Wahitimu wa Tanzania hamuajiriki

Wahitimu wa Tanzania hamuajiriki

Kiukweli graduates wengi sana hamna kitu, kiingereza ndo kabisa hakipandi na pia licha ya yote hayo watu hawataki kuomba msaada mtu anaandika carrier badala ya career nigger are you serious..mimi wakati na graduate kuna mshikaji wangu flani nakiri yuko vizuri na pia updated anajua vitu vingi nikamuomba ebana eeh hivi cover letter unaandikaje akanipa sample yake yangu mimi ilikua ya kimagumashi vibaya basi kuunganisha na yangu Mungu mkubwa kijana nikatokelezea, nimefika ofisini kuna mshikaji alikua anapenda kuomba kazi anajua kutengeneza CV hatari nikamuomba anitengenezee yangu sasa hivi iko full vibaya mno, kama hauwezi kitu omba msaada usione aibu...kama haujui kitu omba ufundishwe....

Kwa hiyo computer engineer asiyeweza kutofautisha career na carier.. Ukimpa kompyuta mbovu atengenezi?
 
FaizaFoxy

Huu uongo wadanganye watoto wa juzi wasiofahamu.

Kwanza inabidi uelewe graduates dunia nzima hawamalizi vyuo wakiwa na uzoefu wa kazi ndio maana dunia yote kuna mifumo ya kuwa accommodate wanaotoka vyuoni huko makazini. Ndio maana wasiotaka graduates wanaweka kigezo cha uzoefu.

Pili hii hadithi uliyotunga haijavaa uusika ipo kama bongo muvi hehehehhehe eti watu sita wamemshindwa kujibu barua ya malalamiko na kuomba appointment kwa mteja mpaka wakazimia... Uongo mwingine mpaka msomaji anaona aibu. Duh utawaokota hao hao, msomi mwongo na mbabaishaji kama wewe utaishia kuwatishia watoto na kiingereza.
 
Last edited by a moderator:
NasDaz

Safi, kila kitu on point umeeleza.
 
Last edited by a moderator:
matumbo;

Kitu unachoshindwa kuelewa ni kuwa graduates wa Tanzania hata lugha hawaelewi hata kuandika barua simple tu wanashindwa, hatuongelei uzoefu wa kazi pekee.

Uzoefu wa kazi hakuna asiyejuwa kuwa kila mtu ni lazima uifanye hio kazi ili uizoee. Barua jee?

Uongo si katika sifa zangu labda hizo ni sifa zako ndiyo maana umekurupuka.
 
Last edited by a moderator:
Kitu unachoshindwa kuelewa ni kuwa graduates wa Tanzania hata lugha hawaelewi hata kuandika barua simple tu wanashindwa, hatuongelei uzoefu wa kazi pekee.

Uzoefu wa kazi hakuna asiyejuwa kuwa kila mtu ni lazima uifanye hio kazi ili uizoee. Barua jee?

Uongo si katika sifa zangu labda hizo ni sifa zako ndiyo maana umekurupuka.

Kwani ww boss unatafuta mtu wa kujua kuandika barua au unahitaji nn.
Kazi za masceretari hizo.
Kwako kigezo ni kuandika barua au engineer,mhasibu,mwalimu au daktari?

Binafsi sijui kuiandika barua ila nasimamia jengo lolote hata gorofa mia linaisha hapo vipi kaka .

Wachina,warusi,wavietnamu na wengine wengi hawajui english ila kwani hawana watalaamu na hawaendelei.
Usitumie english au kujua kuandika barua kumjaji mhasibu bana.


Wachina wana mainjinia na madaktari na wakiwa huku kwetu au shm yyte dunia wanapiga kazi.

Hiyo kozi nadhani itaongezwa chuoni unayotaka wawe nayo.

Kujenga barabara hakuhitaji ujue kuandika barua vizuri au english ila ujue idadi ya magari yanayopita hiyo barabara hiyo na yenye uzito gani.
So kama sina vigezo ivyo utaniacha kisa barua na english.

Pia ifike shm tujikubali kwa lugha yetu na sio kushobokea lugha za kuletwa na meli.
Mjerumani au mrusi hajisikii ufahari kuongea english na akiongea kwao anajificha.

Putin au ji ntao haoengei english bali ni kirusi na kichina wao ni wajinga?
Na wanaijua sana na nyingine zaidi
 
Lugha sio tija mie napinga.ndo yaleyale ya kukaririshana english na mzazi anajicfia kuwa mwanangu kasoma kwelikweli anaongea english kama anakunywa maji.

Uwe unatafuta wanaojua english wapo hata std 1 hawajaenda.standard measure au si unit ya usomi wetu ni english kweli.

Kuna mtu anajua terminology za maths au medicine tu na huyo utamuweka wapi.

Afu hiyo ni lugha kama lugha zingine za kibantu tu kisa kimetokea kwa nguruwe au manguruwe ndo mnakiona cha maana ila kilichotokea kwa masokwe hakina mana.
Namnukuu nyerere,kuna jambo la kipuuzi mtu akisema kiingereza anaknekana la mana
 
iunajua ukiwa na macho ya makengeza ukiangalia unaona watu wawili lakini kumbe ni mtu mmoja, sasa huyu mwenye makengeza asipojitambua kuwa macho yake ndio yenye tatizo anaweza kumlaumu mtu mwingine kama alidhani pale kulistahili kuwepo mtu mmoja.

lipo tatizo la watu wasio na sifa za kuwa viongozi lakini ambao ujanja umewafanya kuwa viongozi kutokujua the right aproach ya kufanya "recruitment" alafu wanaposhindwa kupata wanachokitafuta wanalaumu wengine.

mwajiri yeyote anayeweza kutoa kauli hiyo kwa shughuli zinazofanyika hapa tanzania kwa sasa kimsingi yeye ndiye mwenye matatizo.

kiukweli ukitafuta wataalamu wa nyukilia, wana sayansi za kwenda mwezini au nje ya dunia hao kwa tanzania huwezi kuwapata na mwajiri mwenye akili hawezi kulalamika.

lakini lipo tatizo la wahuni ambao wamepiga porojo tu wakaonekana wanafaa kumbe wababaishaji watupu wanapopewa ofisi hawakosi visingizio.

akiona mrembo anamuahidi kazi na hapo atafanya awezavyo kutengeneza nafasi ya kazi ama kwa kuweka nafasi ambayo haipo au kumfukuza mtu.

mjinga ndiye anaweza kuwa na kazi akaita mtu mmoja amletee maombi ya kazi na kama huyo atakosea aanze kulalamika.

hivi nini maana ya interview? au usaili?

pale kazi inapotangazwa wanajitokeza waombaji wengi, wapo wenye sifa, wapo wahuni wanaofoji sifa, wapo wasio na sifa lakini wanajaribu bahati yao.

sasa ni wajibu wa mwajiri kuwachambua hawa kupata mwenye sifa.

sasa wewe unaenda unamchukua mtu anayejiuza anakudanganya amesoma chuo fulani na unaamua kumuajiri lakini yale uliyomtuma afanye anaposhindwa bado unamtetea yeye na kuona shule alikosoma ndiko tatizo???? huo ni ujinga!

yeyote anayetafuta wafanyakazi kwa kuangalia rushwa ama ya fedha au ya starehe, yeyote anatafuta wafanyakzi kwa kutaka kuajiri watu anaowajua au kuwasaidia ndugu zake atavuna matokeo ya mfumo mbovu anaoutumia katika kutafuta wafanyakazi na matokeo hayo atabeba dhamana yake yeye mwenye kuwa mpumbavu na sio kubebesha wengine lawama.

hakuna kampuni inayotengeneza faida kwa kuangalia makampuni makubwa iliyowahi kutoa malalmiko kama haya, sasa huyu ni nani? hawa wanaoajiriwa na wengine wamesomea wapi?

lipo tatizo la sometimes mtu anapopata nafasi yeye anadhani anajua kila kitu hivyo kama ni interview ataendesha yeye. na ujinga huu umewapotosha wengi kwa maana kila mtu anapekua vitabu na makablasha kutafuta swali na jibu.

elimu ya mtu inachangiwa na mambo mengi sana lakini kila mwajiri ajitambue yeye kwanza badala ya kukimbilia kubebesha wengine lawama.

Nilikuwa kwenye ukurasa mmoja tunajadiliana hatua ya bunge la Tanzania kupitisha sera inayotia ugumu kwa waajiri kuajiri watu kutoka nje ya Tanzania. Katika majadiliano baadhi ya waajiri wakawa wanatoa misimamo yao, wengi walionesha kutokuwa na imani na wahitimu wa vyuo kutoka Tanzania. Hakika points wanazosimamia ni za ukweli, wahitimu wengi wanaakisi sura ya mazao duni vyuoni mwetu.


======================
======================
 
ego;

Na hawa watanzania walioko nchini za nje na wanapiga kazi inakuwaje sasa.
Kuna lectures,engineers,daktari walioko mpaka ulaya na wamepatia hapahapa elimu.

Hapa mie naona kale kadhana ka kutothamini cha kwako na kuona cha jirani ndo mana sana.

Muite mtu wa kila taifa hao unaowaamini zen uwape watatue tatizo fulani wapime kwa utendaji wake ila sio kwa porojo.

Wape mgonjwa wamtibu afu wa kitanzania ashindwe.

Kigeni kinaonekana cha mana sana.
Hata demu ukimtokea huku unamwambia ww sio mtanzania anakuja kwako mia spidi ndogo.

Pia uelewe chako unakijua mpaka na udhaifu unaujua ila cha mbali haujui chochote
 
Last edited by a moderator:
hawa wanaokuja na stori za kudai watu wanaosomea tanzania hawaajiriki ni wababaishaji.

nina rafiki yangu alikuwa ameajiriwa sehemu fulani yeye akiwa kwenye kitengo cha utaalamu na kampuni hiyo kulikuwa na mzungu yeye yuko kitengo cha fedha.

sasa wakaamua kutoka kampuni iliyokuwa imewaajiri na kuanzisha kampuni ya kwao lakini huyu rafiki yangu anasema yeye ndiye mtaalamu na mzungu yeye ni mtu wa fedha. walipewa kazi na kampuni fulani lakini anasema watanzania hawa waliokuwa wakizungumza nao walikuwa wakimsikiliza mzungu tu na mambo ya kitaalamu wakitamani mzungu ndio aseme.

leo hii watanzania walio wengi wakiona mzungu au rangi nyeupe wanajenga dhana kichwani kuwa anajua na wakilinganisha na mwafrika wanaona hajui.

tunahitaji kubadilika.

mimi nimeona wazungu wengi tu wababaishaji, wachina wababishaji, ingawa na wabongo wababaishaji wapo lakini ubabaishaji ni kwa mataifa yote.

ila sisi tumejenga dhana kichwani ukiona rangi unajua huyu anajua, ukisikia huyu anatoka taifa fulani basi unajua anajua au hajui.

haya yanajengwa na watu wasiojua kwa maana anayejua anasikiliza mtu alafu anamhukumu kutokana na what mtu anjua na sio kwa dhana fulani.
keisangora
 
Last edited by a moderator:
Binafsi sijui kuiandika barua ila nasimamia jengo lolote hata gorofa mia linaisha hapo vipi kaka .

Wachina,warusi,wavietnamu na wengine wengi hawajui english ila kwani hawana watalaamu na hawaendelei.
Usitumie english au kujua kuandika barua kumjaji mhasibu bana.

Ndiyo maana majengo hayana ubora. Yaanaanguka hovyo kwa watu kama nyinyi.

Kuongea English ni kigezo kimojawapo cha kujipatia kazi hapa kwetu, kwenye kazi nyingi tu. Hadi sheria zetu na katiba tuliyonayo sasa ilitungwa Kingereza.

Huyo Engineer unaesema kama alisoma Tanzania basi lazima ajuwe Kingereza, ndiyo somo la kufundishiwa hiyo "engineering" na angesoma Urusi basi kwanza ni lazima angefundishwa Kirusi.

Hapa kwetu piga ua huwezi kukiepuka Kingereza kwa sasa, itachukuwa miaka mingi sana.
 
Ndiyo maana majengo hayana ubora. Yaanaanguka hovyo kwa watu kama nyinyi.

Kuongea English ni kigezo kimojawapo cha kujipatia kazi hapa kwetu, kwenye kazi nyingi tu. Hadi sheria zetu na katiba tuliyonayo sasa ilitungwa Kingereza.

Kwa hiyo jengo likijengwa na injinia hasiyejua kiingereza linakuwa sio bora muda wowote litadondoka ?

Ila likijengwa na injinia anaechapa kiingereza kizuri linakuwa ni bora sana?

Teh teh teh teh awa ndio wasomi wetu awa.
 
may alikua yupo internet cafe alikuwa amelipia mda mchache na yeye sio mzuri sana katika matumizi ya computer, so akahofu akiandika na maelezo mda utaisha hajamaliza kutuma, Akaamia kutuma tu. Am sorry
kama sio mzuri katika matumizi ya computer hiyo kazi anayoomba ataifanya vipi vila kujua kutumia computer
 
Me naona hilo somo lisomwe semester ya mwisho tu...kwani ndio anajiandaa kuifanyia applications kwenye maisha ya kutafuta kazi
Yaani unataka university wafundishe watu kuandika barua?mambo mengine hayahitaji kufundishwa una google tu
 
FaizaFoxy;

Siku hizi watoto hawasomi dada,anasubiri boom anahonga lote kwa ma lecturer anasonga mbele.sikutegemea fresh graduate awe na guts za kukuhonga wewe assessor wake,lakini kwa kua ameshazoea kuhonga tokea chuoni,ndio mana akathubutu kujaribu kukuhonga
 
Last edited by a moderator:
Yaani unataka university wafundishe watu kuandika barua?mambo mengine hayahitaji kufundishwa una google tu

Wachangiaji walivosema ni kuwa wanafundishwa kuandika barua mwaka wa kwanza katika somo la DS ..so kutokana na sababu kwamba huwa wanasahau...ndio maana nika suggest hilo somo lifundishwe last year wakiwa wanajiandaa kuingia katika kazi ya kutafuta Kazi
 
Kwa hiyo jengo likijengwa na injinia hasiyejua kiingereza linakuwa sio bora muda wowote litadondoka ?

Ila likijengwa na injinia anaechapa kiingereza kizuri linakuwa ni bora sana?

Teh teh teh teh awa ndio wasomi wetu awa.

Huyo asiyejuwa Kiingereza atakuwa engineer ambae hajasoma Tanzania.
 
Semeni nini kifanyike sasa,sio mnaponda tu as if nyie sio watanzania.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom