Waganda ilipogundua Taifa lao lina mafuta walichukua vijana wao wakakimbizwa ughaibuni kwenda kujifunza kuhusu uzalishaji wa mafuta

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,333
8,254
Uganda ilipogundua Taifa lao lina mafuta walichukua vijana wao wakakimbizwa ughaibuni kwenda kujifunza kuhusu uzalishaji wa mafuta.

Hivi navyokwambia mradi wa mafuta wa Uganda unasimamiwa na vijana waliosomeshwa na Uganda.

Cha ajabu mradi wa mafuta wa Uganda unaajiri hadi watanzania.
Mradi wa Uganda unatunufaisha Afrika mashariki nzima.
Cha ajabu vijana watanzania wanauwaza mradi wa Uganda kuliko hata miradi yao.
Tuna gesi nyingi sana lakini cha ajabu ajira hamna.
Cha ajabu hata viongozi wa taifa letu wanauwaza mradi wa Uganda kwamba utaleta ajira nyingi kuliko hata gesi yetu nyingi inayozalishwa hapa nchini.

Yako wapi mabomba ya kusambaza gesi asilia majumbani mikoa yote?
Viko wapi viwanda vya kemikali na mbolea vinavyotumia gesi asilia?
Viko wapi wapi vituo vya kujaza gesi kwenye magari kila mkoa?
Wako wapi wahitimu wa fani za mafuta na gesi?
Ziko wapi ajira kwenye sekta ya gesi.

Hapa napo hakuna ufanisi, hakika panahitaji mabadiriko ya usimamizi na uongozi badala ya propaganda.
 

Naomba kichwa kisomeke hivi: Waganda walipogundua Taifa lao lina mafuta walichukua vijana wao wakakimbizwa ughaibuni kwenda kujifunza kuhusu uzalishaji wa mafuta​

 
Back
Top Bottom