Wagombea Serikali za mitaa CHADEMA na ACT Wazalendo wanapatikanaje? Mbona sioni kura za maoni zikifanyika?

Wanaogopa
1. Kupigwa risasi
2. Kutekwa
3. Kufungwa kwenye viroba then viokotwe vikafukiwe kusiko julikana
4. Kubambikiwa kesi na kufungwa jela bila thamana baadae unaacha familia inahangaika
5. Msimamizi wa uchaguzi ni mwajiliwa wa chama twawala hawezi kumtangaza tofauti na ccm
6. Wanaogopa kupopolewa mawe kama wengi waliopoteza maisha kisa siasa
7. Wanaogopa Jeshi lenu la polisi kuja kukamata watu kwa kisingizio cha uvunjifu wa amani

Hayo yote yakiondolewa basi vyama vya siasa vitajumuika

Ndio sababu hata waliojiandikisha ni wale wa Kijani maana hakuna uchaguzi bali ni UCHAFUZI TU

CHAGUANENI WENYEWE MAANA TUMECHOKA KUONA MAUWAJI, WATU WANATAKA KUENDELEA KULEA FAMILIA ZAO.
 
Na kwakuwa hakuna uchaguzi huru, basi hao ccm mliowapitisha watakosa ushirikiano kabisa
 
Huko wanachaguana kwa makabila kama chadema kama sio mpare au mchaga hupati nafasi

Act wazushi wao wanaangalia kama unatokea kigoma au zenji unapewa kipaumbele


Tanzania upinzani hakuna wanasubiria uzushi na umbea wanaugeuza Ajenda

Nani atawapa dhamana ya kuwaongoza
Mbona unaidhalilisha ofisi ya msajiri wa vyama Vya siasa? Unamaanisha.msajiri aliyewekwa na serikali anasajiri vyama Vya ukabila?Kama ndo hivyo basi kashindwa kazi aliyopewa na serikali.
 
Umeonesha concern yako kama vile hujui kilichokuwa kikiendelea. Act wazalendo na Chadema vinahitaji only 24 hrs kubadilisha yoote wengine waliyo yafanya kwa four years.
Bodaboda tano tu zikifungwa bendera za chadema na zile motokari saafi nyeupe zilizoandikwa M 4 C mbili tu zinatosha kugeuza meza.
Muda utasema ukweli
Nimesikia kuna operation kamata vyombo vya moto vitakavyovunja sheria ya usalama barabarani na madereva kunyang'anywa leseni. Nadhani hawa watahusika nahii operation.
 
Waitara, Anna yule wa Arusha mpaka wanapewa uwaziri na ukuu wa mikoa wakati wafia chama mpo? What is that? Mimi siku nikianzisha chama changu nitatafuta watu ambao hawajawahi nunua kadi kwa chama chochote.
Utakianzisha katika nchi ya kusadikika.
 
CHADEMA na ACt Wazalendo wagombea Serikali za mitaa wanapatikanaje? Mbona hatuoni mkipiga kura za maoni kama CCM walivyofanya jana jumapili nchi nzima?
Kwani sitayari washindi washajulikana wao yanini wapoteze mda wao ambao kura yao haiesabiwi na haina thamani la msingi omba dua kwa sana maana Giza ninene limetanda kila sehem
 
dogo kama una hata cheti cha mgambo nikutafutie kibarua cha ulinzi upate angalau kipato kuliko kukaa bure,itakusaidia kupunguza jazba.
Ninaajiri zaidi ya watu ishirini kama vipi njoo na wewe upate ajira kuliko kuinamishwa inamishwa hapo Lumumba.
 
Ila chadema imebanwa sana Na vyombo vya dola.Nahisi ACT huenda ikachukua nafasi ya chadema huko mbeleni.
 
Mwite Erythrocyte analo jibu kwa chadema ...Mkuu uje utoe jibu
CHADEMA na ACt Wazalendo wagombea Serikali za mitaa wanapatikanaje? Mbona hatuoni mkipiga kura za maoni kama CCM walivyofanya jana jumapili nchi nzima?
 
Ila kwa sasa kugombea upinzani yataka moyo, uwe tayari kutekwa, kupigwa, kukamatwa Na polis Na au kubambikiziwa kesi ya uhujumu uchumi.
 
Si walisusia kujiandikisha sasa wanategemea wapate kura za misukule au? Wapiga kura million 20 waliojiandikisha ni CCM tupu

Wakae tuwafundishe siasa
 
Back
Top Bottom