Wafumaniana na kubadilishana wake zao

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,834
2,000
Katika hali isiyokuwa ya kawaida huko mkoani Mbeya, marafiki wawili waliofumaniana guest house walifikia makubaliano ya kubadilisha wake zao. Hii ilitokea baada ya marafiki hao walioshibana kufumaniana kila mmoja akiwa na mke wa mwenzake lakini badala ya kulaumiana au kudhuriana wakakubaliana wabadilishane wake.

Mabadilishano hayo yalifanyika kwa maandishi mbele ya Afisa Mtendaji na baada ya tukio hilo kila mmoja aliondoka zake akiwa na furaha baada ya kumpata mke wa ndoto yake.

Hii story nimeipata leo kupitia Redio Clouds wakati wanapitia magazeti asubuhi hii ila sikufanikiwa kupata jina la gazeti. Nikifanikiwa kupata jina la gazeti nitashusha taarifa nzima hapa jukwaani.

MAONI YANGU
Mimi nawaunga mkono marafiki hao kwa ubunifu huo kwani hata kama wasingebadilishana wake bado wangeendelea kuibiana na wangeweza kuja kuumizana siku moja. Haya mabadilishano yamesaidia sana kuepusha figisufigisu zozote ambazo zingeweza kuja kujitokeza siku za usoni.

Daudi1

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
6,860
2,000
Hizo ndoa bado hazikubaliki wangeenda mahakani kutengua, kuyo mtendaji hana mamlaka ya kutengua ndoa za watu
 
suregirl

JF-Expert Member
Jun 8, 2012
6,070
1,225
walipanga tu iwe hivyo sidhan kwa mtu mwenye akili timamu anaweza fanya kitu hicho,,,,,,
 
tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,834
2,000
nani amempa afisa mtendaji mandate ya kusainisha vitu kama hivyo?
Kwa maoni yangu amekosea...!

wamebadilishana kwa maandishi bila shuruti yeyote na kila mmoja wao akiwa na akili timamu. Tatizo liko wapi?
 
Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,951
2,000
wamebadilishana kwa maandishi bila shuruti yeyote na kila mmoja wao akiwa na akili timamu. Tatizo liko wapi?

Akili timamu na bila shuruti, interesting!!! Lakini hii haibatilishi vyetu vyao vya ndoa vya awali, wanahitaji bado kwenda mahakamani kubatilisha ndoa, na ikiwezekana waoe upya na kupata vyeti vingine. Hivi, ukiagiza chakula hotelini na kukionja kiasi/kumeja, unaruhusiwa kurudisha na kupewa kingine??
 
ERoni

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
29,859
2,000
wamebadilishana kwa maandishi bila shuruti yeyote na kila mmoja wao akiwa na akili timamu. Tatizo liko wapi?
Tatizo ni nani anampa afisa mtendaji mamlaka ya kusainisha ndoa?
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
31,672
2,000
Katika hali isiyokuwa ya kawaida huko mkoani Mbeya, marafiki wawili waliofumaniana guest house walifikia makubaliano ya kubadilisha wake zao. Hii ilitokea baada ya marafiki hao walioshibana kufumaniana kila mmoja akiwa na mke wa mwenzake lakini badala ya kulaumiana au kudhuriana wakakubaliana wabadilishane wake.

Mabadilishano hayo yalifanyika kwa maandishi mbele ya Afisa Mtendaji na baada ya tukio hilo kila mmoja aliondoka zake akiwa na furaha baada ya kumpata mke wa ndoto yake.

Hii story nimeipata leo kupitia Redio Clouds wakati wanapitia magazeti asubuhi hii ila sikufanikiwa kupata jina la gazeti. Nikifanikiwa kupata jina la gazeti nitashusha taarifa nzima hapa jukwaani.

MAONI YANGU
Mimi nawaunga mkono marafiki hao kwa ubunifu huo kwani hata kama wasingebadilishana wake bado wangeendelea kuibiana na wangeweza kuja kuumizana siku moja. Haya mabadilishano yamesaidia sana kuepusha figisufigisu zozote ambazo zingeweza kuja kujitokeza siku za usoni.
:israel:

Na bado wataendelea kuibiana au kushea, mke au mpenzi wa zamani hatongozwi!
 
GreenCity

JF-Expert Member
May 28, 2012
5,602
2,000
wamebadilishana kwa maandishi bila shuruti yeyote na kila mmoja wao akiwa na akili timamu. Tatizo liko wapi?

Hakuna mamlaka yoyote inayompa kiongozi wa serikali ya mtaa kutengua hizo ndoa na kuidhinisha hizo ndoa mpya!

Kilicho fanyika hapo ni u-layman wa kihuni kabisa na haikubaliki! Katika issue ya ndoa kisheria ina implications nyingi! Hivyo watu msitoe comments as if ile ni makubaliano ya ki biashara!
 
Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
43,689
2,000
Dah sijui na mimi nifumaniwe na mke wa nani hapa na mimi niepue chombo, kuna mtu hua namtamani sana sana hapa jukwaani, basi tu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom