Anonymous Caller
JF-Expert Member
- Sep 8, 2016
- 480
- 571
Wadau wa lugha,
Na Mimi bwana nimebahatika kupata kashahada fulani kutoka moja ya vyuo vyetu vikongwe.
kwahiyo ka-english ka hapa na pale kakuombea maji huwa ninako. Masomo ya english secondary nilipa daraja B.
Tatizo kuu langu ni moja;
Ukiongea wewe kiingereza (mswahili mwenzangu) huniteti chochote,
nitakuelewa vizuri sana.
Akiongea kiingereza mwafrika mwenzangu(mkenya,mnigeria,msauz nk&)
haniteti pia nitamwelewa anavyoniongelesha.
Akiniongelesha mzungu yeyote asiyekuwa mmarekani,mwingereza,au yeyote ambaye kwake english sio mother tongue, huyu nae hanisumbui sana.
Shida ipo kwny kumwelewa mzungu au mweusi ambaye kwake ENGLISH ni mother tongue au native language.
Naomba niwe muwazi, huwa siambulii kitu.
Sijui midomo ya hawa jamaa ikoje.
wanaongea micharango mno.
Cha ajabu sasa, yale anayonisemesha YAKIANDIKWA mahali ni kiingereza chepesi sana.
Kuna nyimbo nzuri sana za kizungu mfano akina usher raymond, nelly, etc
wakiimba ndio hamna kabisa.
Ila zile lyrics za nyimbo wanazoimba akina rihanna ukipewa ni english changa kabisa.
Mwaka Juzi, nikiwa naangalia mechi fulani ya liverpool, Michael owen alikuwa mchambuzi siku ile.
Nilitamani sana kujua nini owen anasema lakini kutokana na tatizo hili sikutoka na kitu.
utafikiri sikusoma.
Tulikuwa tunaangalia movie fulan nyumbani, ka-wife si kakaomba nikatafasirie! Nilibumbabumba uongo.
Drogba alipokuwa akihojiwa kwenye interview namuelewa. Aongee lampard sasa!
Kujua kiingereza jambo moja, kumsikiliza na kumwelewa English native speaker ni jambo jingne.
Sasa hebu tushaurianeni.