Wafuatao waliwahi kukutana uso kwa uso na busara na hasira za Mwalimu Nyerere!..

Baba alikuwa dikteta kweli kweli
Wapo wengi sana mfano mzee eng abdullah saleem al harthy, idi simba,mwl kazibure wa kibaha sec nk,
Hakuwa anaambilika wala kushaurika

Usimlinganishe mwalimu na hao vilaza wenzako. Hakuwa Dikteta, bali alikuwa mwadilifu ambaye aliweza kusimamia anachoamini kwa kuwa hakukuwa na wa kum-black mail. Hakulimbikiza mali kama wanavyofanya hao uwasemao na ndio maana alikubalika na wengi isipokuwa mafisadi

Juzi juzi hapa tumeona mikakati feki ya watu kujivua gamba, lakini mbwembwe na mashamushamu ya kuvuana magamba viliisha mara baada ya Edward Lowasa kusema 'wakimwaga ugali, namwaga mboga' unaelewa maana yake? Angekuwa Mwalimu asingerudi nyuma kwa kuwa hajashiriki wizi
 
6. Edward Lowassa - Alipokodi ndege binafsi ikampeleka hadi dodoma kwenye vikao vya mchujo wa wagombea Urais kupitia CCM mwaka 1995 alimpa lift JK!.. Nyerere alimuuliza mmekuja na Ndege dodoma pesa mmetoa wapi?!.. Jina la Lowassa likakatwa kabla ya vikao vya mchujo!...
Natamani Nyerere angekuwepo sasa na mwaka 2015!!......[/FONT][/COLOR][/SIZE]

Asante mkuu ila watu tuende mbali kidogo na tuone kwamba Lowasa hakuwa na fedha za kukodi ndege. Lowasa hakuwahi kupewa hata mbuzi na babake useme ndo utajiri ulianzia

Tangu mwanzo EL alikuwa ni mkoba wa JK (wakipiga dili fedha anakamata Lowasa ili Mwalimu asishtuke) ilivyofikia pa maji shingoni kama kawaida ya JK akamtosa Lowasa ndo maana ukaona ilikuwa kama sherehe alipofariki Nyerere baraza lilipanguliwa kwa ushawishi wa JK na Lowasa akarudi mezani....
 
kweli kuna watu wana roho ngumu yani sita na kuchapwa bakora bado alibaki CCM?mm ningeingia upinzani aisee
Nilishawahi kusikia watu wakisema na Mkapa aliwahi kuchapwa na Mwalimu/Raisi Nyerere!!! Wanaolijua hilo wadhibitishe kama kweli nalo lilitokea. Nyerere hakuwa na mchezo.
 
Nilishawahi kusikia watu wakisema na Mkapa aliwahi kuchapwa na Mwalimu/Raisi Nyerere!!! Wanaolijua hilo wadhibitishe kama kweli nalo lilitokea. Nyerere hakuwa na mchezo.
Mkapa kuchapwa na nyerere ilikuwa kawaida, tofauti na Sitta.
Kumbuka kuwa Nyerere alimfundisha Mkapa secondary. Kwa hiyo vigumu sana Mkapa kukwepa bakora at tha time.
 
Kuna mandela day sio nyerere day,au wewe ndie wale wa kijijini ambao wanaamini hadi leo nyerere bado rais?
Bobwe, ni kweli mwl Kazi bure ni kati ya watu wasomi mahiri wa kwanza ambao Nyerere aliwa "adhibu", kama mzazi yeyote anavyo weza kumuadhibu mtoto wake yeyote hata kama ni kipanga kupinfukia kama amekiuka taratibu za nyumbani,hapa namaanisha mzazi mwenye principles,mission na vision isiyiteteleka.
Kazibure amenifundisha kibaha somo la Phisics na kwa kweli alikuwa mzuri sana na nisemeni kati ya wachache enzi hizo waliokuwa wamebobea sana na wajuzi wa phisics na electronics, alipata kutuambia alisoma class moja na Nelcon na alikuwa akimzidi darasani huko uingereza, hakutumia kitabu cha nelkon kufundishia na katika kipindi chote changu cha miaka miwili kibaha sikupata kumuona kazibure akiingia darasani na zaidi ya box la chaki na duster! Somo lake kilaza alipata C national,mm nilipata A ingawa simo kati ya the best 3 wa A leval science kwa mwaka ule,walikuwepo kina Lijei,Salu,Mfundo, nasisi tuliwafuatia.
Kazibure alikuwa genius kweli lakini mm najua pia alikuwa na kiwango fulani cha uzungu na sort of arrogance, and those were against nyerere,s principles in his mission to his vision.
Nyerere was a good dictator. A dictator for the just cause.
Walale mahali pema wote Kazibure(Sir?) na Nyerere.
 
Asante mkuu ila watu tuende mbali kidogo na tuone kwamba Lowasa hakuwa na fedha za kukodi ndege. Lowasa hakuwahi kupewa hata mbuzi na babake useme ndo utajiri ulianzia

Tangu mwanzo EL alikuwa ni mkoba wa JK (wakipiga dili fedha anakamata Lowasa ili Mwalimu asishtuke) ilivyofikia pa maji shingoni kama kawaida ya JK akamtosa Lowasa ndo maana ukaona ilikuwa kama sherehe alipofariki Nyerere baraza lilipanguliwa kwa ushawishi wa JK na Lowasa akarudi mezani....
sasa hivi wanaonja joto ya jiwe,nguvu ya pesa imewaponza
 
wanaosema nyerere allikuwa dikteta kwa upande mmoja wanakosea coz tukumbuke kipindi hicho kilikuwa cha ujamaa,na atika ujamaa mara nyingi huwa hamna demokrasiia na watu wengi hudefine kwamba lack of democracy ni dictatorship
 
Hoja nzuri, ila kuna sehemu hujaweka ukweli, mfano hoja ya Mzee Jumbe, Lowasa ......fact ulizoweka sio sahihi

1. Idd Amini - Alipoivamia Tz.... Mwalimu alitamka tutampiga nduli!.. Na kweli Idd Amini alipigwa hadi akaikimbia Uganda....

2. Kolimba - Alipotamka CCM imepoteza Dira na Mwelekeo... Mwalimu alimwita Dodoma akamuuliza nani kakutuma useme hivyo?!.. Ndio ukawa mwisho wa Kolimba!..

3. Samweli Sitta - Alipokuwa kiongozi wa serikali ya wanafunzi UDSM aliongoza mgomo wa wanafunzi wenzake kudai siagi na maziwa!... Mwalimu aliibuka pale chuoni akamuuliza Samweli Samweli kwenu mnakunywa maziwa kweli?!.. Akamwambia lala chini, akamcharaza bakora na mgomo ukaishia hapo hapo!...

4. Abdul Jumbe! - Alipotaka serikali tatu!.. Nyerere alimuuliza moja kujumlisha moja ni ngapi?!.. Jumbe akajibu ni mbili!.. Nyerere akamwambia kama ni mbili mbona unataka serikali tatu?!.. Huo ndio ukawa mwisho wa Abdul Jumbe kuwa Rais wa Zanzibar!..

5. John Samwel Malecela - Ni baada ya taarifa kuzagaa kuwa amebadili dini na jina ili apate kuungwa mkono na nchi za kiislamu kugombea Urais mwaka 1995!.. Nyerere alimwambia wee John wewe umeenda Arabuni mara moja umebadilisha jina sasa unaitwa Jumanne!. Ukienda mara ya pili si utabadilisha kabila?!... Huo ukawa mwisho wa ndoto zake kuwa Rais wa Tz !...

6. Edward Lowassa - Alipokodi ndege binafsi ikampeleka hadi dodoma kwenye vikao vya mchujo wa wagombea Urais kupitia CCM mwaka 1995 alimpa lift JK!.. Nyerere alimuuliza mmekuja na Ndege dodoma pesa mmetoa wapi?!.. Jina la Lowassa likakatwa kabla ya vikao vya mchujo!...
Natamani Nyerere angekuwepo sasa na mwaka 2015!!......
 
Nimeipenda hiyo ya 4 ya abdul jumbe hahahahahahah lazma uishiwe pozi ukiulizwa hvyo hahahah RIP the father of traditional African socialism
 
Njaa ni kali mpaka sasa

Vyakula na nguo vipo sasa madukani (soko huria) wananchi hawana hela ya kuvinunua

barabara alizitoa kutoka kwenye kiwango cha sufuri mpaka barabara angalau za vumbi (alijitahidi)

Freedom of speech na kuruhusu kumcriticise alizuia kwasababu ilikua ndio njia pekee ya kumkalisha mbali mkoloni kwasababu hizi ndio zilikua njia kuu za mkoloni kupenyea (ukizingatia wakoloni hawakupenda kuondoka)

Fikira za Nyerere lazima zidumu kwasababu zilikua nzuri (sio zote). Hata za JK tunazipinga lakini zinadumu

Waliokimbia nchi walikua ni waliotaka kupindua nchi (wahaini). Ila sasahivi wanakimbia zaidi kuliko kipindi kile!

Mashirika yalikufa kipindi cha Mwinyi (Huyu ndio rais Mbovu aliewahi kutokea TZ). Alirudisha nyuma kila sekta, hasa elimu na kilimo.

Usalama na majirani ulikuwepo kuliko sasa!

Nyerere bado anashika namba 1 katika marais walioingoza TZ.

huyo mtoto wa late 1990s hawezi kuelewa haya mambo mkuu,alishamezeshpwa sumu ya kutosha na wazazi/ndugu zake,sasa ndio wakati wa kuitoa.
 
Najaribu kufikiri sanaaaaaa

TUNAKUMISS SANA J.K.NYERERE

1. Idd Amini - Alipoivamia Tz....Mwalimu alitamka tutampiga nduli!.. Na kweli Idd Amini alipigwa hadi akaikimbia Uganda.......

2. Kolimba - Alipotamka CCM imepoteza Dira na Mwelekeo...Mwalimu alimwita Dodoma akamuuliza nani kakutuma useme hivyo?!.. Ndio ukawa mwisho wa Kolimba!..

3. Samweli Sitta - Alipokuwa kiongozi wa serikali ya wanafunzi pale UDSM aliongoza mgomo wa wanafunzi wenzake kudai siagi na maziwa!... Mwalimu aliibuka pale chuoni akamuuliza Samweli "Samweli kwenu mnakunywa maziwa kweli?!.." Akamwambia lala chini, akamcharaza bakora na mgomo ukaishia hapo hapo!...

4. Abdul Jumbe! - Alipotaka serikali tatu!.. Nyerere alimuuliza moja kujumlisha moja ni ngapi?!.. Jumbe akajibu ni mbili!.. Nyerere
akamwambia kama ni mbili mbona unataka serikali tatu?!.. Huo ndio ukawa mwisho wa Abdul Jumbe kuwa Rais wa Zanzibar!..

5. John Samwel Malecela - Ni baada ya taarifa kuzagaa kuwa amebadili dini na jina ili apate kuungwa mkono na nchi za kiislamu kugombea Urais mwaka 1995!..Nyerere alimwambia wee John wewe umeenda Arabuni mara moja umebadilisha jina sasa unaitwa Jumanne!. Ukienda mara ya pili si utabadilisha kabila?!... Huo ukawa mwisho wa ndoto zake kuwa Rais wa Tz !...

6. Edward Lowassa-Alipokodi ndege binafsi ikampeleka hadi dodoma kwenye vikao vya mchujo wa wagombea Urais kupitia CCM mwaka 1995 alimpa lift JK!..Nyerere alimuuliza mmekuja na Ndege dodoma pesa mmetoa wapi?!.. Jina la Lowassa likakatwa kabla ya vikao vya mchujo!..

Wakamuuliza Nelson Mandela,tukupe nini ili uache usumbufu na harakati zako,wakampa cheki ajiandikie kiasi cha fedha,yeye akaigeuza kwa nyuma akaandika UHURU NA USAWA WA WATU WANGU-

Hakuna tena mfano wa viongozi hawa siku hizi.

Kwahisani ya mtu wa BKM2015
 
Mwalimu alikuwa kiongozi aliyejua udhaifu wa kila kiongozi aliyekuwa CCM, wakatii huo ndiyo maana ilikuwa ni rahisi sana kudili nao.
Katika mambo mengine mwalimu ametuachia upendo na umoja, ndiyo maana unaweza kwenda mkoa, wilaya, kijiji, au mji wowote Tanzania ukaweka makazi yako au kufanya shughuli zako, lakini nchi za jirani hawawezi kufanya hivyo kwani hawana lugha 1 inayowaunganisha.


Najaribu kufikiri sanaaaaaa

TUNAKUMISS SANA J.K.NYERERE

1. Idd Amini - Alipoivamia Tz....Mwalimu alitamka tutampiga
nduli!.. Na kweli Idd Amini alipigwa
hadi akaikimbia Uganda.......

2. Kolimba - Alipotamka CCM
imepoteza Dira na Mwelekeo...Mwalimu alimwita Dodoma akamuuliza nani kakutuma useme hivyo?!.. Ndio ukawa mwisho wa Kolimba!..

3. Samweli Sitta - Alipokuwa
kiongozi wa serikali ya wanafunzi pale UDSM aliongoza mgomo wa
wanafunzi wenzake kudai siagi na maziwa!... Mwalimu aliibuka pale chuoni akamuuliza Samweli
Samweli kwenu mnakunywa maziwa
kweli?!.. Akamwambia lala chini, akamcharaza bakora na mgomo ukaishia hapo hapo!...

4. Abdul Jumbe! - Alipotaka serikali tatu!.. Nyerere alimuuliza moja kujumlisha moja ni ngapi?!.. Jumbe
akajibu ni mbili!.. Nyerere
akamwambia kama ni mbili mbona unataka serikali tatu?!.. Huo ndio ukawa mwisho wa Abdul Jumbe
kuwa Rais wa Zanzibar!..

5. John Samwel Malecela - Ni baada ya taarifa kuzagaa kuwa amebadili dini na jina ili apate kuungwa mkono na nchi za kiislamu kugombea Urais mwaka 1995!..Nyerere alimwambia wee John wewe umeenda Arabuni mara moja umebadilisha jina sasa unaitwa Jumanne!. Ukienda mara ya pili si utabadilisha kabila?!... Huo ukawa mwisho wa ndoto zake kuwa Rais wa Tz !...

6. Edward Lowassa-Alipokodi
ndege binafsi ikampeleka hadi dodoma kwenye vikao vya mchujo wa wagombea Urais kupitia CCM mwaka 1995 alimpa lift JK!..Nyerere alimuuliza mmekuja na Ndege dodoma pesa mmetoa wapi?!.. Jina la Lowassa likakatwa kabla ya vikao vya mchujo!..

Wakamuuliza Nelson Mandela,tukupe nini ili uache usumbufu na harakati zako,wakampa cheki
ajiandikie kiasi cha fedha,yeye akaigeuza kwa nyuma akaandika UHURU NA
USAWA WA WATU WANGU-

Hakuna tena mfano wa viongozi hawa siku hizi.


Kwahisani ya mtu wa BKM2015
 
Back
Top Bottom