Wafanyakazi wa TANESCO!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi wa TANESCO!!!!!

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Katavi, Mar 4, 2011.

 1. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #1
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Enzi nikiwa mdogo hawa jamaa walikuja kuweka nguzo katika nyumba yetu, lakini cha kushangaza baba siku hiyo alitufukuza watoto wote pale nyumbani.......tuliporudi tukakuta nguzo imesimamisha.
  Nilibaki nikijiuliza kwa nini tuliondolewa pale nyumbani, lakini siku moja nilipata jibu baada ya kushuhudia jamaa wakisimamisha nguzo sehemu moja jirani na pale nyumbani......dah!!! Jamaa nyimbo wanazoimba ni balaa, yale matusi ya nguoni yanageuzwa nyimbo nzuri sana za kuvutia kusikiliza............sasa najiuliza sijui zile nyimbo ndio zilikuwa zinawapa nguvu!! Au walikuwa wanafundishwa huko vyuoni kwao kuwa bila matusi yale kazi haziendi..
  Sijui kama mpaka sasa wanaendelea na utaratibu ule!!
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Mkuu siyo siri si kwamba nakopi ila nakumbuka nilikuwa nasoma shule ya msingi na enzi hizo shule ilikuwa ni sa moja hadi sita na nusu mchana kisha tunarudi home kula na tunarudi shule saa nane kwa ajili ya masomo hadi kumiunusu. Nimekumbuka waliwahi kuja kusimamisha nguzo saa sita na ndo kwanza tulikuwa tumerudi siku hiyo mama alitwambia chakula kimeungulia so turudi shule mapema tutakula saa kumi akatupa hela ya andazi moja moja. Kumbe shida ilikuwa ni hii? Wazazi bwana!
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mdau nikiwa Sumbawanga miaka ya 80-82 mitaa ya Regional Block kwa wale wanaoijua Sumbawanga miaka hiyo ndo walikuwa wanapitisha nguzo za umeme kule na kuweka umeme niliwashuhudia live na tulikuwa tunaimba sana nyimbo zao na misemo yao ni matusi makubwa sana ya nguoni lkn kuna misemo hii ya Ali fum fum mwanaume fum fum wanapandisha mlingoti juu na alijuu juu mwanaume juu juu hahahaa wale jamaa nuksiiiiiii
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Ahahahaah wale jamaa nuksi, kuna jamaa mmoja aliwahi mwambia mama yake aondoke nyumbani aliposikia jamaa wanakuja kubadili nguzo hapo!
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Mitaa hiyo naipata sana mkuu!
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Teh, si mchezo
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mambo ya uchi balaa
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Mar 5, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Jamaa wanamwaga matusi kama hawana akili nzuri vile...
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Mar 5, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Ahahahahaaah!!
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nimefanya kazi kidogo kwenye sehemu za ujenzi na hizi ni kwa Tanzania na bara la Ulaya miaka ya 90.

  Nikiwa huko, nilifikiri Wazungu hawatukani, mhhhh.....

  Jamaa walikuwa wakijenga Drinage System kubwa mjini na ilikuwa kama wanajenga line ya Metro. Nikashuka hadi chini na kwenda hadi sehemu wanayochimba na kuweka zile kuta kwa juu na chini na kukausha maji. Kuna Zee la Kizungu, lilikuwa kila likikata udongo, maji yanaruka na lenyewe linaweka tusi. Basi kila action ilikuwa ni K..., mb......, Mb.. ndani ya Ma..... Na kila kitu kibaya basi wanakilinganisha na Mb....
  Kwa Tz nilishawahi kufanya kazi pale Interchick...... Mhhh wale wabeba zege hasa kijana mmoja aitwaye Kuti akikaa Kawe.... Huyu alikuwa na tabia akiwa nyumbani, haongei kabisa na wabeba zege wenzake kwa kuhofia watamkumbushia aliyoyasema kazini.

  Kiboko ni Mkurugenzi mmoja wa Interchick aitwaye Makongoro (Nyerere family). Jamaa na shule yake swaafi USA, akarudi zake Bongo. Wakati akijenga nyumba yake, akakubaliana na wabeba zege kiasi cha Sh.60,0000 ya miaka ya 80. Jamaa wamekula mzigoooo wakaona hela mbuzi na wakagoma kufanya kazi. Kufika usiku kama saa sita, Makongoro kaingia na msosi kwenye Pajero lake na anakuta kazi imesimama. Wakadai walipwe Tsh 80,000 wamalizie kazi. Jamaa likawaangalia na kuwaambia " mkitaka hiyo hela, sawa ntakupeni ila nikuf*** kwanza nyote." Jamaa wakajua leo wamekutana na mtoto wa kihuni na wakamalizia tu kazi na kujiondokea.

  Siku iliyofuata wakaja wenyewe wanasema "hili li Makongoro halifai, jana limetutukana kishenzi....."

  Wabeba zege, Makuli wa bandari, wafanyakazi wa Tanesco, Dawasco nk nk matusi ni kama MAFUTA yao. Wakisharusha matusi ni kama wamejiwekea petrol.

  Matusi huwa yanasaidia sana kupandisha morali ya mtu na kumpa nguvu na kujiamini.

  Kama hujaingalia film ya KING'S SPEECH, basi nenda humo ndani uone Baba yake Queen Elizabeth akiporomosha matusi.
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  sure,tanesco+makuli wa bandarini,ni laana
   
 12. Ba Martha

  Ba Martha JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mafundi magari..pikipiki..nao wamo mkuu.
   
 13. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ha hahaaaaa!!!!
  mie nilishuhudia nguzo ya jirani yangu ilidondoka wakaja, ghafla nikaona kina mama wamejazana wanacheka sana, nikatamani nichungulie dirishani, huwezi amini, sikubanduka pale mpaka nguzo ilivyosimamishwaaaa, ilikua balaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!

  Tanesco ni nuksi naona wamefundishwa kutukana wale!!
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Mar 5, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kumbe ni sehemu zote tu wanakotumia nguvu lazima matusi yawepo!
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  Mar 5, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Sijui wanapewa semina kabla maana wote akili zinafanana!
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Mar 5, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Bila kuwasahau wabeba mizigo kwenye masoko makubwa kama pale kariakoo.
   
 17. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #17
  Mar 5, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Ahahahahaaah!! Huenda ulijifunza maneno mengi sana.
   
Loading...