Wahitimu wa Tanzania hamuajiriki

Wahitimu wa Tanzania hamuajiriki

Kwa ushauri wangu tu, nawaasa vijana wa Kitanzania wajizoeshe na wapendelee sana kujisomea vitabu mbali mbali, magazeti mbali ya ndani na nje ya nchi, hususan ya lugha za kigeni, iwe ni hobby yao kujisomea wawapo, kuanzia mashuleni, vyuoni hadi majumbani.

Usilale hata siku moja bila kujisomea japo nusu saa tu, chochote kile.

Kujisomea vitabu mbali mbali kunakuza uelewa, muono na lugha, na wasibaki kwenye vitabu vya masomo yao tu.
 
Sema hakuwepo muislamu katika list ya hao sita, maana wewe mdini ile mbaya, ukisikia majina ya kikristo akili inakuhama kama alshabab vile.
Alafu hayo ni matokeo ya serikali yako isiyoheshimu professionals na kutumbukiza siasa katika mambo ya professional
 
Corse ya kuandika barua alimaarufu communication skills vyuo ving huwa inafundishwa semista moja tuu ya mwaka wa kwanza na mtu unakuta anamiaka mitatu au mnne ndo anamalza unadhani atakumbuka kweli kuandika cv au official letter? Sasa change inabidi ianzie vyuoni ikiwezekana ilo somo lisomwe semista zote mwanafunzi awapo chuoni

Ukishapewa course yoyote ile unatakiwa uendelee mwenyewe kwa kufanya mazoezi, hakuna chuo kitakufundisha communications skills kila siku.

Nnawashauri vijana msome kitabu cha Dale Carnegie, How to win Friends and Influential People. Kinafundisha si kuandika barua bali mbinu nyingi nyingine za ku "communicate effectively" kila siku.
 
Wewe ni msomali?

mm ni Mtanzania halisi, lakn Miafrika ya Tanzania ni mijinga sana, eti mtu anaomba ruhusa aende kwenye send off ya mtu asiye mfahamu, msiba wa ndugu ya shoga yake, n.k mbona wenzetu wa kenya hawafanyi hivyo?
 
Na "ukweli ni ule unaoamini na sio unaoambiwa"
Happy Easter..
Unaweza ukawa unaamini wrong concepts mkuu....Hivi unadhani on-job training zinahitaji ku-orrient watu hata uandishi wa barua ama repoti?Mbona hayo ni mambo very basic?Sasa nini maana ya kuwa na degree ya miaka 3 kama hata a simple office correspondence unatakiwa ufundishwe?Kama hilo ni gumu je ukipewa kazi ya kuandaa lets say sera ya manunuzi ya kampuni yako mpya utaanzia wapi...kama barua ya kujibu wateja tu inakushinda?THINK AGAIN!
 
Kwamba sisi hatuajiriki, sawa lakini kwa wengine ambao tumewahi kufanya kazi pamoja na hao wanaoajirika wala sikuwahi kuona tofauti kati ya hao wanaoajirika na sisi tusioajirika zaidi ya mbwembwe za Kiingereza ambazo, wengine huwa hatuoni maana yake kupiga ngeli hata pasipohusika ili mradi tu u-prove kwamba wewe ni mtaalamu wa lugha!

Pamoja na itangulizi, napata shaka kuiamini habari ya mleta mada! Inawezekana hatuajiriki lakini ni upumbavu uliovuka mipaka ya upumbavu kusema mhitimu wa chuo kikuu Tanzania bado hafahamu kwamba, panapo maombo ya kazi, cover letter na CV ni lazima unless kama umeambiwa kutoambatanisha vitu hivyo hususani cover letter! Si tu kwamba maombo kama hayo hayawezi kutumwa na graduate hata kama angekuwa anatoka kwenye chuo kikuu kibovu kuliko vyote Tanzania bali pia haiingii akilini kwamba huyo mhitimu hajawahi kuongea hata na wenzake na kuona ni nini na nini kinatakiwa kwenye maombi ya kazi! Hivi inawezekana vipi, barua za kazi ambazo watu wanafundishwa tangia O-level mtu aache kuiandika huku tayari akiwa na shahada, tena shahada! Huu ni ujinga; ujinga unaolenga kuonesha kwamba Watanzania ni very stupid! It's very unfortunate kwamba na Watanzania wenyewe wanapokutana na ujinga huu huwa wanaamini na hivyo kujiona ni kama wasio chochote wala lolote kiasi cha kujiona ni kama inferior mbele ya mataifa jirani!

Hebu tujiulize, hususani wale wanafunzi na wahitimu wa SAUT... ina maana hiki chuo hakina kompyuta za bure ambazo zimeunganishwa na internet huku nikijilazimisha kuamini kwamba mhusika hana hata simu yenye uwezo wa access internet? Hivi ni nini wanafunz wanaotarajia ku-graduate huwa wanahangaika nacho wakiwa bado chuoni zaidi ya job search techniques? Hivi kweli inaingia akilini, mtu anayesomea marketing na public relations aifahamu umuhimu wa cover letter na CV wakati kazi anayoandaliwa nayo itakuwa ni ya ku-work out na official letters? Ina maana huyi mtu hajawahi kusoma kitabu chochote?

This's stupid, I repeat, it's very stupid! Hata hao wanaosema Watanzania hawajiriki, wafanyakazi wengi wa kampuni zao ni Watanzania! Ikiwa Watanzania ni stupid kiasi hicho, inakuwaje tena shughuli zao zinaendelea kama kawaida? Binafsi nilishawahi kuhudhuria interview iliyokuwa inaendeshwa na raia wa nchi fulani ambao ni hodari sana kuwakashifu Watanzania! Wakati naenda pale, nilidhani tumeitwa kwa session... nafika pale nakuta interviewees wote tumeitwa kwa pamoja! Nikaenda kwa wahusika kuuliza ikiwa ni written interview au nini lakini wakanijubu ni oral... yaani aingie mmoja baada ya mwingine... what a stupid!

Nikawaambia wazi kwamba siwezi kusubiria foleni ya kuwa interviewed! Lakini hawa nao wakikutana na Watanzania vilaza wakipewa sumu kwamba nyie Watanzania you're so dumb, na yenyewe kama mazuzu yanakubali tu bila kujiuliza what's so special coming from those smart fellows! Juzi hapa, in less than a week, nikakutana na Mkenya mmoja... hanijui wala simjui! Katika tu ile kuanza kufahamiana, akaanza kuponda Watanzania! Nikajitahidi kumvumilia hivyo hivyo! Hatimae kuna issue ilibidi itukutanishe pamoja... huku mie nikiwa ndie naifahamu hiyo issue kisha nimuelekeze! Alinipa headache kiasi cha kumwambia tusitishe hili zoezi na tuelekezane kesho! Sikuwa na huo mpango zaidi ya jana kupokea SMS yake ya kuniuliza mbona nipo kimya nami bila kusita nikamjibu am busy!

Lakini Mkenya huyu akipata nafasi mahali, nae ataanza kuongea kwamba Watanzania are so dumb na nyinyi mnakubali tu! Kama Watanzania ni so dumba kiasi hicho, kuna wageni wangapi CRDB, NMB, NBC, NHC, NSSF, TSPF, PPF, n.k? Yaani huko kote wafanye vizuri lakini wakija kwenye kampuni za kuuza vyombo, sabuni, masufuria na upuuzi mwingine kama huo ndio waonekane are just dumbs? By the way, hata kama hiyo habari ingekuwa ni kweli, hivi inatosha kuhitimisha kwamba Wahitimu wa Tanzania hawaajiriki?
 
mm ni Mtanzania halisi, lakn Miafrika ya Tanzania ni mijinga sana, eti mtu anaomba ruhusa aende kwenye send off ya mtu asiye mfahamu, msiba wa ndugu ya shoga yake, n.k mbona wenzetu wa kenya hawafanyi hivyo?

na wewe mwenyewe ukiwemo katika hiyo mijinga.
 
mm ni Mtanzania halisi, lakn Miafrika ya Tanzania ni mijinga sana, eti mtu anaomba ruhusa aende kwenye send off ya mtu asiye mfahamu, msiba wa ndugu ya shoga yake, n.k mbona wenzetu wa kenya hawafanyi hivyo?

Mjinga wa kwanza wewe na hapa sio kenya ni tz
 
NasDaz;

Taasisi zote ulizozitaja ni choka mbaya. Mtoa mada ana point
 
Last edited by a moderator:
NasDaz;

Well said mkuu, unanifanya nazid kujipenda km Mtz na nazid kuupenda utz. As u said cku hz kizungu ndo kinatambulisha usomi. Huu nao ni upuuzi tena usiopangiliwa kama anavyosema jenerali Ulimwengu

Mtu kasoma tena kamaliza shahada eti anakuja humu anasema watz hamuajiriki kwa 7bu hamjui kiingereza, upuuzi.

Umekaa na shahada yako na kampuni lako eti unawaajiri wakenya kisa wanajua kuzungumza kiingereza, huu nao ni upuuzi na utumwa.
 
Last edited by a moderator:
Nilikuwa kwenye ukurasa mmoja tunajadiliana hatua ya bunge la Tanzania kupitisha sera inayotia ugumu kwa waajiri kuajiri watu kutoka nje ya Tanzania. Katika majadiliano baadhi ya waajiri wakawa wanatoa misimamo yao, wengi walionesha kutokuwa na imani na wahitimu wa vyuo kutoka Tanzania. Hakika points wanazosimamia ni za ukweli, wahitimu wengi wanaakisi sura ya mazao duni vyuoni mwetu.


Tuache kuwabeza wasomi wetu kwa kuangalia vitu visivyo na mashiko.

1. Wasomi wa Tanzania wapo vizuri sana katika taaluma zao, tatizo kubwa ni lugha ya malkia.

2. Makampuni mengi hapa TZ wapo watz kibao ambao ndiyo vinara wa operations kubwa katika makampuni hayo. Mfano kampuni za SIMU hapa TZ zinategemea vichwa vya ki Tanzania kuliko hao mnaowahusudu.

3. Sijawahi kusoma ndani ya nchi ya Tanzania, lakini elimu ya Tanzania bado ni nzuri kuliko hata za hao mnaowahusudu.

4. Nimesoma na watu wa mataifa kibao, wengi wao walikuwa watupu, wana copy hadi assignment kutoka kwetu vijana wa Ki Tanzania. Sasa sioni faida ya hicho kiingereza chao kama darasani wao ni majanga

5. Ajira nyingi hapa nchini mmewapa hao majirani zetu ama kwa ulimbukeni ama kutokujua athari za mnachokifanya. Hivi juzi tumeshuhudia car parking ya hapa Tanzania iko managed na wafanyakazi wakenya, then bado mnajiona mna akili timamu.

6. Ma HR kibao kwenye makampuni hapa TZ ni wakenya na waganda na wao wamekuwa wakiwahifadhi na kuwaficha wahamiaji haramu au wale wanaofanya kazi bila work permit, bado mnajiona mmefanya uchaguzi sahihi.


Tuna kila sababu za kuwapongeza wabunge walioibua hii ISSUE kwani imeharibu na itaharibu ma deal kibao yaliyokuwa yakichezwa na hawa washenzi wanaojiita wafanyakazi wenye sifa.

Mwisho ndugu zangu wa Tanzania, tusibweteke. Kama unaweza kujifunza Driving muda wa jioni basi weka na muda mwingine ukasome lugha ya malkia pale British Council au kwingineko. Kujifunza ni sehemu ya maisha yetu.

Msiogope kwa kutojua lugha hiyo vizuri, waoneni wachina majority hawajui hiyo lugha lakini wapo mbali kimaendeleo kwasababu wanajituma na wanajifunza sikuzote.

Umasikini wetu upo mfukoni, SIYO KICHWANI.
 
Tatizo hawasomi na hawataki kujiendeleza.

Baada ya kupata hizo degree zao ndoo inakuwa mwisho wa kusoma. Unachotaka kufanya chochote hapa bongo kilishafanywa mahali kitu kama hicho GOOGLE first to see what is out there then study your situation and WORK.

Graduate wengi hawajui hata kuandika CV barua wamekalilishwa ipo inazunguka tunaoina.

Shida kubwa.
 
Kwa hiyo kigezo cha kuajiri mtu ni kiingereza? Huu utumwa mpaka lini watu wanaweza sema nafasi za kazi ni chache na nafasi waliyotangaza kapewa demu wako au mjomba wa bosi .mbona wasomi walivokuwa wachache mliwafuata chuo na hakuna mliyemwambia aandike barua..barua itabaki barua uwezo wa mtu utabaki uwezo wa mtu wangapi wanaandikiwa barua wakifika interview chali? Acheni kukitukuza kiingereza washika pembe ninyi mchina yuko wapi now na kichina chake? Au naye angesubiri hicho kiingereza ndio atoke?
 
Asilimia kubwa ya waliochangia huu uzi ni wapuuzi na elimu yao ni ndogo sana ndio maana wanashindwa ata kuona upuuzi wao. Eti wahitimu wa kibongo hawaajiriki, kivipi?

Yani msomi mzima unapima uwezo wa kazi wa mtu kwa kuangalia lugha? Hii nchi ndio maana inakuwa maskini.

Hivi daktari anaitaji kiingereza kutoa tiba? Hicho kiingereza ndio kinafanyia operation pale muhimbili watu kila leo? Au wale ni waganda na wakenya?

Hicho kiingereza ndio kinajenga madaraja uko mitaani? Yani engineer unampima ujuzi kwa kiingereza chake au? Na akibabaisha kiingereza basi hawezi kazi.

Watanzania mbona tumekuwa wajinga hivi!

Imefikia mpaka wafagizi kwenye maofisi jitu linaangalia kiingereza alafu ofisi ni ya waswahili watupu. Eti tungekuchukua ila kiingereza chako kibovu. Jingaz .
 
Hayo ni makosa ya wachache,lakini usiseme watanzania hatuajiriki.kwani hii nchi imejengwa na wageni au hao hao watanzania?sasa watanzania ndo wameshaamua kuwa lazima kuwe na sheria ya ajira itakayozingatia wazawa kwanza,mtu ambae hawezi aondoke Tanzania hatumtaki.

Hii sheria ya ajira kwa wageni ipo kwenye hatua gani mkuu, hii ni nzuri sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom