Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,239
- 12,756
El Salvador ni nchi ndogo ya Amerika ya Kati. Ina watu kama milioni saba hivi. Lakini ni nchi ambayo ilikuwa imeandamwa vibaya sana na magenge ya uhalifu na mauaji. Ilikuwa ni moja ya nchi zinazoongoza duniani kwa mauji. Kati ya watu laki moja watu 53 waliuwawa kwa mwaka(Nchi kama Tanzania ni watu kama 5 wanauwawa kwa kila watu laki moja).
Mwaka 2019 El Salvador walimchagua Nayib Bukele mwenye miaka 37 kuwa Rais wao. Moja ya ahadi yake kubwa ilikuwa ni kupambana na uhalifu. Baada ya kuingia madarakani akajenga gereza kubwa la kuchukua wafungwa kama 60,000. Ikaanza kamata kamata ya wote wenye tatuu za magenge na wote waliotiliwa shaka ya uhalifu. Na sheria zikabadilishwa ili aweze kuwashikilia na kuwashtaki kirahisi. Mpaka sasa inadaiwa kuwa zaidi ya watu 73,000 wamekamatwa na gereza lile kubwa lina watu 40,000 mpaka sasa.
Matokeo yake ni El Salvador kutoka kuwa moja ya nchi hatari duniani hadi kuwa nchi salama zaidi katika Latin Amerika. Vifo kutokana na mauaji kati ya watu 100,000 vilitoka 53 hadi 2.4! Leo watu wengi wanashangilia hilo. Bahati mbaya au nzuri vyombo vya haki za binadamu vimeanza kupiga kelele kuwa anashikilia watu kinyume na sheria!!
Wahalifu gerezani humo.