Huo ni ukweli usiopingika, katika mia labda mmoja.
Ukiwa na nia ya kuajiri Watanzania waliomaliza chuo, basi ujiandae tena kuwapa mafunzo ya kazi utayowaajiri kwa mwaka mmoja au miwili.
Kwanza lugha wanakuwa hohe hahe.
Mtu anakuja anakwambia nimesoma Business Management na ukitazama makaratasi ya uthibitisho aliyokuletea unakuta kasoma pia na IT ukimuuliza IT umesoma nini? anakwambia "excel", mpe hiyo "excel" mwambie haya chukuwa risiti hizi niwekee matumizi ya vitu hivi na unifanyie analysis vitu gani vinatugharimu sana. Utalia machozi, hajui hata aanzie wapi.
Kuna shirika lilinipa kazi ya ku assess wafanyakazi wapya waliomaliza "orientation" na walikuwa kwenye "probation" ili wajuwe nani wakumbakisha na nani wakumwachia akatafute kazi kwengine. Nililia na kucheka at the same time kwa kimbembe nilichokutana nacho.
Vijana walikuwa sita, wanawake wawili na wanaume 4.
Kila mmoja nilimpa barua ya mteja kaleta malalamiko, nikamwambia tunaomba muandike draft ya majibu mniletee, kuwa tunashughulikia malalamiko yake na tunaomba mkutano nae siku fulani ili tupange "way forward plan" na team yetu itakuwa na fulani na fulani na fulani na tungependa tuufanye mkutano nje ya mazingira ya kiofisi, tutagharamia lunch, watujulishe watakuja wangapi tunapendekeza tukutane hoteli fulani kuanzia saa tatu asubuhi mpaka wakati wa lunch.
Kazi ambayo walikuwa tayari wamefanyiwa orientation na wapo hapo kwa mwezi mmoja na nusu, haki ya Mungu nililia.
Wa kwanza kaja mwanamme, kama baada ya lisaa limoja, akanambia naomba kuuliza kidogo, nikamwambia karibu uliza tu. Nilishangaa! ananambia, mama naomba nisaidie, mimi hii kazi nnaihitaji sana kwetu kuna matatizo haya na haya na haya, kwa hiyo nisimwangushe na yupo tayari kugawana na mimi nusu kwa nusu mishahara yake ya miezi sita ya mwanzo.
Haki ya Mungu nililia machozi. Imagine a simple letter imemshinda kuandika na akaona aje kunihonga.
Wa Pili kaleta barua aliyoiandika, kaenda sijuwi kuchukuwa barua gani alijibiwa mteja akaikopi neno kwa neno akaniletea, haihusiani kabisa na nilichomwambia, yeye kaleta barua ya kuwaalika wateja kuhudhuria uzinduzi wa bidhaa mpya hoteli ya Serena. Nilibaki kucheka tu.
Watatu kaona isiwe tabu, kaja, kanambia Anti, mimi kazi basi, waambie mabosi nilishapata kazi kwengine.
Wanne na watano hawajarudi kabisa siku hiyo na wala hawajaleta nilichowaagiza, siku ya pili wamekuja kazini kama kawaida nikaita mmoja kwa boss wao kila mmoja kwa wakati wake wakanipa "identical Answer", kuwa "ala, kumbe barua ilikuwa inatakikana tukuletee jana" mimi sikujuwa na sijaanza kuitayarisha kwani nilikuwa na kazi zingine!
Wa sita, kajisikia vibaya kaomba kwenda kumuona daktari.
Hao ndiyo nguvu kazi ya Kitanzania. halafu tunauliza kwanini hatuendelei?