Wahitimu wa Tanzania hamuajiriki

Wahitimu wa Tanzania hamuajiriki

Mkuu nakuunga mkono kwa 101%. Shule za kata zimechangia sana kuharibu elimu yetu.
 
FaizaFoxy
Engineering language ni tofauti na hayo unayotaka injinia ayajue.

Anajua terms za mathematics na physics.

Hizo blah blah zako sijui slang au fluency hajui.

Anajua injini ilivyo au inavyofanya kazi.au jinsi ya kuchanganya zege,kutoa michoro ya nondo za gorofani ila hayo madubwasha hajui.

Engineers talk through drawings kaka.

Pia kuelewa kitu sio lazima uelewe hiyo lugha.hata mwafrica anajifunza kiarabu cha kujifunzia kiislamu ila kiarabu hajui,anajua terms za dini na kama unataka anayejua kiarabu nenda uarabuni
 
Last edited by a moderator:
Engineering language ni tofauti na hayo unayotaka injinia ayajue.

Anajua terms za mathematics na physics.

Hizo blah blah zako sijui slang au fluency hajui.

Anajua injini ilivyo au inavyofanya kazi.au jinsi ya kuchanganya zege,kutoa michoro ya nondo za gorofani ila hayo madubwasha hajui.

Engineers talk through drawings kaka.

Pia kuelewa kitu sio lazima uelewe hiyo lugha.hata mwafrica anajifunza kiarabu cha kujifunzia kiislamu ila kiarabu hajui,anajua terms za dini na kama unataka anayejua kiarabu nenda uarabuni

Wacha porojo, jibu swali. Engineering Tanzania inafundishwa Kiswahili?

Ukiona engineer kasomea Tanzania na hajuwi Kingereza, ujuwe hilo ni bomu.
 
Tujifundisheni Lugha jamani. Ni muhimu sana.
Tuwe na malengo sio nchini tu bali hata nje ya nchi.
Lugha ya kiingereza ni muhimu sana. Muda ambao unaopoteza kukaa tu nyumbani bila ajira, tumia fursa hiyo kujiweka vizuri kwenye kuongea. Kuwa tu na elimu ya shahada haitoshi, ila kuna mengi zaidi kazini kama vile mawasiliano, umaridadi, uwezo wa kufikiri na kutatua jambo, busara, hekima, ukarimu, huruma, upendo, uaminifu, uadilifu n.k. Vitu ambavo ni muhimu na hauvipati shuleni.
 
Tujifundisheni Lugha jamani. Ni muhimu sana.
Tuwe na malengo sio nchini tu bali hata nje ya nchi.
Lugha ya kiingereza ni muhimu sana. Muda ambao unaopoteza kukaa tu nyumbani bila ajira, tumia fursa hiyo kujiweka vizuri kwenye kuongea. Kuwa tu na elimu ya shahada haitoshi, ila kuna mengi zaidi kazini kama vile mawasiliano, umaridadi, uwezo wa kufikiri na kutatua jambo, busara, hekima, ukarimu, huruma, upendo, uaminifu, uadilifu n.k. Vitu ambavo ni muhimu na hauvipati shuleni.

Kwani wachina wanaokuja mnawapa tenda wanajua english.

Usikariri English sio ujuzi ni lugha kama lugha zingine.

Hakuna madaktari wa kichina au wa kihindi wanatibu watu na wanapona.

Kuna jambo la kipumbavu ila ukisema kiingereza linaonekana la mana sana.

Pia nyie ndo mnaokimbiza wanao medium mnadhani ndo kuna elimu bora kisa anafundishwa english kumbe anakalilishwa tu akija kwako akiongea english unajiona ufahari kuwa umesomesha sana kisa kutema english.

Mie nimeenda kidato cha kwanza hao watoto tunawaacha mbali sana mpaka hiyo english yenyewe anazidiwa na kayumba sema yy anatuzidi kuongea ktk debate.

Pia chuoni wanafunzi wa kiganda au watanzania waliosomea kule uganda na wamedisco na huku wanajua english.

Tofautisha utendaji na uongeaji.

Kuna wazee hawajaenda darasani kutumia karatasi na kalamu ila wanatengeneza mashine zilizowashinda wasomi wa darasani.

Na huyu mzee utamuomba vyeti au utamuuliza kama anajua english.

Mlinzi anaulizwa na boss wake kama anajua english naye kamuuliza boss wake kama hao wezi wanaokuja kuiba wanaongea english.
 
Elimu si shahada wala cheti,ni uwezo wa kuchambua,kufikiri kwa njia pana,kuwa mbunifu,kuuliza maswali,kuwa jasiri,kujiamini,kujua jinsi ya kujifunza zaidi,kupanga mambo vizuri,kupima kuweza kutatua matatizo ambayo hujawahi kukabiliana nayo
 
tpaul
Elimu si shahada wala cheti,ni uwezo wa kuchambua,kufikiri kwa njia pana,kuwa mbunifu,kuuliza maswali,kuwa jasiri,kujiamini,kujua jinsi ya kujifunza zaidi,kupanga mambo vizuri,kupima kuweza kutatua matatizo ambayo hujawahi kukabiliana nayo

Hapo hawajasema kuwa elimu ni kipimo cha kuongea english
 
Last edited by a moderator:
kuna mambo ambayo huyazungumzi nyuma ya majengo kuanguka.

leo hii tanzania tumejenga utamaduni wa kutotumia wataalamu bali ubabaishaji na matokeo yake tunabebesha dhamana wataalamu.

watu wanatafuta cheap labour, mtu anatafuta mtu tu ilimradi anajua kupanga tofali basi anamtaka amudesignie nyumba na kusimamia ujenzi sasa unategemea nini?

mtu anaona kumuajiri engineer na architect ni gharama hivyo anatumia mafundi ambao wao wanatumia uzoefu wa kuangalia kitu fulani aliona hivi lakini hawezi kutofautisha kitaalamu kwa maana ya kutafuta size, umbo, wa kitu kwa kutumia utaalamu na matokeo ndio hayo. hili linahusisha taasisi za serikali pia kwa maana zinatakiwa kusimamia kila sekita kuhakikisha kila mwenye kujenga anatumia wataalamu na lengo ni kuepuka majanga kama haya au kutumia gharama kubwa katika ujenzi.

inahusisha watoa kazi wote kutambua risk ya kutotumia wataalamu, na inawahusu wataalamu wenyewe kwa kutokufanya vitu vya kuwapotezea sifa za kitaalamu au kupata adhabu zaidi.

lakini yote yaanazia pale mifumo ya usimamiaji inapokuwa inafanya kazi ndipo nidhamu katika sekita inakuwepo kwa kila mdau kuangalia majukumu yake.

na hapa sio swala la elimu ya watanzania bali mimi naweza kusema zaidi ni corruption.

Ndiyo maana majengo hayana ubora. Yaanaanguka hovyo kwa watu kama nyinyi.

Kuongea English ni kigezo kimojawapo cha kujipatia kazi hapa kwetu, kwenye kazi nyingi tu. Hadi sheria zetu na katiba tuliyonayo sasa ilitungwa Kingereza.

Huyo Engineer unaesema kama alisoma Tanzania basi lazima ajuwe Kingereza, ndiyo somo la kufundishiwa hiyo "engineering" na angesoma Urusi basi kwanza ni lazima angefundishwa Kirusi.

Hapa kwetu piga ua huwezi kukiepuka Kingereza kwa sasa, itachukuwa miaka mingi sana.
 
Mapungufu ya kujieleza(Communication Skills) ni kweli watanzania wengi tunayo! Hata hivyo hiyo ni Cover of the book...and not the content of the book!!!

Nimefanya kazi na wakennya, waganda za wasauzi. Katika swala la communication skills na kujipendekeza kwa maboss ili ku-gain quick and cheap acceptance wako vizuri sana...hasa wakenya!

Ila katika utendaji halisi wa kazi husika(content of the book) watanzania wako juu mno. Mtanzania anaweza kufanya kazi nzuri mno but result ya ile kazi akai-communicate improperly kwa Boss wake na akaishia kupata dharau ambayo hakustahili! Vyuo vya TANZANIA vinatakiwa kufanya jitihada kubwa sana kwenye Communication Skills kwa wahitimu wa vyuo vyetu....la sivyo tutapewa uboya tusiostahili kabisa. Umombo duni unachangia sana katika hili

Suluhisho la kwanza ni Watanzania kuwa na tabia ya KUJIAMINI (SELF CONFIDENCE) kwamba wanaweza and should demonstrate that! Hili ni muhimu sana kwasababu CARRIER PATH za watanzania wengi zipo chini coz hawajiamni hata kama utendaji wao kivitendo ni mzuri.

Suhisho la pili ni kuboresha Communication Skills. Mfano mzuri ni huo aliotoa mtoa mada wa Watanzania kukurupuka wakati wa kuandaa nyaraka za kuombea kazi(CV and other related documents)! Kuomba kazi sio lele mama. Kumbuka kuwa ushindani wa kuomba kazi ni mgumu kuliko vita coz unayeshindana naye kwenye kazi hiyo humjui kabisa iwe kwa personality au kwa sifa! Ni kwa sababu hii unatakiwa kutuliza kichwa vizuri wakati wa kuandaa CV yako na nyaraka nyingine muhimu! Vilevile, ukiwa umeshapa kazi tayari hakikisha unatumia APPROPRIATE COMMUNICATION SKILLS and MEDIUM kama emails, Phone-calls, conversations ili kufikisha taarifa kwa usahihi na kwa wakati muafaka. Pangilia point zako kwa ACCURACY, RELEVANCY, and degree of importance kulingana na subject matter kabla ya kuzi-communicate kwa destination point husika. Ufanyaji kazi wako hata uwe mzuri kiasi gani if not accompanied by appropriate communication skills unaweza kusababisha uonekani hujui kazi.

Suluhisho la tatu ni kufanya jitahidini kujua KIMOMBO na lugha zingine za kigeni kwa sababu sekta binafsi Tanzania inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na wawekezaji wa kigeni ambao hawajui kiswahili! Oral communication skills challenges ambazo watanzania wengi wanazo zinatokana na ufahamu hafifu wa lugha za kigeni hususani Kiingereza.

Suluhisho la nne ni kwamba unaposhinda interview ya kazi fulani ukienda kazini jiamini na fanya kazi kwa bidii! Hakikisha unakuwa na POSITIVE ATTITUDE always. Hata kama kitu fulani ni kigumu kwako...amini kwamba unakiweza na hakika utakiweza if you employ necessary skills, competencies and efforts!


Be advised accordingly!
Nilikuwa kwenye ukurasa mmoja tunajadiliana hatua ya bunge la Tanzania kupitisha sera inayotia ugumu kwa waajiri kuajiri watu kutoka nje ya Tanzania. Katika majadiliano baadhi ya waajiri wakawa wanatoa misimamo yao, wengi walionesha kutokuwa na imani na wahitimu wa vyuo kutoka Tanzania. Hakika points wanazosimamia ni za ukweli, wahitimu wengi wanaakisi sura ya mazao duni vyuoni mwetu.


======================
======================
 
ego;

Aliyeelimika hawezi kuwa "corrupt". Ukiona mtu anakuwa "corrupt" mpaka anafikia kutokujali maisha ya wengine ujuwe huyo hajaelimika na shule haijamsaidia kitu bali imemjaza ujinga tu.
 
Last edited by a moderator:
Tuache kujitetea communication skills ni tatizo kubwa,wala vyuo tusivitupie lawama mchango wao ni mdogo sehemu kubwa ya mafanikio shuleni ni juhudi za mtu binafsi.Kama wewe unajiamini uko vizuri communication skill haya sema ni chuo kilikusaidia au juhudi zako binafsi?
Mimi niko vizuri communication skills kwa juhudi zangu binafsi. Wewe je?

Tujifunze kuwa wadadisi hapa kuna mtu amenadika wingi wa njia za mawasiliano ni media na si medium,ni kama stadium ni uwanja ukiwa mmjo,viwanja nistadia.Kama bado hujanielewa fuatilia angenda na agendum( agendas inatoka wapi?).

Proof reading ni tatizo kubwa pia,nilishawahi andika siku za nyuma sasa huwa hatujui kushukuru,muda si mrefu Mungu akipenda nitakuwa nasaidia katika mambo haya however there is a price tag.

Mwingine anasema Engineer haihitaji kujua lugha yeye anacommunicate kwa drawings,je ataweza kumwelezea mteja wake hizo drawings mteja ambaye hajui hiyo michoro inamanisha nini?Je engineer hawezi takiwa kufanya presentation ya project yake?Communication skills ni muhimu kwa kila mtu haijarishi umesomea mambo gani.


NB:"When you stop learning you stop growing"
 
keisangora;

Mkuu wewe ndo umekariri. Hao wachina unaowaongelea wana Technologia yao wala hawahitaji kizungu.

Wakipewa tenda bongo hawatumii kiingereza wanatumia elimu yao ndo maana wanaajiriwa. Sasa bongo technologia hauna na lugha pia haujui?

Angalia wa Kenya wanavoajiriwa nchi za nje wengine hawajasoma lakini kutokana na lugha wanaweza kujipatia rizki nje ya nchi yao. Lakini bongo uvivu wetu wa kujituma na lugha ya kiingereza hata ukifanya interview ya nje mtu anakua na wasi wasi na elimu yako. Unajivunia na nini? Na cheti chako hicho cha chuo cha bongo chuo hata hakitambuliki kimataifa.

Hata bongo ukipewa ajira bado kuandika barua haujui. Kunyoosha sentensi unamtumia meneja reporti kizungu kimekaa kiunaga ubaga. Haueleweki umeandika nini, broken tupu. Usitake kubisha kuna vitu muhimu zaidi ya kua tu na fani ya darasani, sasa mbona bado watu wapo mtaani?

Mtu anatuma CV yake unataka kutapika, Ukimuita kwenye interview unaona anakupotezea mda, unamuuliza jielezee, kitu cha dakika moja anatumia dakika tano na bado hajaeleweka vizuri. Ukikosa ajira unasema walishachagua watu. Sasa wewe kwa akili yako akija mtu ana degree yake plus anajua kiingereza na mwingine ana degree yake pia hajui kiingereza utamuajiri nan?

Tanzania ni aibu, wakenya na wauganda wanatushinda. Waacheni waendelee kuajiriwa na sisi tubaki na ujinga wetu wa kusema degree ninayo inatosha. Kwa dunia ya sasa hivi unatakiwa kua competent, ikiwezekana hata lugha tatu siio english tu, ukijua na kifaransa bado ni added advantage. Baki hivo hivo na akili yako hiyo sawa eeeee.
 
Last edited by a moderator:
Niseme lakini ni ukweli, na tuuweke wazi.

kwa miezi michache nilibahatika kufika kwenye viwanda, mahoteli ya kitalii na ofisi nyingi zisizo za kiserekali.

Nilichoona

1. Walinzi wa chini wote ni watz wenzangu. Wasimamazi wao ni wahindi, wakenya, wachina na hata wazungu (kk) na kwa sehemu kubwa hata hawa wa chini kwenye mahoteli ya nyota 3 kuja juu si watanzania na zile sehemu ambazo lugha ya malkia inakipaumbele. .
2. Sehemu ya mapokezi ni mchanganyiko, lakini kadiri hadhi inavyopanda ndio utakuta watoto wa vibosile na watu wa nje.
3. Viongozi wote wakuu kama HR, Production, wahandisi wakuu hapa ni funga kazi, hakuna mtz ni mataifa mchanganyiko.
4. Nafasi ya Mhasibu mkuu hapa kuna wahindi karibu kwa sehemu zote nilizoona, hata zile ambazo HR au prod maneja ni mtz. Hawa wahindi sio hawa koko wa hapa, wameletwa.
Niliweza kuuliza sababu ni nini hasa? Na nilipewa majibu haya.
1. watz ni wezi - niliambiwa kuwa watanzania wakifika kazini kitu anafikiri ni kuiba tu, hata vitendea kazi yake anaiba. Alifananisha na askari wa barabarani akiwa anakagua gari je, anataka kusaidia au anafanya mahesabu ya ngapi avute kutoka kwako.
2. watz ni wavivu - kiutendaji watanzania wanasikitisha. They are non delivering.
3.Wanamatamanio yasiyowezekana - na hasa ukilinganisha na utendaji na wizi wao mf- kila mtanzania anayeajiriwa leo, baada ya miezi miwili anataka gari na matanuzi ya kila aina, na utakuta wakielezana waliofanikiwa mf mapolisi, wauza madawa, walarushwa na wezi wa mali ya uma. Wana role model zao
4. Uwezo wa kiutendaji na weledi wa watz ni mdogo kweli kweli, na hii uangalie kwa mapana na kina kwa namna walivyosoma, walivyofaulu mitihani, kazi za mafunzo (field work) walizofanya nk.
5 watz hawaaminiki kabisa = kwa maneno na matendo yao
6. watz hawaweki maslahi ya tasisi zao na wanamuono mfupi sana wa kimalengo
Baada ya hapo wote waliozungumza nami walihitimisha kuwakampuni zote zinazofanya vizuri zimechukua mtamo huu, na zinazo/zilizo feli ni kwa kupenda watz na wala siyo maslahi ya kiuchumi. Mbaya zaidiwanasema hata watanzania, wakubwa kwa wadogo hawatafika mbali kibiashara kwa sababu unayemwajiri anasifa hizo hapo juu, pili vyombo vinavyohusika na kutoa vibali na kodi vinakukamua mpaka mtaji, tatu vyombo vya kiusalama na kisheria vitakuandama ili uonekane mhalifu kila siku ili wavute chochote na ole wako uwe na kausafiri hata kama ni toyo, kila ukienda hatua 100 wanataka.
Kama huu ni uwongo angalia na tafakari utendaji wa bunge, ofisi yako ya kijiji, kata, shule, polisi, halimashauri, mahakama hata tasisi za kiaraia au hata kwenye makanisa na misikiti au sehemu za kuabudia kama hali siyo hiyo.

Ama kweli hii ni BIG RESULT -tumeua elimu kwa zaidi ya miaka 25 sasa na tutalipa hii kwa miaka 100 ijayo kama tutajirekebisha sasa
 
nani kakudanganya?

sheria na kanuni ambazo zinaambatana na adhabu ndizo pekee zinaondoa corruption katika jamii. kama ukimkabidhi duka mtu bila kumsimamia akaligeuza duka hilo lake yeye kwa maana anatumia mtaji wako kujitengenezea faida yeye sijui nani anakosa elimu hapa mwenye duka mzembe/ mvivu au mfanyakazi mwizi au mjanja.

corruption kwa kifupi ni ile dhana ya mtu kutumia ofisi ya umma lakini akitumikia vitu vingine na sio umma. umepewa nafasi ya kugawa tenda unaweka 10% ya kwako, unapewa kumsimamia mtu anakupa fedha ya kuweka mfukoni mwako na unaacha kufuatilia majukumu ya jamii.

kutambua ugonjwa ni hatua ya kwanza na ya muhimu katika kutibu ugonjwa wako.

siku mamlaka husika zikianza kutoa adhabu kali kwa wanaokiuka taratibu za ujenzi basi wajenzi watafuata taratibu.

siku mamlaka husika zikiwa serious katika kuadhibu walioko kila mtendaji anayekosea basi watendaji wote watakuwa makini.

lakini kama aliyepewa rungu la kuadhibu analitumia kutafuta ulaji kwa kuwatisha hata wasio na makosa ilimradi watoe chochote na aliye na kosa akiwa ametoa chochote anapeta.

kama watoa kazi hawaangalii utaalamu bali wanabeba ajenda zao kama kuangalia rushwa.

hapa tatizo sio elimu bali mifumo holela kwani mjinga anayeweza kujifanya anajua taratibu anaishia kuadhibiwa hata yeye mifumo itamtoa huko kwenye taratibu na kuanza kufuata njia za kupata pesa.



Aliyeelimika hawezi kuwa "corrupt". Ukiona mtu anakuwa "corrupt" mpaka anafikia kutokujali maisha ya wengine ujuwe huyo hajaelimika na shule haijamsaidia kitu bali imemjaza ujinga tu.
 
ego;

Zunguka na maneno ya kila aina mwisho wa siku, kumbuka hili:

Aliyeelimika hawezi kuwa "corrupt". Ukiona mtu anakuwa "corrupt" mpaka anafikia kutokujali maisha ya wengine ujuwe huyo hajaelimika na shule haijamsaidia kitu bali imemjaza ujinga tu.
 
Last edited by a moderator:
hapa tunatofautiana kimtizamo kwani kwako wewe unadhani rushwa, wizi, upendeleo vikizidi katika jamii basi mitaala ya elimu irekebishwe.

swala la elimu linakuja baada ya mifumo ya sheria na usiamiaji wake linapokuwa linafanya kazi kwa maana mwenye dhamana kutambua risk anazoweza kuwa anazichukua kwa kujihusisha na corruption, mwananchi kutambua kuwa serikali inawajibu wa kumtumikia kwa utaratibu waliokubaliana kitaifa na yeyote anayeleta ajenda zake kakiuka na anastahili kutolewa taarifa.

lakini mfano mimi ni kama ni daktari niliyeajiriwa katika hospitali ya umma, yanaletwa madawa ya kugawa kwa wananchi bure au kwa bei nafuu, nayahamishia katika zahanati yangu au duka langu la dawa na wananchi wakija kutibiwa katika hospitali ya umma ni dawa hakuna na wanaenda kununua dukani kwangu. ninatengeneza supa profit kwa maana sinunui bali nachukua katika hospitali ya umma.

hivi mimi nastahili kupelekwa kusoma ili nielimike niache au nishitakiwe?

kutokufanya haya ninawaza nini? ama elimu niliyoisoma popote au kuogopa sheria nisiadhibiwe?

ni kipi ambacho kikikosekana ndio nafanya haya? je maarifa au wa kunisimamia?

lakini mimi nadhani haya yakishamiri kunakuwa na tatizo katika mfumo wa sheria na usimamiaji wake na hapa ndio pa kutafutia ufumbuzi.

tunaweza kukubaliana katika kutokubaliana kwa maana hakuna alimshwawishi mwenzake kuchukua idea ya mwingine basi wewe unabaki kuamini hivyo na mimi kuamini ninavyoamini, kama zingekuwa proposals kwa customers basi customers wenyewe wangechagua which option wanaiprefer.

Zunguka na maneno ya kila aina mwisho wa siku, kumbuka hili:

Aliyeelimika hawezi kuwa "corrupt". Ukiona mtu anakuwa "corrupt" mpaka anafikia kutokujali maisha ya wengine ujuwe huyo hajaelimika na shule haijamsaidia kitu bali imemjaza ujinga tu.
 
ego;

Aliyeelimika hawezi kuwa "corrupt".

Hata awe na shahada za juu 100 anakuwa bado ni mjinga tu.


"power corrupts, and absolute power corrupts absolutely".
 
Last edited by a moderator:
Huo ni ukweli usiopingika, katika mia labda mmoja.

Ukiwa na nia ya kuajiri Watanzania waliomaliza chuo, basi ujiandae tena kuwapa mafunzo ya kazi utayowaajiri kwa mwaka mmoja au miwili.

Kwanza lugha wanakuwa hohe hahe.

Mtu anakuja anakwambia nimesoma Business Management na ukitazama makaratasi ya uthibitisho aliyokuletea unakuta kasoma pia na IT ukimuuliza IT umesoma nini? anakwambia "excel", mpe hiyo "excel" mwambie haya chukuwa risiti hizi niwekee matumizi ya vitu hivi na unifanyie analysis vitu gani vinatugharimu sana. Utalia machozi, hajui hata aanzie wapi.

Kuna shirika lilinipa kazi ya ku assess wafanyakazi wapya waliomaliza "orientation" na walikuwa kwenye "probation" ili wajuwe nani wakumbakisha na nani wakumwachia akatafute kazi kwengine. Nililia na kucheka at the same time kwa kimbembe nilichokutana nacho.

Vijana walikuwa sita, wanawake wawili na wanaume 4.

Kila mmoja nilimpa barua ya mteja kaleta malalamiko, nikamwambia tunaomba muandike draft ya majibu mniletee, kuwa tunashughulikia malalamiko yake na tunaomba mkutano nae siku fulani ili tupange "way forward plan" na team yetu itakuwa na fulani na fulani na fulani na tungependa tuufanye mkutano nje ya mazingira ya kiofisi, tutagharamia lunch, watujulishe watakuja wangapi tunapendekeza tukutane hoteli fulani kuanzia saa tatu asubuhi mpaka wakati wa lunch.

Kazi ambayo walikuwa tayari wamefanyiwa orientation na wapo hapo kwa mwezi mmoja na nusu, haki ya Mungu nililia.

Wa kwanza kaja mwanamme, kama baada ya lisaa limoja, akanambia naomba kuuliza kidogo, nikamwambia karibu uliza tu. Nilishangaa! ananambia, mama naomba nisaidie, mimi hii kazi nnaihitaji sana kwetu kuna matatizo haya na haya na haya, kwa hiyo nisimwangushe na yupo tayari kugawana na mimi nusu kwa nusu mishahara yake ya miezi sita ya mwanzo.

Haki ya Mungu nililia machozi. Imagine a simple letter imemshinda kuandika na akaona aje kunihonga.

Wa Pili kaleta barua aliyoiandika, kaenda sijuwi kuchukuwa barua gani alijibiwa mteja akaikopi neno kwa neno akaniletea, haihusiani kabisa na nilichomwambia, yeye kaleta barua ya kuwaalika wateja kuhudhuria uzinduzi wa bidhaa mpya hoteli ya Serena. Nilibaki kucheka tu.

Watatu kaona isiwe tabu, kaja, kanambia Anti, mimi kazi basi, waambie mabosi nilishapata kazi kwengine.

Wanne na watano hawajarudi kabisa siku hiyo na wala hawajaleta nilichowaagiza, siku ya pili wamekuja kazini kama kawaida nikaita mmoja kwa boss wao kila mmoja kwa wakati wake wakanipa "identical Answer", kuwa "ala, kumbe barua ilikuwa inatakikana tukuletee jana" mimi sikujuwa na sijaanza kuitayarisha kwani nilikuwa na kazi zingine!

Wa sita, kajisikia vibaya kaomba kwenda kumuona daktari.

Hao ndiyo nguvu kazi ya Kitanzania. halafu tunauliza kwanini hatuendelei?

Pia vijana wetu ni wavivu na hata stadi za kazi ni shida,wanachowaza wakipata kazi waibe na wawe na maisha ya juu,ukimwambia nitakulipa mshahara wa laki nne kwa kuwa kwanza hujui kazi nitakufundisha utasikia ah kwa huo mshahara siwezi ,lakini anasahau kuwa hapo angetumia kujifunza kazi ili apate uzoefu wa kazi,kingine kinacho niacha mdomo wazi kwa hawa vijana ni kutojua hata kuandikareport ya kazi,umempa kazi na sasa unataka report ya kazi uliyompa ,inakuwa shughuli sana sana atakuandikia hata robo ukurasa haufiki na aliyoandika hata la muhimu hakuna ,sasa kimbembe mwambie afanye mahesabu kwenye excel ndio umempoteza kabisa,na huyu ana shahada ya Uchumi,excel inamshinda kutumia.Kusema ukweli bado tunasafari ndefu kwenye soko la ajira,pia kuna tofauti kubwa kati ya Mtanzania aliyesoma vyuo vya nje na kuishi nje na huyu wa hapa hapa linapokuja swala la ufanisi,vinginevyo huyu aliysoma hapa awe amebahatika kufanya kazi katika haya makampuni makubwa ya kigeni ambayo hufundisha stadi za kazi kwa wafanya kazi wao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom