Wafumaniana na kubadilishana wake zao

Habari haijajitosheleza bado, msimpinge mleta mada tu, kuna ndoa hazina vyeti, ukikaa na mwanamke ndani miezi sita kisheria anakua mkeo, atleast tungekua tunajua mahusiano yao yalikua ya namna ipi,

Anyway...nimependa ubunifu wao, wananikumbusha hadithi moja ilikua kwenye gazeti la Kiu/ Sani miaka ya nyuma...

Ni ndoa halali hizo zilikuwa
Mi ninesikiliza kwenye redio wapo leo nimecheka sn
 
Duh hiyo fair play ya nguvu! watu wanabadilishana jezi wao wameenda mbali!
 
Duh hiyo fair play ya nguvu! watu wanabadilishana jezi wao wameenda mbali!

hahahaha! kila mmoja amepata kitu roho inapenda. badala ya kulaumiana wameona bora kila mmoja aondoke na "mpenzi" wake wa moyoni akajipigie papuchi gheto kwake bila matata. huu ndio unaitwa urafiki wa kushibana...a friend in need (of a material wife) is a friend indeed. safi sana!
 
hawa wataendelea kuibiana
hao wake zao wamekua mbuzi ndio wabadilishwe kama nguo
ama kweli kua uyaone
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida huko mkoani Mbeya, marafiki wawili waliofumaniana guest house walifikia makubaliano ya kubadilisha wake zao. Hii ilitokea baada ya marafiki hao walioshibana kufumaniana kila mmoja akiwa na mke wa mwenzake lakini badala ya kulaumiana au kudhuriana wakakubaliana wabadilishane wake.

Mabadilishano hayo yalifanyika kwa maandishi mbele ya Afisa Mtendaji na baada ya tukio hilo kila mmoja aliondoka zake akiwa na furaha baada ya kumpata mke wa ndoto yake.

Hii story nimeipata leo kupitia Redio Clouds wakati wanapitia magazeti asubuhi hii ila sikufanikiwa kupata jina la gazeti. Nikifanikiwa kupata jina la gazeti nitashusha taarifa nzima hapa jukwaani.

MAONI YANGU
Mimi nawaunga mkono marafiki hao kwa ubunifu huo kwani hata kama wasingebadilishana wake bado wangeendelea kuibiana na wangeweza kuja kuumizana siku moja. Haya mabadilishano yamesaidia sana kuepusha figisufigisu zozote ambazo zingeweza kuja kujitokeza siku za usoni.


Aiseee hili tukio lilitokea Mwanza-Bugarika pia ila mmoja alishindwa kuvumilia akamuua mwenzake
 
Back
Top Bottom