Wahenga tukumbushane Klorokwini na mambo yake

nakumbuka baada ya serikali kusitisha usambazaji wa chloroquine, waka-introduce dawa tiba nyingine ya malaria iliyoitwa fansida, ilikuwa ina nguvu sana.

kuna mwaka fansida ilitaka kuniua mazima huku najiona....iliniongezea homa maradufu.
 
Natafakari, hivi aliyetengeneza Chloroquine alikuwa anawaza nini hasa ile harufu bado naisikia dawa ile ili upone ni lazima ukimaliza dosage utapike ndipo upate nafuu.

Mara ya mwisho kutumia ilikua mwaka 2000 sijui kama muuguzi yule wa Minaki Dispensary bado yupo 4X4X2 ule uchungu basi sio wa dunia hii olivia common dosage.
,ebana nilikuaga naiweka katikati ya ndizi au tonge ndo naimeza kukwepa uchungu.
Halafu ilikuwa nawshwa muda wa siku nne, ole wako uoge ,utajuta
 
'Kolokwini' ile dawa ina nguvu za ajabu, yaani ikikaribia kugusa ulimi tu ina uwezo wa kukivuta nje chakula chote ulichokula. Dawa chungu kama imetengenezwa na mashetani, halafu bahati mbaya iwe inakuonea, yaani ukinywa ni full kuwashwa kwa muda siku tatu mfululizo bila kupumzika, halafu muwasho wake ni hadi kwenye kinyeo na makende. Ukianza kuwashwa hujitokezi mbele za watu, maana kuna maeneo utashindwa kujikuna. Ukigusa maji hata tone tu kuwasha kunaongezeka mara tatu zaidi.
-,kweli we muhenga, mjomba umenielezea maswaibu yaliokua yakinipata
 
vijana waliozaliwa wakati mzee mwinyi anakaribia kumaliza mda wake wa urais, hawawezi kutuelewa haya tunayojadili hapa kuhusu klorokwini (chloroquine).

uhenga una gharama zake...acheni tu jamani.
Teh nashangaa hapa watu wamezaliwa enzi za mkapa ila wanavyochangia utasema walikuwepo
 
klorokwini ni kitu ingine nilimeza mara moja tu maishani miaka ya 99 au 2000 lakin cjasahau uchunguzi
 
Mie zilikuwa hazinipi shida, tatizo muda wa kumeza ule uchungu jamani mpaka kikombe nitakachotumia nitamaliza hata mwezi sikigusi, ila siwashwi wala kutapika ni kupona tu, ila uchungu ule niliziacha na kuanza kumeza fansida za Kenya rangi ya blue bahari
 
Iyo dawa imeniletea ulemavu wa kudumu kila nimalizapo kuoga lazima mwili uwashe. .hakika klorokwini sitakusahau
 
Ule muda wa kuwashwa ulikua ukifika, nazunguka nyuma ya nyumba naanza kujisugua kwenye ukuta zile kuta za upele zile nikitoka hapo mambo yanakua muswano kabisa.

Ila zilinikosakosa kuniondoa baada ya kubugi dose. Hazifai zile hata kidogo.
 
IMG_20180127_102547_399.JPG
Mhenga mwenye mafanikio aliyewawahi kukutana ana kwa ana na chloroquine hospitali.
 
Natafakari, hivi aliyetengeneza Chloroquine alikuwa anawaza nini hasa ile harufu bado naisikia dawa ile ili upone ni lazima ukimaliza dosage utapike ndipo upate nafuu.

Mara ya mwisho kutumia ilikua mwaka 2000 sijui kama muuguzi yule wa Minaki Dispensary bado yupo 4X4X2 ule uchungu basi sio wa dunia hii olivia common dosage.
Bora harufu....kuwashwa jamani, nilikuwa nawashwa iwe ni sindano yake iwe ni vidonge.....lol!
 
Back
Top Bottom