Wahenga tujuane hapa..

Tuliozaliwa 1996 tujuane hapa.
Ila shiling tano nmeitumia kununua barafu na kipnd hicho soda ya chupa 250 na kuna chupa fupi ya cocacola watoto tuliipenda kwel.

Utoto wangu mim kilo ya mchele walinunua 400
 
Mzee alikuwa ana msuli wa kiuchumi inaonekana
Naam,

Kwa sababu hiyo laki laki hivyo milioni na nusu mwaka 1992, huku anasomesha watoto, huku anajenga, huku mambo kibao, si mchezo.

Ila alikataa ulevi, alikataa wanawake wa majiani, alijituma sana kuwekeza kama hivi, na sasa tunafurahia maamuzi yake.
 
Ila zile nyimbo au mashairi ya kizalendo tuliyaimba kwa furaha, kujiamini na kwa ufahari wa hali ya juu. Mambo siku hizi tafrani, hata wimbo wa taifa tu mtoto hauheshimu.
 
Nilimwibia marehemu bibi sh 2000 nilikula wiki nzima na haikuisha nikanunua na saa ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Mwaka 1996 hiyo std 2 mpaka nilikamatwa hela nilikuwa naficha kwenye majani ya viazi vitamu shambani nyuma ya nyumba
Ukiiba hela....
Unakula vitu bila idadi.....hela ikibaki unaitupa usikamatwe๐Ÿคฃ
 
Ukiiba hela....
Unakula vitu bila idadi.....hela ikibaki unaitupa usikamatwe๐Ÿคฃ
Niliteseka sana na ile hela, mpaka nikashitukiwa na Bibi alikuwa ananipenda kunipiga alikuwa hataki , akamwambia mwalimu mkuu aisee nilichezea bakora zaidi ya laki ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Asubuhi nilipo amka makalio na mapaja yalikuwa yamevimba , Bibi akaanza tena kunikanda na maji ya vuguvugu.

What a love ๐Ÿ˜
 
Yaani 2004 unamwita mhenga huyo? Hebu tuache dharau! Watu wanazungumzia enzi ya mwisho ya Julius KN wewe unasema deni za Kiwete? Tuliotumia thumuni hebu tujuane!
Sijamwita Muhenga nimemwambia huyo ni Gen Z , mwaka 2004 nilikuwa form 3 mimi
 
Nimekumbuka nilitembezewaga kichapo na mama aliunga fimbo kama 3 za matunda passion, mbona nilitaja ela zilipo๐Ÿ™†๐Ÿฝโ€โ™€๏ธ
 
Sijamwita Muhenga nimemwambia huyo ni Gen Z , mwaka 2004 nilikuwa form 3 mimi
Na wewe siyo mhenga. Wahenga ni Sisi tuliotumia thumuni! Unaijua thumuni wewe? Au ile senti 5 ya samaki sijui alikuwa samaki gani yule mwenye mdomo umechongoka kama sindano!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ