Wahalifu siyo wa kucheka nao, hiki ndicho walichofanya El Salvador

Kunyooshana kunapaswa kuende sawa na upatikanaji wa fursa nyingine muhimu za maisha kwa raia kama elimu na biashara, udhibiti wa rushwa, upatikanaji madaraka kwa njia halali na huduma bora za kijamii. Kunyooshana tu bila haya mengine hakusaidii kitu.
Kasome history ya Japan, Wajapan hawa wamestaarabika miaka ya karibuni, ila wamenyooshana sana huko nyuma, same to SK,

Kuhusu canada kuna jamii ndio zina ustaarabu damuni,
Ila kubali kataa, kuna level ya criminal activities ikifika dawa ni kurudishana kwa Mungu tu, same to panya road hapa bongo, sema hapa huwa hatufanyi intensive sana, ila kama unakumbuka walitaka kuja, wakawahishwa kadhaa kwa Mungu pakatulia, wamerudi tena wengine wamewahishwa, unaona kuna utulivu,

Watu wengine wanakuwa wameharibika beyond repair, hao unawapiga jela maisha au unawarudisha kwa Mungu,

Et leo umpeleke veta yule Dangote wa Chuga kisha umpe 4M ajiajiri unadhani ataacha uhalifu ?
 
Kunyooshana kunapaswa kuende sawa na upatikanaji wa fursa nyingine muhimu za maisha kwa raia kama elimu na biashara, udhibiti wa rushwa, upatikanaji madaraka kwa njia halali na huduma bora za kijamii. Kunyooshana tu bila haya mengine hakusaidii kitu.
Hapo tunakubaliana, kama nilivyokuambia mwanzo, watu wakizidi uhalifu wanyooshe, kisha leta hizo huduma kuzuia wimbi la pili, pia hizo nch za latin nying ni madawa tu ndo yanatesa, ila huduma za kijamii zipo poa kabisa,
 
El Salvador ni nchi ndogo ya Amerika ya Kati. Ina watu kama milioni saba hivi. Lakini ni nchi ambayo ilikuwa imeandamwa vibaya sana na magenge ya uhalifu na mauaji. Ilikuwa ni moja ya nchi zinazoongoza duniani kwa mauji. Kati ya watu laki moja watu 53 waliuwawa kwa mwaka(Nchi kama Tanzania ni watu kama 5 wanauwawa kwa kila watu laki moja).

Mwaka 2019 El Salvador walimchagua Nayib Bukele mwenye miaka 37 kuwa Rais wao. Moja ya ahadi yake kubwa ilikuwa ni kupambana na uhalifu. Baada ya kuingia madarakani akajenga gereza kubwa la kuchukua wafungwa kama 60,000. Ikaanza kamata kamata ya wote wenye tatuu za magenge na wote waliotiliwa shaka ya uhalifu. Na sheria zikabadilishwa ili aweze kuwashikilia na kuwashtaki kirahisi. Mpaka sasa inadaiwa kuwa zaidi ya watu 73,000 wamekamatwa na gereza lile kubwa lina watu 40,000 mpaka sasa.

Matokeo yake ni El Salvador kutoka kuwa moja ya nchi hatari duniani hadi kuwa nchi salama zaidi katika Latin Amerika. Vifo kutokana na mauaji kati ya watu 100,000 vilitoka 53 hadi 2.4! Leo watu wengi wanashangilia hilo. Bahati mbaya au nzuri vyombo vya haki za binadamu vimeanza kupiga kelele kuwa anashikilia watu kinyume na sheria!!

Wahalifu gerezani humo.

View attachment 2867360
Nyie Chadema si mnalaumu panya road kuliwa chuma?
 
Tanzania vp tuweke sharia
Labda ufisadi ,uwizi utapungua

Ova
Niliwahi kuandika hivi:

 
Hata Mimi nikiwa Rais wa Tanzania, baada ya siku 100 hautaombwa rushwa, hutasikia ujambazi, hutaona ajari,


Kuna jwtz Ina watu zaidi ya 100,000
Polisi zaidi ya 70,000
Tiss kama 21,000
Magereza kama 15,000
Pccb kama 6000
Na migambo


Sitahurumia kiumbe, sheria zote zitafuatwa.
Hutofika hata hizo siku 100,kwani unafanya kazi na malaika?
 
Kuna nchi kiongozi ukileta fyoko fyoko wanaanza na wewe,wakikushindwa wanahamia kwenye familia yako wanawapoteza wapendwa wako hadi utaomba poo.
 
Yaah! Uko sahihi mkuu. Haiti waliomba msaada wa polisi elfu 3 (Wala siyo milion moja) toka umoja wa mataifa . Na Kenya ikaridhia kupeleka polisi elfu moja. Sorry.
Na sisi tungepeleka jamaa zetu wakachangamshwe kidogo.
 
Mkuu, unachosema ni sawa, ila sio sahihi kwa 100%, huwez wapa hizo fursa hao watu waliokubuhu, inabidi usafishe kwanza hao watu ili uanze upya na kizazi fresh, yan watu wateseke kusoma kisa kuna madarasa wakati anajua anaweza pita kwenye magenge ya uhalifu akaiba mali akawa tajiri ndani ya mwezi mmoja, na hakuna kitu atafanywa ? Dawa ni hio, kamata hao wapuuzi wote, piga vya kutosha ili wengine wajue uhalifu sio njia ya maisha, kisha endelea kutoa elimu na mazingira bora ya biashara ili kutoleta wimbi la pili la uhalifu,

Huyo raisi yuko sawaaa
Bila kusahau involvement ya west na Biashara za madawa ya kulevya kwenye nchi za kilatino, kuna madon wakubwa wakubwa ambao bila kutumia nguvu hutoboi,

Mujica wa Uruguay pia alipigana sana na hawa watu alivyowashinda ghafla uchumi wa Uruguay ukapaa.
 
Back
Top Bottom