubwa huku wataalamu wakihoji hekima na sababu ya kupoteza mamilioni ya fedha kwa ajili ya kufanya utafiti kama huo.

doctortipster said:

A Dutch researcher has created a virus with the potential to kill half of the planet’s population. Now, researchers and experts in bioterrorism debate whether it is a good idea to publish the virus creation ”recipe”. However, several voices argue that such research should have not happened in the first place.

The virus is a strain of avian influenza H5N1 genetically modified to be extremely contagious. It was created by researcher Ron Fouchier of the Erasmus Medical Center Rotterdam, Netherlands. The work was first presented at a conference dedicated to influenza, that took place in September in Malta.

Avian influenza emerged in Asia about 10 years ago. Since then there were fewer than 600 infection cases reported in humans. On the other hand, Fouchier’s genetically modified strain is extremely contagious and dangerous, killing about 50% of infected patients. The former strain did not represent a global threat, as transmission from human to human is rare. Or, at least, it was before Fouchier genetically modified it.

Fouchier and his team used a pair of ferrets for testing because they react in similar ways as humans, when exposed to the flu virus. Researchers transmitted the deadly virus from one ferret to another, in order to make the virus more adaptable to a new host. After 10 generations, the virus has mutated allowing it to spread through air. The result was that ferrets could get sick just being near another infected animal.

A genetic study showed that new virus strain presented five mutations, and all could be also observed in nature - but only separately, not all five combined. Fouchier’s strain is as contagious as seasonal human influenza, which kills tens of thousands of people, just that, much more lethal.

doctortipster
 
Ni wazi kuwa wameona idadi ya watu inazidi kwa kasi duniani. Lakini wanaozidi kwa kasi ya ajabu sio wazungu, ni hizi jamii za yellow, brown, blacks.
Ukuaji na ongezeko hili la watu wa rangi ni tishio kwa "race teule!". Walishaanza kuvijaribu kuvieneza virusi hivyo kwa majaribio kuna siku wataviachia visambae hasa katika hizo nchi za warangi.
 
Akili nyingi huondoa maarifa...hasara kwetu tunaotegemea kudra za Mwenyezi Mungu kutupa mkate wa kesho...
 
Kuna source zingine zaidi ya hiyo article hapo? St Ivuga we umeziskia wapi?Ni government yenyewe au ni pharmaceutical firm?
 
kwani wazungu hawafi???? Sidhani kama wakiua watu wa rangi zingine zote then watabakia na faida yoyote.....mtu akisha kufa that's the end of his/her life cycle. Wanaobaki ndo wanababaika...... fikiria wasomali/al-caeda walipo waua askari a marekani na kuwaburuza barabarani...... mbona bado wasomali ni maskini tu?????

Pia hili linanikumbusha niliwahi kuandika kuwa HIV virus imetengenezwa huko Cancer research intitute marekani..... nikabishiwa mno..... sasa tutambue kuwa HIV ni mradi wa UN na mataifa makubwa.
 
Uhai wa mtu upo mikonöni mwa Mungu tu,akisema hata aliyepewa hicho kijidudu apone anapona,im not worried,everything that hapens hapen for a reason
 
Uhai wa mtu upo mikonöni mwa Mungu tu,akisema hata aliyepewa hicho kijidudu apone anapona,im not worried,everything that hapens hapen for a reason
umesahau kuwa MUNGU huruhusu mateso kwa watu wake? Unafikiri kwa YESU ni tambarare eeh? Angalia kwa sababu ya kumezeshwa kwako imani usije ikana imani kwa shida. Ni hayo tu.
 
Nadhani huu ni muendelezo wa yale aliyoyasema Botha kwenye hotuba yake wakati akiwa rais wa SA juu ya mkakati walioweka ili kupunguza idadi ya weusi.Tangu nisome hotuba ile sina imani na misaada ya yoyote ya huduma za afya kutoka kwa wazungu.Huwa najiuliza sana kwanini waathirika wakubwa wa ukimwi ni waafrika?
 
Nadhani huu ni muendelezo wa yale aliyoyasema Botha kwenye hotuba yake wakati akiwa rais wa SA juu ya mkakati walioweka ili kupunguza idadi ya weusi.Tangu nisome hotuba ile sina imani na misaada ya yoyote ya huduma za afya kutoka kwa wazungu.Huwa najiuliza sana kwanini waathirika wakubwa wa ukimwi ni waafrika?

huo ni mpango mzima wa freemarsons.

Ngoja kwanza nimtume kijana aende kuniletea DICLOPAR (dawa ya maumivu makali)
 
Back
Top Bottom