Wafanyakazi wa Posta na wizi wa mizigo ya wananchi

Mtawalaumu tu bure wale watu wa posta, yaani huwezi amini zaidi ya 50% wa pale wako over 50 years na mbaya zaidi 50% ya wafanyakazi wa posta ni darasa la saba so unategemea mabadiliko gani tena.Cha zaidi ni kwamba lile shirika la posta limejaa ukabila yaani hata hao wazee na darasa la saba wamepata kazi kikanda,ntasema kweli daima fitina kwangu mwiko shirika la posta limejaa wachaga na wapale so tegemea kuibiwa mpaka mwisho wa maisha yako.Tunataka damu changa pale watu wanaoweza kuleta mabadiliko na sio hao wazee na darasa la saba "I stand to be corrected"!

naunga mkono hoja 100 kwa 100
 
Nimetumiwa parcel toka china since august mpaka sa hv haujafika ila ilikuwa nikitumia fedex ama usps within 2 weeks tayari nimepata
 
Mkuu EMT,

Pole sana kwa hayo mambo ya hao wafanyakazi wajinga.

Mimi nikiwa nje ya nchi kwa muda mrefu nimekuwa nikituma mizigo yangu kwa kutumia kampuni tofauti-yaani, posta ya kawaida, DHL, FEDEX na hata mikononi tu kwa watanzania wenzetu.

Mimi nimeibiwa sana, tokea mwaka 1998 nikiwa Ughaibuni. Lakini vitu nilivyoibiwa mpaka sasa ni vile vodogovidogo ingawa kwa Tanzania ni vitu ghali na vya maana sana. Nimewahi kutuma vitu kama ifuatavyo na kuibiwa na watu wa posta:

Saa za mikononi

Manukato

Vinguonguo tu kidogo- mashati, na vingine.

Lakini kwasasa nimeamua kuwa kila nikituma huwa nawataarifu ile sehemu ambayo mizigo inakwenda na wao hufuatilia na huipata bila usumbufu.

Posta na bandarini mizigo inaibiwa sana na ni aibu sana kwamba sisi waafrika tunashindwa kutumia akili hata za kufikisha mzigo kwa walengwa. Tena unaweza kupewa boksi tupu au bahasha tupu ambayo imechanwa. Ni tabia tu ya UFISADI imekolea kwenye akili ya watanzania.

Ni tabia hii ndiyo imepelekwa hata ughaibuni na hata waafrika na wageni wengine, sasa wanaiba vifurushi vya watu wanapovichambua kule kwenye "depot" za Royal Mail.

Kuna masimulizi yanayohusu baadhi ya watanzania walio ughaibuni ambao wamewahi kukamatwa kwa kuiba vifurushi na bahasha pale UK na leo hii wanaonekana ni watu wa maana. Ni katika wizi huo walikuwa wakiiba kadi za benki za watu, na vitu vingine vyenye thamani.

Mimi ni mwanachama wa Ebay na pia Amazon na huwa nanunua vitu vingi vyenye thamani lakini kila wakati nikituma mizigo Tanzania basi hutumia DHL au FEDEX maana mtumiwa atakwenda kuchukua palepale osifini kwao lakini nilikwishapoteza imani na posta Tanzania.

Ni wezi sana.

Ushauri - kwa kiingereza

postgraphicDM0405_468x321.jpg

Angalau tukiafuata ushauri huu tutaokoa asilimia fulani ya mizigo.
 
Hii nimeikuta kule wavuti. Hii siyo mara ya kwanza kusikia malalamiko kama haya. Nimeyasikia kwa watu wengi tuu. Parcel wanazotuma haziwafikii walengwa. January Makamba (Naibu Waziri) ambaye amemwambia mlalamikaji kuwa atafuatilia hili, kasema pia kuna mwananchi mwingine aliwasilisha tatizo linalofahanana na la huyu mlalamikaji. Kwa nini hii kadhaa iwepo in the first place? Imagine watu badala ya kufanya shughuli zao wanalazimiswa na wadokozi wa posta kufuatilia mambo kama haya. Halafu watu wanapoamua kutumia makampuni au njia nyingine kutuma parcels zao wanaanza kulalama eti hatulitakii mema shirika la posta. Posta ya Tanzania inaiba parcel za watu?

==================================================

Nimetuma parcel Tanzania (na hii si mara ya kwanza), kwa njia ya USPS Express Mail, 3-5 days delivery na mara zote ninaowatumia wanapokea kati ya siku ya 5 - 7.

Hii niliyotuma tarehe 17 Septemba, 2012 aliyetumiwa hakupigiwa simu wala kutaarifiwa kwa namna yoyote kuwa parcel imefika. Baada ya zaidi ya siku 7 kupita, akaanza kufuatilia. Akipiga simu anaambiwa hatuuoni, bado haujafika. Akaamua kwenda kuwaona ana kwa ana jana, akapewa majibu yale yale. Nikamfahamisha kuwa waliwahi kunipotezea mizigo hawa kwa kauli hizo hizo, na baadaye walipopigiwa simu na "Mkubwa" wao, mzigo ulijulikana uliko ndani ya saa chache siku ile ile.

Nikamfahamisha aombe kuonana na Meneja, akafanikiwa. Wakatizama parcel, computer zao (huko kwa Mameneja) zikaonesha parcel ilifika tangu tarehe 23. Meneja akaagiza watizame vifurushi ili wampatie. Kwa kuwa ilikuwa imekaribia muda wa kufunga ofisi, wakamwambia arudi kesho (yaani leo) kuuchukua, lakini kwanza apige simu asubuhi au wao watampigia utakapokuwa tayari. Akawapigia simu asubuhi, wakamwambia bado, apige saa nne. Akapiga simu saa nne, anapewa maelezo tofauti na ya jana, Meneja anamwambia kifurushi hakijapokelewa na maelezo mengine ya kuwa maelezo ya jana haikumaanisha hivyo bali vingine. Amepiga simu kutaka kutoa maelezo mwa Mkubwa wa Posta (Rais Kikwete ateua mkuu mpya wa Shirika la Posta), anajibiwa kuwa hawezi kuzungumza naye suala hilo, amwambie tu aliyetuma ajaze hayo makaratasi ya USPS ya refund alipwe fidia.

Nilipoandika juzi pale wavuti.com kuwa baadhi ya Wafanyakazi wa Posta ni wadokozi na waache udokozi, ni kwa sababu nimeshapata usumbufu mara tatu na sasa ni mara ya nne katika Shirika la Posta la Tanzania, EMS, mkoa wa Dar es Salaam.

Mara mbili kati ya hizo parcel nilizotuma kwa njia ya kawaida hazikufika. Mara moja nilipotuma kwa njia ya USPS Express Mail waliupoteza lakini walipigiwa simu na Mr. Mndeme na ndani ya saa chache maelezo yote na ulipo mzigo vilipatikana. Hii mara ya nne, inakuwa ni mara ya pili kutuma kwa USPS Express Mail parcel inapotea na maelezo ya kufuatilia kujua ulipo ninayopewa ni hayo niliyoeleza hapo juu.

Nimetaka ku-vent off kwa sasa, ila kazi ndiyo (isiyo ya lazima) ndiyo imeanza tena. Kwa bahati mbaya (au nzuri) kazi ndiyo imeanza rasmi. Posta, nina nyie, mpaka kieleweke kwangu kwa lugha yangu!

YOU WILL COUGH UP TO THE LAST DIME!!! This I promise you! Here I come..

Posta ya Tanzania, Dar es Salaam: Mara tatu ilitosha, si hii ya nne. Hapana! - wavuti.com

Njaa mbaya sana ndugu yangu shilika la posta lina nuka shida na kifo chake kinakaribia
 
Mkuu ilitakiwa iwe imewasili baada ya muda gani? Ingekuwa bora kujua ni wangapi walishawahi kupatawa na tatizo kama hili maana kwa wengine inaonekana kama kero sasa.

Mimi nimepoteza parcel nyingi sana posta, sasa hivi huwa nahakikisha inakuja na registered service (signed-for), kwa namna hii zote nimezipata

Posta kuna wizi mkubwa sana!

 
Tukisubiri wateja wote wa posta wafanye kama hawa wazungu huu wizi hamtaukomesha!
Mchawi mpe mwana akulelee.Sasa Mkumbo Kitilla Mh ni sehemu ya serikali.
Tutategemea ushauri wako uupeleke Bungeni na kwenye Cabinet. Ninaamini utamsaidia Posta master General na Ndugulile.
 
Back
Top Bottom