Wagombea Serikali za mitaa CHADEMA na ACT Wazalendo wanapatikanaje? Mbona sioni kura za maoni zikifanyika?

Watajiandaaje wakati hawakujiandikisha kupiga kura
Wako twiter huko miaka ya insta iliisha
 
Ulizia jinsi watu wanavyofurumishwa kwenye vikao kila siku. Kuna wilaya viongozi wapo ndani kwa kuitisha vikao vya uteuzi. Nani hapendi familia yake. Chama ni kimoja na kitadumu mpaka Yesu arudi point.!!!!!!! Wajinga ni wale watakaong'ang'ania mfumo wa vyama vingi. Tupo China hapa na Korea Kaskazini. Tunataka viwanda siyo siasa.
 
Sijui mnakulaga kunde za wapi? Kwa mawazo hayo ya kusubiri boda boda tano bila strategy ya kueleweka na sio ile ya kusubiri waliokatwa CCM, jiandae kusubiri sana bandugu.

Sina sababu yoyote ya kutokuheshimu maoni yako lakini sikubaliani nayo.
 
CHADEMA na ACt Wazalendo wagombea Serikali za mitaa wanapatikanaje? Mbona hatuoni mkipiga kura za maoni kama CCM walivyofanya jana jumapili nchi nzima?
Wanaogopa kuzuiliwa na Polisi,maana hukawii kuskia Polisi wamezingira eneo wanapofanyia vikao vya uteuzi
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom