Wahenga semeni ukweli, kuna mengi hamsemi

Wahenga semeni ukweli, kuna mengi hamsemi

Pata mtu sahihi yaan yule mnaoendane,mnachukuliana ,mnaheshimiana na kila mtu anaheshimu mipaka ya mwenzie aisee mtakaa sana ...mm na miaka 23 sasa ya ndoa ila mke wangu ndo furaha yangu ndo roho yangu.Kijana ukija pata mtu sahihi aisee ndoa ni tamu sana
 
Hivi mliwezaje kukaa na mwanamke mmoja tu miaka 35+?

Katika jambo wahenga mlizingua ni hili

Sijawaelewa
Watu wanakaa bila mwanamke kama watawa bila hata ya kuwa watawa, nini huyo mmoja.

Jishikilie kijana.
 
Hivi mliwezaje kukaa na mwanamke mmoja tu miaka 35+?

Katika jambo wahenga mlizingua ni hili

Sijawaelewa
Nipo na wife mwaka wa 24 huu.

Ukitaka kuishi nao vizuri inabidi kwanza utimize majukumu yako vizuri na pia usimbane mwache ajiachie lakini mfanye ajue mistari gani asivuke katika huo uhuru.
 
Kwa kweli mwanzo ni ngumu lakini jinsi siku zinavyoenda mnasomana tabia na kuvumiliana

Nina miaka mingi sana kwenye ndoa,
Mungu aniongoze mpaka naondoka duniani
 
Wahenga wanazingua hawasemi ukweli
Wengine wanasema walipokuwa wakikaribia nyumbani walikuwa wanafikia sehemu na kutuma watoto watangulie nyumbani kusema kuwa "Mzee amerudi yupo sehemu fulani baada ya nusu saa au lisaa atakuwa hapa". Kwa maoni yao wanasema hii iliwezesha pale nyumbani kurudisha mazingira ya kawaida na kutengeneza mazingira ya kumkaribisha mwenye mji kwa amani kabisa😀
 
Kwasababu wanawake wa enzi hizo hawakua na tabia za hovyo kama hawa wanawake wa sasa,full heshima,full utii,Mume aliheshimiwa kama mfalme wa Nyumba.
 
Back
Top Bottom