muzee mbona unaandika uongo ambao wewe mwenyewe unaelewa ni uongo.
Kuhusu mizigo mingi inapotelea hapo hapo tanzania bada ya kufungua hilo bag la posta, sasa ukizungumzia bag la posta kupotea ni kitu kikubwa, hata usa au uk na nchi zingine kutokea hilo ni vigumu, bali kupotea kwa item, kabla ya kuwekwa katika bag. hilo lina weza kutokea usa au uk etc, lakini wenzetu wana taratibu ya kuandika vitu vinavyo wekwa katika bag, hivyo ni rahisi kugundua kitu kiliondoka au la. kuhusu kwenda sehemu tofauti linaweza kutokea lakini mwisho wa siku kitu kitarekebishwa na kwenda ilipotakiwa kwenda.na nafikiri si kitu kunacho ongelewa hapa.
kitu kinacho ongelewa hapa ni kupotea kwa item, sio bag, kwa sababu mimi kama mtu moja ninapo tuma kitu na tuma kama item na sio bag ambalo litajumuisha barua au vitu mbali mbali toka kwa watu mbali mbali.
nafikiri utakuwa umenielewa na wadau wengine wameelewa. kwamba kinachoongelea hapa ni item ambayo mtu binafsi anatuma kwa nduguye au rafiki na si bag, la posta ambalo lina-contain vitu mbali mbali, sasa wizi unaweza tokea kabla ya kufunga hilo bag au baada ya kufungua hilo bag kwenda stage nyingine.
Serikali inafanya nini kuhusu wizi katika posta nchini Tanzania? Hata barua za kawaida zinaibiwa na kufunguliwa na wafanyakazi wa posta.
Nimewaandikia ndugu zangu mara nyingi na, kila mmoja wao, wamesema barua pamoja na picha nilizowatumia hazikuwafikia. Na wote wameniambia nisithubutu kuwatumia kitu chochote kupitia posta nchini Tanzania. Na mmoja wao amesema wananchi wengi wanasema itakuwa ni vizuri posta zikifungwa kwa sababu ya wizi huo ambao unaendelea kwa kasi.
Malalamiko hayo yanatoka sehemu zote za Tanzania. Ndugu zangu niliowaandikia wanaishi sehemu mbali mbali - Dar es Salaam, Mtwara, Iringa, Mbozi, Mwanza, Bukoba, Tabora, na Arusha.
Hakuna posta nchini ambayo haina wafanyakazi wanaoiba vitu mbali mbali - barua, vifurushi - vinavyotumwa kutoka n'gambo. Pia wana akili pungufu wanapofikiri kwamba kuna fedha katika barua hizo wanazozifungua.
Labda wananchi wakigoma kutumia posta, hatua zitachukuliwa kupambana na wizi huo.
Nimeishi n'gambo miaka michache (au mingi?) - zaidi ya kumi - na ni jambo la kukatisha tamaa kwa watu kama mimi tunaotaka kurudi nyumbani tunapoona serikali haifanyi chochote kurekebisha mambo - wizi, rushwa, mahongo, ufisadi na kadhalika.
Tutajengaje taifa letu? Kama Mwalimu alivyosema, "Tanzania itajengwa na wenye moyo."
Haitajengwa na wezi. Haitajengwa na wala rushwa au mahongo, na haitajengwa na mafisadi. Wamejaa serikalini na katika kila wizara na idara na sehemu mbali mbali kazini.
Halafu kuna viongozi wanashangaa kwa nini wananchi wengi hawataki kurudi nyumbani? Si Tanzania tu bali nchi zote katika bara letu.
tatizo ni kuwa hapa kwetu huu wizi unatokea na hakuna kinachoonekana kuwa kinafanywa kukabiliana nao tofauti na huko majuu ambako wizi unatokea na inaonekana simething is being done kushughuklikia tatizo hilo, ndio maana hata mnaweza kwua na data kwua asilimia fulani ya vifurushi vinapotea. Uliza hapa kwetu kama utapata data kama hizo, hii inaamnisha kuwa hakuna anayeshughulikia tatizo hilo kwa ukamilifu
Ushauri wangu wa kitaalamu kwenu ni kama ifuatavyo:
Ni vyema zaidi kwa mtumiwa kuwa na sanduku lake binafsi la barua ili kuweza kudhibiti barua ziingiazo katika sanduku lake. Gharama ya sanduku binafsi la kupokelea barua kwa mwaka ni sh. 12,000/- kwa Ofisi Kuu ya Posta Dar es Salaam, sh. 9,600/- kwa ofisi za Posta zilizoko miji mikuu, sh. 7,200/-kwa Ofisi za Posta Wakala (Franchised Post Offices) na zile zilizoko wilayani na sh. 1200/- kwa ofisi za Posta zilizoko vijijini. Uwezekano wa mzigo kupotea au kuibiwa ni mkubwa kama unatumia address ya taasisi, kijiji au jirani.
Je Shirika letu la posta lina masanduku ya kutosha kwa watanzania wote??
Kana ka Nsungu (Katoto ka Kizungu),
Bado siamini you have the audacity kuja hapa kuongopa na kutetea shirika la posta in spite of all the incontrovertible evidence there is kuhusu wizi wa wafanyakazi katika posta nchini Tanzania and knowing full well that nothing is done about it.
SIJAONA MTU ALIYETOA USHAHIDI HAPA KUHUSU BARUA AU PARCEL YAKE KUIBIWA POSTA ZA NYUMBANI.
It's more than just incompetence on the part of the postal workers - it's pure theft on their part and gross negligence by the postal administrators many of whom are thieves themselves; compounded by the unwillingness of the government itself to address the problem.
HIZI LAWAMA ZISHIISHIE KWA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA TU NA SEREKALI YETU, FOR INTERNATIONAL MAIL AMBAZO WENGI MNAZILALAMIKIA HUMU WAHUSIKA NI WENGI!
And you come here to lie for them? You've got the nerve!
I HAVE NOTHING TO GAIN, AM ONLY HERE TO SHARE MY INSIDE KNOWLEDGE WITH YOU.
Baada ya kumaliza masomo yako Uingereza na kurudi Tanzania, ikiwa hutaamuwa kubaki huko UK, you're going to be part of the problem and not part of the solution to this national crisis which is also a national scandal.
FOR THE RECORDS- NILIRESIGN SIKU NILIYOPATA VISA YA KUJA UK, AM WORKING IN A COMPLETELY DIFFERENT INDUSTRY NOW.
In this era of globalisation nchi yetu imejaa investors na watu wengi kutoka nchi za nje. And you don't think they notice this? Is this the kind of image we want to project for our country hata kama hujali hali na matatizo ya ndugu zako wanaoibiwa kila siku na wafanyakazi wa posta?
HUU WIZI/UPOTEVU KWENYE MASHIRIKA YA POSTA NI MKUBWA SANA HUKO HAO MAFOREIGN INVESTORS WANAPOTOKA,NAAMINI PARCELS ZETU ZINAIBIWA HUKO HUKO KWAO LAKINI KWA ULIMBUKENI WETU WENGI TUNAAMINI KUWA 'WAZUNGU SIO WEZI!'
Kama nilivyosema mwanzoni, niliwahi kulalamika posta, via mail, nilipomwandikia postmaster Dar. Hakunijibu. Pia nilimpa email address yangu. I was just ignored. And I'm NOT the only one who has complained to the authorities in Tanzania about theft at our post offices across the country. We all have been ignored by these arrogant, corrupt leaders.
TUMIA ZILE CONTACTS AMBAZO NIMETOA HAPA, THOSE GUYS WILL RESPOND. BADO POSTA MASTERS WENGI NI WALE WAZEE WA ENZI YA MKOLONI NA HAWAONI UMUHIMU SANA WA KUJIBU EMAIL KAMA ZAKO BUT THANKS GOD WANASTAAFU MMOJA MMOJA NA VIJANA WADOGO WAMEANZA KUCHUKUA NAFASI. POSTA YA LEO SIO ILE YA ZAMANI, ITS IMPROVING.
Kana ka Nsungu, sijiu hata ukiweza kuwasikia wananchi wote waliobiwa posta utabadilisha mawazo yako.
NAJUA WIZI UPO LAKINI NINACHOPINGA HAPA NI WATU KAMA NYIE KUSISITIZA KUWA HUO WIZI UNATOKEA BONGO TU, MASHIRIKA YA POSTA DUNIANI YANAFANYA KAZI KWA KUSHIRIKIANA WHEN IT COMES TO INTERNATIONAL ITEMS SASA ITS UNFAIRS KUMWAGA LAWAMA ZOTE KWA MOJA TU.
Everybody who has read what you have written knows you are not telling the truth. And you know it. There's also the suspicion that you have been sent here to lie for the postal service or you're doing it on your own for future promotion when you return to Tanzania and rejoin this disgraceful corporation riddled with scandal.
SIJATUMWA NA MTU AND I HAVE NO PLANS TO GO BACK THERE, THEY CANT AFFORD TO PAY MY WAGES!
Nani amesema hakuna wizi katika posta nchi za wazungu? Tofauti, na ni tofauti kubwa, ni kwamba they do something about it. They arrest and prosecute the culprits. And they punish them severely.
THESE ISSUES ARE DEALT WITH INTERNALLY BY THE CORPORATION AND SITAKI NIANZE KUTAJA MAJINA YA WATU AMBAO WAMESHAFUKUZWA KAZI HAPA. And you still don't see the difference kati ya nchi zao na nchi yetu in terms of what's done and what's not done to address the problem?
The government itself should be ashamed of this. Obviously it's not because it has many thieves itself at very high levels in all ministries and all departments.
KUNA POSTA MASTA GENERAL(MKUU WA SHIRIKA), KUNA WAZIRI WA MAWASILIANO, KUNA TUME YA MAWASILIANO, ETC- UTAKUWA MVIVU WA KUFIKRI KAMA UNAAMINI KABISA KWAMBA WOTE HAO WANAJUA KWAMBA KUNA WIZI KWENYE SHIRIKA LETU LA POSTA NA WAMEKAA KIMYA TU.
But we're going to pay a heavy price for this as a nation; in fact we already are.
ABOLISH THE POSTAL SERVICE! CLOSE IT DOWN!
And start afresh with a privatised postal service. If it also fails, close it down as well and use private mail delivery services - no matter what the cost.
HII KALI, TANZANIA ITAKUWA NCHI PEKEE DUNIANI ISIYOKUWA NA SHIRIKA LA POSTA! AND I DONT THINK THESE POOR TPC CHAPS ARE THAT BAD. HIZO PRIVATE COMPANIES-UPS, DHL,ETC WANAOPERATE MIJINI TU AND ALL THEY CARE ABOUT IS MAKING PROFIT WAKATI POSTA INATOA HUDUMA ZAKE HADI VIJIJINI. WEWE KWA KUWA UKO MAMTONI NA UNAJIONA UTAMUDU GHARAMA ZA DHL UNATAKA NDUGU ZAKO KULE BUSH AMBAO KWA SIKU HAWAINGIZI HATA BUKU WASHINDWE KUANDIKA AU KUANDIKIWA BARUA, IT WONT HAPPEN!
Masanduku ya barua yaliyoko wazi ni mengi sana na hii inatokana na watu kupenda kutumia anuani za makazini, majirani au hata vijiji na hii inaongeza risk ya barua au kifurushi chako kupotea. Sio lazima kila mtanzania awe na sanduku lake la barua lakini ni kitu ambacho ningekipendekeza kwa kila household na taasisi.
barua za kwenda Mufindi haziibiwi kwa kuwa wanajua hazina kitu zaidi ya salamu na mengineyo.
Barua za Majuu wanajua kuwa zina "dola".
what you say makes sense,BUT the problem is that,people are no longer confident with the "shirika la Posta".
Shukrani kwa aliyeleta mada.mimi nimetuma zawadi za xmas mwezi na nusu sasa na bado hawajazipata na ni private box.Nimetuma vitu vya gharama na nilikuwa na wasiwasi kabla kuwa vinaweza kuibiwa lakini wakaniambia nitume tu na hawataki pesa kwani vilivyopo kule ni fake si vizuri.Baada ya kusoma hapa nahisi hivi vitu havitafika kamwe.Sasa najuta kwa gharama nilizotumia.
ongea na kkn anaweza kuarrange for refund
Shukrani kwa aliyeleta mada.mimi nimetuma zawadi za xmas mwezi na nusu sasa na bado hawajazipata na ni private box.Nimetuma vitu vya gharama na nilikuwa na wasiwasi kabla kuwa vinaweza kuibiwa lakini wakaniambia nitume tu na hawataki pesa kwani vilivyopo kule ni fake si vizuri.Baada ya kusoma hapa nahisi hivi vitu havitafika kamwe.Sasa najuta kwa gharama nilizotumia.
suala la wizi ni katabia ka mtu hivyo sio wote nadhani hii inatokana na mishahara midogo itolewayo na mashirika haya ya posta