FaizaFoxy
Kitu kinachojitokeza hapo pia ni kukosa kujiamini pengine ndio tatizo kuu la vijana wasaka ajira. Mtu anaenda kwenye inerview akiwa tayari anaamini sifa stahili hanazo lkn anajaribu tu. Nataka kushare nanyi interviea tatu za kazi nilizohudhuria.
Ya kwanza ilikuwa kwenye shirika moja la kimataifa arusha. Kabla ya interview niliingia net na kureview vitu gani natakiwa nivijue kabla ya kwenda interview. Nikaandaa list na nikahakikisha nimevipitia vyote. Shirika lilikuwa linaongozwa na mghana mholanzi na mkenya. Kulikuwa na candidate kama kumi na nafasi ilikuwa moja. Basi tukaanza interview ya kuandika maswali manne kwa mtindo wa essay. Baada ya kupewa karatasi msimamizi akatoka nje.
Kama kawaida ''simbi'' zikaanza. swali la kwanza linauliza tuandike tunalifahmu vipi shirika pamoja na vission na mission yake. Kila mmoja anamuuliza mwenzake kama anajua. Mimi nlikuwa nimeshasoma kwenye mtandao na wakati tunasubiri kuanza interview nikawa naperuzi vipeperushi kadhaa vilivyokuwa mezani zaidi kuhusu hilo shirika.
Kuepuka usumbufu nikaanza kujibu maswali mengine. Hata hivyo kwenye oral nilishindwa kujibu swali moja na hivyo sikuipata ajira hii. Baada ya mwezi mmoja walinipigia wakaniambia nilikuwa second best hivyo wanataka waniajiri tena. Nikaenda tukazungumza tukakubaliana na nikapangiwa tarehe ya kusign mkataba na kuanza kazi. Lakini ksichoriziki hakiliki kwani kabla sijasaini mkataba shrika likasitisha kuajiri ghafla nadhani project ilisimamisha.
Ya pili ilikuwa iringa ambayo nilijiandaa vyema zaidi ya ya kwanza. Katika hii interview nilibabaika kujibu swali moja lililoulizwa na mkurugenzi mmoja mmarekani kwani lugha yake ilinipiga chenga lakini wengine ambao walikuwa ni wakenya wakarudia kuuliza nikaelewa nikajibu. Niliamini ntaipata hii kazi. Baada ya wiki mmoja mkurugenzi akanipigia simu kwa namba yake ya simu ya mkononi. Akaniuliza kama ni mimi nliyefanya interview nilipojibu akaniambia sawa ataanipigia baadaye kunifahamisha zaidi. Nikajua tayari.
Ajabu wiki ikapita. Nikaona bora nimpigie mimi akapokea na akaniambia nisubiri watanipigia baadaye nikajua nimeshachezewa faulu. Baadaye nilikuja kufahamu kuwa katika tuliofanya interview alikuwepo mtoto wa kurugenzi mstaafu wa hiyo kampuni ambaye alipewa hiyo kazi lkn kutokana na ulevi wa kupindukia mwaka mmoja baadaye kazi ile ikatangazwa. Classmate wangu aliyekuwa kwenye kampuni ile akaniambia mabosi walijuta baadaye kwa kutonipa ajira.
Ya tatu ilikuwa unilever. Hii ilikuwa ya siku mbili na ngumu. Waliomba zaidi ya watu 300 tkwa nafasi nne. Tukaitwa kwenye interview watu 30. siku ya kwanza tukatembezwa sehemu zote za kampuni mpaka jioni saa 11 tukapewa karatasi yenye maswali manne ya kiutendaji. Siku ya pili asubuhi tukaingizwa kwenye ukumbi tukapewa swali tufanye debate na tuje na ufumbuzi huku tumevaa lebo za majina yetu kila mchangiaji wananote jina. Baada ya hapo ikawa ni face to face. Watu wanne wanakuuliza mmoja baada ya mwingine unamjibu maswali yake. Na yalikuwa maswali ya kiujumla kutokana background ya mtu lakini magumu. Mfano namna ambavyo umewahi kusolve matatizo huko nyuma ya kikazi au kimasomo. Hata hivyo nilitishika na mazingira na nikaamua siwezifanya kazi hapo. Tuliambiwa mwaka ulopita wafanyakazi 11 walikufa kwa kupigwa na radi na mwaka huo tayari 8 walishafariki. kampuni ilifunga minara ya kutect radd ambapo dakika 15 kabla ya radd taarifa husambaza na watu hukimbilia ndani haraka. Wakati tunasubiri interview mara kweli watu wakaanza kukimbilia ndani tukaambiwa tusitoke mpaka radd ipige. Nikaona dah siyawezi maisha hayo nikaomba usafiri wa kunrirudisha mjini na jioni hiyohiyo nikaondoka iringa. Hata hivyo nilijifunza mengi na nikajua kwa mazingira kama hayo hakuna mbabaishaji anaweza kupata ajira na hata wakurugenzi wengi wa hapo walitoka kenya.
samahanini kwa gazeti