Wafungwa wa kitanzania walia njaa Kenya

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Wafungwa Wa Kitanzania Walia Njaa Kenya

WATANZANIA zaidi ya 66 waliofungwa katika Gereza la Kamiti jijini Nairobi nchini Kenya, wamelalamika kuteswa na kunyimwa chakula, hivyo kuomba Serikali ifanye utaratibu wa kuwarudisha nchini ili kumalizia vifungo vyao.

Katika mazungumzo yao na gazeti hili kutoka Nairobi, wafungwa hao walidai kuwa wapo katika hali mbaya sana kiafya na mateso mengi, ikiwa ni pamoja ya kutokuwa na chakula.

“Kenya imetangaza baa la njaa na sisi Watanzania tulioko jela tunanyimwa chakula na kuambiwa kuwa Serikali ya Tanzania imekataa kuuzia mahindi Serikali ya Kenya,” walidai wafungwa hao.

Walidai kwamba Balozi wa Tanzania nchini humo (hawakumtaja jina), hafiki kuwasaidia licha ya wapo kupeleka malalamiko yao tangu mwaka 2009 wakati wafungwa wengine kutoka Nigeria, Uganda na Ghana husaidiwa na balozi zao zilizopo nchini humo.

“Tumepeleka taarifa za malalamiko yetu kwa balozi wetu tangu mwaka 2009, lakini hakufika kutusaidia na hatujui iwapo kahamishwa au katudharau,” walilalamika wafungwa hao ambao hawakutaja makosa yaliyosababisha watupwe jela.

Walidai kuwa katika gereza hilo la Kamiti, wako wafungwa 66, na wengine wako katika magereza ya Naivasha na Kisumu.

Walidai kwa sasa kuna wafungwa wengi Watanzania ambao ni wagonjwa na baadhi wanatakiwa wakafanyiwe upasuaji, lakini wanaambiwa magereza ya Kenya hayana fedha, hivyo wasubiri ndugu zao watoe fedha ndipo wafanyiwe upasuaji wakati hawana ndugu humo.

Aidha, walidai wako Watanzania wanaokufa kwa kukosa huduma za matibabu kutokana na kubaguliwa hivyo wanaomba Serikali kuwarudisha nchini wamalizie vifungo vyao.

“Tunaomba Mheshimiwa Jakaya Kikwete atusaidie kupitia Muungano wa Afrika Mashariki turudishwe Tanzania kwani Watanzania tuliopo magereza ya Kenya tunanyanyasika sana…haki hakuna na tunabaguliwa sana kwani hata sasa kuna Mtanzania mwenzetu amevunjwa mkono na askari na hajapatiwa matibabu yoyote,” walidai wafungwa hao.



Chanzo: habarileo
 
Masikini, huyo Balozi mbona anakuwa na roho mbaya hivyo! Sasa kazi yake ni nini huko kenya! Navyoijua Kenya ilivyo watakuwa wanateseka sana ndugu zetu
 
Masikini, huyo Balozi mbona anakuwa na roho mbaya hivyo! Sasa kazi yake ni nini huko kenya! Navyoijua Kenya ilivyo watakuwa wanateseka sana ndugu zetu
kwani mabalozi ya tanzania yalyoko nje yanajua nin kilichoyapeleka huko zaidi ya kubweteka 2,check washkaj wanavoteseka hapo sasa.
 
Nadhani ingekuwa bora wange uliwa tu na polisi kama waKenya walivyofanywa pale Moshi, haina haja serekali ya kenya izidi kuwa host na kuwalisha bure.
 
Nadhani ingekuwa bora wange uliwa tu na polisi kama waKenya walivyofanywa pale Moshi, haina haja serekali ya kenya izidi kuwa host na kuwalisha bure.
Bravo smatta, ican see it in your face.
 
Tatizo kwenye hayo magereza ya kenya hamna mtoto wa kigogo wa Tanzania,kama angekuepo mtoto wa kigogo huyo balozi angechangamka
 
Kweli kabisa warudishwe hapa waje kwenye magereza yetu wamalize vifungo vyao!!!wasiwatese mara 2 maana vifungo adhabu tosha!!!uchungu sana ndg zetu!!!
 
Nadhani hii ishu ya ku export petty thieves kisha kutumikia kifungo kwenye nchi ya watu tunafaa kuimaliza kiurahisi. wale wezi wangefanyiwa mob justice mara moja tumalizane nao ama police wangewapiga risasi walipowashika, hamna haja ya kuwalisha na kuwapa hifadhi japo duni kwa mda mrefu, na sote twajua kwa uvivu wao hawatalima mashamba ya serekali inavyotakikana, kazi ni kulalamika kuwa hawajashiba. ujamaa bana.
 
"Kenya imetangaza baa la njaa na sisi Watanzania tulioko jela tunanyimwa chakula na kuambiwa kuwa Serikali ya Tanzania imekataa kuuzia mahindi Serikali ya Kenya," walidai wafungwa hao.

Hii habari ingekuwa ya miaka hii, pangechimbika hapa.
 
Nadhani ingekuwa bora wange uliwa tu na polisi kama waKenya walivyofanywa pale Moshi, haina haja serekali ya kenya izidi kuwa host na kuwalisha bure.

Ukifika nyumbani kwenu muulize mama yako akupe bahasha nimekufungashia tusi lako
 
Ukifika nyumbani kwenu muulize mama yako akupe bahasha nimekufungashia tusi lako

mamangu hapa anaingilia wapi mkuu? ingawa hatukubaliana ki mawazo, kunitusi haitamfaidi yeyote. post yenyewe ni ya 2011, sijui mkuu EMT ameipata akitafuta nini. Bado na simama na statement yangu ya awali, wapigwe tu risasi hao wezi na wazungusha bakuli wabebwe na Nairobi City Council wamwagwe Dar, tushachoka eti.
 
Chai ama breakfast ikulu ni zaid ya shilingi milion32 kwa siku . Iyo nikifungua kinywa tu hapo magogon. Angalia binadamu walivyo walafi na roho mbaya!
 
Back
Top Bottom