rosemarie
JF-Expert Member
- Mar 22, 2011
- 6,887
- 3,412
Kumekucha Arumeru na sisi kama watanzania tunaotakia mema nchi hii tumeamua kujitoa kwenda kusaidia mapambano huko Arumeru, tumeingia Jiji la Moshi jana mchana na kwa mara ya kwanza nimepata nafasi ya kutembea mji wa moshi baada ya miaka mingi, huwa nakuja moshi kila mwaka lakini kila tukifika moshi tunakuwa hatuna muda wa kutembea na tunaendelea moja kwa moja hadi kijijini kwetu ambako huko hukaa hadi likizo ikiisha na huondoka kwenda stand ya mabasi na kuishia unakotakiwa kwenda.
Lakini kwa sasa nimepata nafasi ya kutembea jiji hili na kushangaa jinsi maduka makubwa niliyozoea kuyaona wakati nikiwa mdogo hayapo tena, nimeshangaa kuona zile nyumba walizokuwa wanaishi wahindi zimegeuzwa kuwa za biashara mbalimbali ambazo zinaendeshwa na watanzania wenzetu.
Tulipodadisi tumeambiwa wahindi wamekimbia baada ya kushindwa mashindano ya biashara, kwa kweli nimeshangaa sana kumwona mwafrica akimpiga bao muhindi, kazi inaendelea tutawaletea update za Arumeru kaeni mkao wa kula!