Nakumbuka siku tunapelekwa kutailiwa tuliashwa alfajili saa kumi Moja kundi Letu lilikuja na vijana 7 na mimi ndyo nilionekana mkubwa kwa hyo tulipelekwa polini na wa kwanza kutailiwa anakuwa mkubwa nikatangulizwa kwakua tupo wengi tunapangwa umbali kidogo anachukuliwa mmoja mmoja kule kwenye tukio unakutana na vijana wawili wa kukukamata na Mzee wa kazi (ngaliba).
Nimefika nikakalishwa chini yaani kuna taimingi ya kukukamata na wala sikuona kama kutakuwa na hatari yeyote kwa sababu Ngaliba alikua ameficha kisu na sikuona mtu yeyote mwenye silaa , wakanza kuniongelesha story mbili tatu, ghafla nikasikia sauti ya mama yangu nikageuka Ile kurudisha kichwa GOVI lipo chini napewa nasaha huu ndyo ukubwa usipige kelele wenzio watasikia, nikala buyu, wakimaliza wanakuficha sehemu anayekuja nae hawezi elewa kilichoendelea ilifanyika hvyo Hadi wote wakaisha, suala la ganzi na kushonwa nimekuja kulikua baada miaka kama 5+ .
Baada ya hapo unaletwa uji wa moto Sana na unanyunyiwa UNGA mweusi hivi ilikuwa inasemekana ni dawa inayotokana na GOVI lako linachomea na kusagwa inasaidia kidonda kupona mapema. Ilipofika saa Moja tukaletewa madafu.
Baadae tukapelekwa kwenye nyumba iliyopo polini na kila mtu na msimamizi wake. Hyo nyumba ni ya muda mfupi tu inakua ya nyasi kuanzia ukuta Hadi paa lake mkishapona wote Ile nyumba inachomwa moto siku ya mwisho ya kutoka inakua ni usiku, wakati inachomwa moto unambiwa usigeuke ukigeuka na Hiyo kitu Ina pinda, ( hii siyo chai mdoho wangu aligeuka kidogo nayo ikapinda kidogo)
Huyu msimamizi ndiye mwalimu wako atakaekufundisha life skills atakusimulia Hadith za mafunzo na kila kitu ukikaribia kupona unapewa Sasa Hadith za mapenzi na mengineyo.