Mapendekezo ya kuboresha ufanisi wa Shirika la Posta Tanzania

ndo vile

Member
Mar 11, 2023
25
12
POSTA KIDIJITALI, (TUPO SITE TOUR), TUtume Popote SIsi Tumeenea kila Eneo.

TUPO SITE ni kauli mbiu inayowakilisha utayari, nia thabiti na dhamira tulionayo Shirika la Posta Tanzania katika kuwafikia,kuwasikiliza na kuwahudumia wananchi na wadau wetu pasipo kuangalia umbali na sehemu wanapotoka,(popote tunafika), utayari wa kwenda sambamba na mabadiliko ya kiteknolojia yanayotokea ulimwenguni na kutoa huduma zinazokwenda na wakati zenye ubunifu,ufanisi na kwa haraka kwa kuzingatia matakwa na mahitaji ya wananchi/ wadau, utayari wa kuja na huduma na biashara zenye ubunifu na mvuto zenye kukidhi mahitaji na matakwa ya wananchi/ wadau kutoka kada tofauti na maeneo tofauti, kama wanafunzi, wakulima, wavuvi, wafanyabiashara kutoka maeneo ya mijini na vijijini, utayari wa kufanya kazi kwa uwaminifu, uzalendo,weledi na bidii kubwa ili Shirika tuweze kutoa mchango katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Kwa upande wa pilii TUPO SITE ni kufupi cha maneno yanayokilisha TUtume POpote SIsi Tumeenea kila Eneo likimaanisha ,Shirika la Posta Tanzania pekee ndiyo tuna uwezo na uhakika wa kutoa huduma katika kila pembe ya Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania, Shirika la Posta Tanzania tuna ofisi katika kila wilaya Tanzania nzima,pia sisi ni wanachama wa mashirikisho ya posta duniani kwa kupitia sisi pekee unaweza kutuma na kupokea mzigo eneo lolote ulimwenguni,Tutume Popote Sisi Tumeenea kila Eneo pia linawakilisha uwezo wetu wa vitendea kazi na teknolojia tunazotumia katika kuwahudumia wananchi na wadau wetu,mfano tuna wafanyakazi wa kutosha kila wilaya,magari,pikipiki,bajaji,ofisi n.k

POSTA KIDIJITALI (TUPO SITE TOUR), TUTUME, POPOTE, SISI, TUMEENEA KILA, ENEO TOUR
Ni ziara zinazoandaliwa na Shirika la Posta Tanzania zenye lengo la kukutana na kuwajengea uelewa wananchi/wadau juu ya huduma na biashara zinazotolewa na Shirika la Posta Tanzania na kuzitangaza huduma kwa wananchi/wadau wa maeneo ya mjini , vijijini na nje ya mipaka ya nchi.

POSTA KIDIJITALI, (TUPO SITE TOUR), TUTUME POPOTE SISI TUMEENEA KILA ENEO TOUR, ni jukwaa muhimu kwa Shirika la Posta Tanzania kuzitangaza huduma na biashara tunazozitoa kwa wananchi na wadau wetu,wananchi na wadau wetu kupata uelewa juu ya umuhimu wa huduma na biashara za Posta zilizoboreshwa kidijitali, wananchi/wadau kupata fursa ya kutoa maoni yao juu ya huduma na biashara zitolewazo na Shirika la Posta, fursa kwa shirika kueleza mipango na mikakati yake kwa wananchi/ wadau, fursa kwa shirika kueleza ubora wa huduma/biashara tunazozitoa kulinganishana na wapinzani wetu, fursa wadau na wateja kuelekezwa jinsi ya kutumia huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika la Posta hususani huduma za kidijitali, fursa kwa wadau na wateja kuelezewa kwa mapana faida na manufaa yatokanayo na utumiaji wa huduma mbalimbali zitolewazo na Shirika la Posta Tanzania.

Kwa kupitia POSTA KIDIJITALI (TUPO SITE TOUR), shirika tutapata fursa ya kutembelea mikoa mbalimbali inayopatikana Tanzania bara na visiwani. Kwa kutumia makongamano,semina,michezo na maonyesho ya wazi tutakayoandaa shirika la posta tutapata fursa ya kukutana na wananchi na wadau wetu muhimu, kuonyesha na kutangaza huduma na biashara zitolewazo na shirika, kuwaelekeza wananchi na wadau namna ya kutumia huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hususani zitolewazo kwa njia za kijiditali,kupokea mrejesho juu ya ubora pamoja na changamoto wanazokutana nazo wananchi na wadau wetu pindi wanapotumia huduma zetu,na kujionea hali halisi ya ubora wa huduma zinazotolewa katika ngazi za wilaya.

Ili kuongeza mvuto na tija katika ziara zetu tutaongozana na watu maarufu,wanaopendwa na wenye ushawishi kwenye jamii zetu ambapo tumepanga kuongozana na wasanii wa muziki wa kizazi kipya ili basi wananchi na wadau wetu watakaojitokeza kwenye ziara zetu mbali na kupata elimu juu ya huduma zitolewazo na Shirika la Posta Tanzania pia waweze kupata burudani,pia tutawatumia wasanii katika kututangazia huduma na biashara tunazozitoa kwa wananchi pindi tutapokuwa katika ziara mikoani,pia kututangazia huduma na biashara zetu katika majukwaa mengineyo kama mitandao yao ya kijamii wakati na baada ya ziara.

MALENGO YA POSTA KIDIJITALI (TUPO SITE TOUR)

LENGO KUU
Shirika la Posta Tanzania kutangaza huduma/biashara tunazozitoa kwa wananchi/wadau ili wananchi pamoja na wadau wetu waweze kupata uelewa mpana juu ya huduma na biashara zitolewazo na Shirika la Posta Tanzania.

MALENGO MENGINEYO
Wananchi na wadau wetu kupata uelewa juu ya umuhimu wa hudumana biashara zilizoboreshwa kidijitali.Wananchi wadau wetu kuelezwa kwa kina faida na manufaa yapatikanayo kwenye matumizi ya huduma za Posta zilizoboreshwa kidijitali.

Kuwavutia wananchi na wadau wapya kuanza kutumia huduma zinazotolewa na Shirika la Posta Tanzania na kuongeza wigo wa wateja.

Kukutana na wananchi na wadau na kupata maoni,mitazamo na mirejesho tofauti juu ya utendaji wetu ili tuweze kujua mahali gani tunafanya vizuri na mahali gani bado tuna changamoto.

Shirika la Posta Tanzania kupata fursa ya kuona na kung’amua fursa mbalimbali za kibiashara zilizopo katika maeneo tofauti,ambazo tunaweza kuzifanyia kazi na zikawa na tija kwa shirika.

Wananchi na wadau kupata fursa ya kupata taarifa sahihi zinazohusu Shirika la Posta Tanzania,fursa ya kuuliza maswali na kupewa ufafanuzi kuhusu maswala mbalimbali yanayohusu Shirika la Posta Tanzania.

FAIDA ZA POSTA KIDIJIITALI, TUPO SITE TOUR
Itaongeza uelewa wananchi na wadau wetu juu ya huduma na biashara mbalimbali tunazozitoa hivo kutuongezea wigo wa wateja wapya.

Itaa kwa wananchi na wadau wetu kutoa maoni na mawazo yao hivo kutuwezesha shirika kupata mitazamo mipya,pia kitendo cha kutoa fursa kwa wananchi na wadau kutoa maoni na mawazo yao itaongeza mahusiano ya muda mrefu kati ya wananchi na Shirika la Posta Tanzania.

Itatoa fursa kwa Shirika la Posta Tanzania kuzitangaza huduma zetu mpya zilizoboreshwa kwa njia za kidijitali,litaongeza kasi katika kufanikisha mpango mkakati wa 8 wa kibiashara wa Shirika la Posta Tanzania wa miaka 4 (2022-2026) ambapo lengo ni kulifanya shirika la posta kidijitali kwa biashara endelevu.

Itatoa fursa kwa Shirika la Posta Tanzania kuuelezea uma wa watanzania ubora wa huduma zetu,faida na manufaa ya kulichagua Shirika la Posta Tanzania,uwezo wetu wa vitendea kazi na teknolojia,sehemu tunazofika ambazo wengine hawafiki,nguvu kazi yetu tulionayo n.k ili wananchi waweze kuvutiwa na waanze kututumia Shirika la Posta Tanzania.

UTEKELEZAJI
Makongamano na semina,
Maonyesho ya wazi,
Matangazo kwenye runinga,,
Matangazo kwenye radio,
Matangazo kwenye mitandao ya kijamii,
Bill boards,
Vipeperushi.
 
Shirika hili ndilo shirika letu watanzania lakini sifahamu kwa nini linakuwa linakosa wabunifu ndani yake,

Yapasa lijigeuze kwa sasa na lifanye kazi na ulimwengu mzima, tukumbuke lina matawi tanzania nzima, kwa nini kwa sasa lisijigeuze na kuwa kama alibaba, tukaagiza mzigo duniani kote tukaletewa mpaka milangoni?

And viceversa, wakatengeneza apl kubwa, tukauza na hata kwa kilo uko ugaibuni.
 
Fungueni branch zenu kwenye kila bus terminal muanze kudeal na parcels nyie ni rahisi kuaminiwa kuliko haya mabasi maana nyie mzigo mtu anaweza kuufuata muda wowote ila mabasi lazima uwepo basi likifika tu

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app

Fungueni branch zenu kwenye kila bus terminal muanze kudeal na parcels nyie ni rahisi kuaminiwa kuliko haya mabasi maana nyie mzigo mtu anaweza kuufuata muda wowote ila mabasi lazima uwepo basi likifika tu

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Moja sifa ya shirika la posta limeenea kila wilaya ya Tanzania hivo tuchange shirika hili katika kupokea na kutuma mizigo yetu,"tuchague kuwa wazalendo tuchague shirika la posta"
 
Shirika hili ndilo shirika letu watanzania lakini sifahamu kwa nini linakuwa linakosa wabunifu ndani yake,

Yapasa lijigeuze kwa sasa na lifanye kazi na ulimwengu mzima, tukumbuke lina matawi tanzania nzima, kwa nini kwa sasa lisijigeuze na kuwa kama alibaba, tukaagiza mzigo duniani kote tukaletewa mpaka milangoni?

And viceversa, wakatengeneza apl kubwa, tukauza na hata kwa

Je wizi na udokozi umekwisha?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Jamani sifanyi KAZI posta nimetoa mapendekezo Tu kwa mawazo yangu namna ya kuboresha huduma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom