Wafuatao waliwahi kukutana uso kwa uso na busara na hasira za Mwalimu Nyerere!..

Ha! Ha! Ha! Ha! Kwa hiyo baada ya LOWASA KUULIZWA ALIKOPATA hela ya kukodi ndege ndiyo ukawa MWISHO WAKE ?
 
mbowe na slaa wangeulizwa walipo zipata chopa 3 na wapiwalipo wanandoa wa ujana wao. wangelazwa chini pale ufipa wangepigwa saana hadi kuvimba makalio chezea bakora za teacher jurius
 
Mwalimu alikuwa kiongozi aliyejua udhaifu wa kila kiongozi aliyekuwa CCM, wakatii huo ndiyo maana ilikuwa ni rahisi sana kudili nao.
Katika mambo mengine mwalimu ametuachia upendo na umoja, ndiyo maana unaweza kwenda mkoa, wilaya, kijiji, au mji wowote Tanzania ukaweka makazi yako au kufanya shughuli zako, lakini nchi za jirani hawawezi kufanya hivyo kwani hawana lugha 1 inayowaunganisha.

Mtakatifu Julius Nyerere hata sahaulika kwa hayo
 
mbowe na slaa wangeulizwa walipo zipata chopa 3 na wapiwalipo wanandoa wa ujana wao. wangelazwa chini pale ufipa wangepigwa saana hadi kuvimba makalio chezea bakora za teacher jurius
mkuu huna hoja nyingine zaidi ya hizi za 1.Chopa tatu - 2. Mbowe na Slaa na hii ya Mtaa wa ufipa - Yaani ndani ya kichwa chako zimo hizi hizi tu!!
 
"uhuru wetu hauwezi kuwa safi mpaka afrika yote imekuwa huru-mwalimu"

Huyu mwalimu alijua kuwa hajui ndio maana alikuwa kiongozi mzuri.
 
mbowe na slaa wangeulizwa walipo zipata chopa 3 na wapiwalipo wanandoa wa ujana wao. wangelazwa chini pale ufipa wangepigwa saana hadi kuvimba makalio chezea bakora za teacher jurius

ha ha ha mkuu, umenichekesha sana mkuu, hao ingekuwa ni viboko tu kila siku asubuhi na jioni
 
Najaribu kufikiri sanaaaaaa

TUNAKUMISS SANA J.K.NYERERE

1. Idd Amini - Alipoivamia Tz....Mwalimu alitamka tutampiga
nduli!.. Na kweli Idd Amini alipigwa
hadi akaikimbia Uganda.......

2. Kolimba - Alipotamka CCM
imepoteza Dira na Mwelekeo...Mwalimu alimwita Dodoma akamuuliza nani kakutuma useme hivyo?!.. Ndio ukawa mwisho wa Kolimba!..

3. Samweli Sitta - Alipokuwa
kiongozi wa serikali ya wanafunzi pale UDSM aliongoza mgomo wa
wanafunzi wenzake kudai siagi na maziwa!... Mwalimu aliibuka pale chuoni akamuuliza Samweli
Samweli kwenu mnakunywa maziwa
kweli?!.. Akamwambia lala chini, akamcharaza bakora na mgomo ukaishia hapo hapo!...

4. Abdul Jumbe! - Alipotaka serikali tatu!.. Nyerere alimuuliza moja kujumlisha moja ni ngapi?!.. Jumbe
akajibu ni mbili!.. Nyerere
akamwambia kama ni mbili mbona unataka serikali tatu?!.. Huo ndio ukawa mwisho wa Abdul Jumbe
kuwa Rais wa Zanzibar!..

5. John Samwel Malecela - Ni baada ya taarifa kuzagaa kuwa amebadili dini na jina ili apate kuungwa mkono na nchi za kiislamu kugombea Urais mwaka 1995!..Nyerere alimwambia wee John wewe umeenda Arabuni mara moja umebadilisha jina sasa unaitwa Jumanne!. Ukienda mara ya pili si utabadilisha kabila?!... Huo ukawa mwisho wa ndoto zake kuwa Rais wa Tz !...

6. Edward Lowassa-Alipokodi
ndege binafsi ikampeleka hadi dodoma kwenye vikao vya mchujo wa wagombea Urais kupitia CCM mwaka 1995 alimpa lift JK!..Nyerere alimuuliza mmekuja na Ndege dodoma pesa mmetoa wapi?!.. Jina la Lowassa likakatwa kabla ya vikao vya mchujo!..

Wakamuuliza Nelson Mandela,tukupe nini ili uache usumbufu na harakati zako,wakampa cheki
ajiandikie kiasi cha fedha,yeye akaigeuza kwa nyuma akaandika UHURU NA
USAWA WA WATU WANGU-

Hakuna tena mfano wa viongozi hawa siku hizi.

Kwahisani ya mtu wa BKM2015

mkuu. hivi mzee mtei alivyoisaliti nchi kwa kukataa kupigania uhuru wa nchi alipewa adhabu gani
 
Kwa nia njema tu, nakusahihisha kidogo tu mkuu,kolimba alihojiwa katika utawala wa mwinyi sio nyerere.ila mengine yote big up.
 
mbowe na slaa wangeulizwa walipo zipata chopa 3 na wapiwalipo wanandoa wa ujana wao. wangelazwa chini pale ufipa wangepigwa saana hadi kuvimba makalio chezea bakora za teacher jurius

mkuu. pale mtaa wa ufipa ingekuwa na viboko tu kila siku
 
Namba 4 imenigusa sana, Mwalimu angekuwepo, WARYOBA na MBOWE na serikali zao 3 wangekwishne kabisaaaa.
 
mkuu huna hoja nyingine zaidi ya hizi za 1.Chopa tatu - 2. Mbowe na Slaa na hii ya Mtaa wa ufipa - Yaani ndani ya kichwa chako zimo hizi hizi tu!!

vipi madai yao haya ya serikali tatu, wasingekula viboko kweli?, 6 siku ya kuingia bungeni, 6 siku ya kutoka wakawaoneshe wake zao?
 
Back
Top Bottom