Jeshi la Magereza lazindua sare mpya wa wafungwa wakike

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Screenshot 2023-04-26 125950.png

Jeshi la magereza nchini limezindua sare mpya ambazo zitaanza kutumika rasmi kuanzia leo Aprili 26, 2023 kwa wafungwa wakike wote wanaotumikia vifungo vyao gerezani.

Akizindua sare hizo, Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini, CGP Mzee Ramadhan Nyamka amewataka wakuu wa magereza katika mikoa yote nchini kuhakikisha wanapokea mabadiliko hayo kwa kuhakikisha wafungwa wanakuwa na sare hizo.

Azam TV
 
Hazifai

1.zinawahi kuchafuka,za blue ,orange zinaficha uchafu vizuri na zinawafaa wafungwa maana hawamudu gharama za sabuni
2. Mfungwa akiingia siku ghafla itawahi mchoresha
3 mmetuonea yanga kutuchafulia hadhi ya jezi zetu
4.skuli bus zetu zitaitwa jezi za wafungwa
 
Jeshi la magereza nchini limezindua sare mpya ambazo zitaanza kutumika rasmi kuanzia leo Aprili 26, 2023 kwa wafungwa wakike wote wanaotumikia vifungo vyao gerezani.

Akizindua sare hizo, Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini, CGP Mzee Ramadhan Nyamka amewataka wakuu wa magereza katika mikoa yote nchini kuhakikisha wanapokea mabadiliko hayo kwa kuhakikisha wafungwa wanakuwa na sare hizo.

Azam TV
Ni sababu gani zilizopelekea kubadilisha sare, au ni namna ya kupiga hela za walipa kodi?
 
Wakuu wa JF Max mello siku hizi picha na video hazifungiki kama mwanzo. Hebu irekebishwe hili au ndio tutumie app gani tuingie huko kwa simu?
Tumia app ya web.... huku hamna shida yoyote kwenye picha wala video ..... fuata maelekezo kwenye uzi huu 👇👇👇

Back
Top Bottom