nguvukazi mikono
JF-Expert Member
- Jan 1, 2013
- 490
- 32
hii inamaanisha umefanya utafiti na kugundua sehemu zenye waislam wengi hazina skuli za kutosha, je, ulitafiti kwanini maeneo hayo hayana skuli za kutosha? (kipi kilisababisha hayo maeneo yakose skuli?) hapo kwenye uwiano, ni pagumu zaidi ya ufikiriavyo sababu mwisho wake tutaleta udini wa pili (udini wa kwanza ni kipindi hiki ), just imagine zinatakiwa nafasi 8 za watumishi na ktk hao nane mmewafanyia usaili watu 100 na ktk hao 100 hamsini ni wakristo and the rest are muslims. Kama wakristo wawili tu kati ya 50 wamefanya vizuri na waislam zaidi ya 8 wamefanya vizuri zaidi ya wale wakristo wawili,je, mtaenda kuwachukua wakristo wengine wawili ktk kundi la waliofanya vibaya usaili na kuwapunguza waislam wanne waliofanya vizuri ili kupata idadi ya waislam wa4 na wakristo wa4 ili kubalance? hapa pia nakubaliana nawewe ila kuhusu kuitwa vilaza, kumbuka kwenye msafara wa mamba kenge wamo,kuna wakristo jina tu, japo haya matusi dini zote mbili haziepuki dhambi hii,kama unataka kuhakiki fungua mitandao ya kizanzibar jinsi wakristo wanavyotukanwahapo nitaongea mtazamo wangu,mimi ukiniambia yesu sio Mungu sipungukiwi kitu,hata ukisema hakuwahi tokea mtu hapa duniani aitwaye Yesu napo haitani-affect sababu nafuata biblia inanifundisha nini, ila akiongea mkristo mwenzangu hayo maneno nitakaa naye ili tuelimishane (sio nimuelimishe, bali tuelimishane) tuko pamoja ktk hili nataka ingekuwa hivi, mikataba ya serikali na taasisi za kidini iwe WAZI isifanywe siri sawa kabisahaya ni maajabu kwangu kwa serikali kuwaundia waislam chombo huku ikisema haina dini hapo katiba itakuwa inavunjwa,kila mtu ana uhuru wa kuwa muumini wa dini aitakayo, je, ikiwakataza hao watu itawalipa? Labda katiba iseme hvyo ila ni vigumu sana
Nawasilisha
asante![/QUOTE]
Nikianza na hoja yangu ya kwanza,asababu ya maeneo yenye waislamu wengi kuto kuwa na shule za kutosha,na shule zilizopo hazina walimu ni nyingi;
1.Mkoloni alikuwa mkristo hakujenga shule maeneo ya waislamu,maeneo haya waislamu walijikitika katika elimu ya dini.Kumbuka muarabu aliwafundisha watu kiarabu na kuandika lugha ya kiarabu kwa kutumia herufi za kirumi,hivyo kabla ya mjerumani waislamu ndio walikuwa wasomi katka nchi hii.Alipokuja Mjerumani akasema watu wote waliokuwa wanajua kusoma na kuandika kiarabu hawajuai kusoma na kuandika,dunia ikabadilika kama vile kutoka mfumo wa analojia kwenda digitali.
2.Baada ya uhuru serikali haikuchukua hatua zozte kuhakikisha maeneo haya yanakuwa na shule za kutosha na walimu wa kutosha ili kubalance gap lililokuwepo kabla ya uhuru,kwa hiyo maeneo haya yakaendelea kubaki nyuma kielimu na kimaendeleo.
3.Serikali haikujenga miundombinu yya maana kwenye maeneo yenye waislamu wengi,hivyo wafanyakazi wengi wakiwemo walimu waliopelekwa huko walikimbia,pia iliwanyima wenyeji wa huko fursa ya maendeleo,uwezi kulima nyanya mtwara kisha uisafirishe mpaka Dar
4.Kwa kuwa makazi wa maeneo haya walikosa elimu na barabara basi pia umasikini ulitamalaki katika jamii yao hivyo wasingeweza kuwapeleka watoto wao kwenye shule nzuri wala kujenga shule.
5.Mtu akikosa elimu hajui thamani ya elimu,hivyo serikali ilipaswa kupeleka nguvu zake huko ili watu waende shule.
Katika hoja yangu namba tatu na kumi,tukitaka kujenga taifa lililoimara,hasa katika nchi kama hii ambayo idadi ya waislamu na wakristo inalingana au kuzidiana kidogo tu,lazima tufanye mambo ambayo tunaona hayawezekani yawe yanawezekana.Nasema hili linawezekana tukihamua labda wanaofaidika na mfumo kristo walipinge.
Katika hoja yangu namba saba,nasema serikali ijitoe kabisa kusaidia taasisi za dini kwa fedha na wafanyakazi,hakuna cha mkataba wala nini,hizo taasisi zijiendeshe kwa pesa za sadaka za waumini,kama hawawezi wafunge taasisi zao na serikali iwahudumie wananchi wake ndio jukumu lake,hili sio jukumu la misikiti na makanisa.