Wageni wengine bwana du!

Nadhani kuna angle nalazimishwa kuifikia
 
Sasa hapo ubaba wako ukowapi...

Kama wewe baba mwenye nyumba unashindwa kukemea tabia mbaya ndani kwako, unadhani sisi ndio tutaweza kufika kwako ili tuwakanye..!!??
Natafuta hapa experiences
 
kwako hutakiwi kuishi hivyo bana, amani pekee ambayo utaridhika kuipoteza ukiwa kwako ni ile inayochukuliwa na mamlaka, sio mtu mmoja, kikundi cha watu, au mnyama.

halafu hao ni watoto wadogo wanakutawala vipi!!!
Sio kutawaliwa mi nilitaka wewe free kuenjoy bila kuchupa mipaka
 
Sio kutawaliwa mi nilitaka wewe free kuenjoy bila kuchupa mipaka
sasa wameshindwa vigezo na masharti, wewe inaonekana ni wale aina ya watu wasiotaka kukwaza mtu kama mimi.

ila lazima ujiwekee mipaka, ni bora kuishi na mtoto mvivu kuliko aliyekosa adabu, siku mtakunjana humo ndani utashangaa ujasiri wametoa wapi.
 
sasa wameshindwa vigezo na masharti, wewe inaonekana ni wale aina ya watu wasiotaka kukwaza mtu kama mimi.

ila lazima ujiwekee mipaka, ni bora kuishi na mtoto mvivu kuliko aliyekosa adabu, siku mtakunjana humo ndani utashangaa ujasiri wametoa wapi.
Yaani taabu tu
 
tena wakilala sebuleni ndio watakeleka wataondoka mapema mi kwangu chumba cha wageni sijakifanya luxury kabisa kuna kitanda tu cha tano kwa sita raha utazipata kwako sijui utake kochi na AC
Nani amekuambia chumbani hata kukuwa na mkeka anajikunja vizuri anauchapa usingizi, mgeni mwenye dhamira ya kukaa kwa munda asie ba malengo ya kuondoka leo anakomaa eneo lolote utakalo mpa, as long anakula bure, anaangalia tv bure nk
 
kwako hutakiwi kuishi hivyo bana, amani pekee ambayo utaridhika kuipoteza ukiwa kwako ni ile inayochukuliwa na mamlaka, sio mtu mmoja, kikundi cha watu, au mnyama.

halafu hao ni watoto wadogo wanakutawala vipi!!!
Labda wataenda kusema kwao shemeji mtata
 
Duh jaman mbona n umri ambao unaweza kuongea nao na kuwapangia vya kufanya maana bado watto hao ukizid kuwaendekeza watakupanda kichwan kwanza hyo tv Kama vp chomoa nyaya zote ili hata wakija na flash wasiweze kufanya lolote au peleka chumban kwako then tafuta cku panga na wife mnawaita mnawapa mashart atakae shindwa awe huru kuondoka ama ukute Dada yao ashaenda kukusema vbaya kijijin ssa ndo maana wanakudharau
 
Hivi wanaume wenzangu mkoje aisee? Mwanaume ndio head of the family. Sasa hapo wewe ndio unaendeshwa. Mke anakuendesha na familia yake inakuendesha. Umeshakubali iwe hivyo, na sasa kubadilisha mfumo ni ngumu. Kitu wanaume wanakosea ni kutokuwa na msimamo imara tokea mwanzoni. Jaribu kama unaweza kuwaleta kwenye msitari, ila sasa hivi utaonekana mbaya tu. Hata ivyo usijali kuonekana mbaya. Mwisho wa siku cha muhimu ni mke na watoto. Na kama mke anazingua sana na kukupatia stress kila siku, mwambie abadilike au utaanza jali watoto tu
 
Kwani shemeji ni watoto wako? Unawafukuza sana tu. Nyumba ni ya shemeji au yako? Kwa nini watu mnaruhusu maisha yenu yanavurugwa na ndugu? Mnakosaje misimamo? Ndugu hawana shukrani. Kwao utakuwa mbaya hata ufanyeje. Mie niliachana na ndg na ndio mambo yangu yakaanza kunyooka sana sana na kampuni faida zikaongezeka mnoo. Ndg zangu ni wafanyakazi wangu.

We unaweza kumfukuza shemeji yako?
 
Nahofia watajisikia vibaya
Watajisikia vibaya wakati wewe unaumia? Na ukiumia unapata stress na hata kuhudumia watoto vizuri unashindwa na maendeleo yanarudi nyuma. Wajisikie vibaya kabisaaaa. Africa ni mambo kama haya yanaturudisha nyuma. Watu wajifunze kuwa wapambanaji. Hao vijana 15 and 17, wana wazazi. Walipowazaa walikuhusisha kwamba utakaa nao na kupata mateso juu yao? Wanatakiwa wawe na wazazi wao huko walipo. Mtoto ni jukumu la wazazi na sio shemeji. Simama imara kwa nyumba yako aisee.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…