Wafanyakazi wa Posta na wizi wa mizigo ya wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi wa Posta na wizi wa mizigo ya wananchi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kileleni, Dec 25, 2008.

 1. K

  Kileleni Member

  #1
  Dec 25, 2008
  Joined: Dec 24, 2008
  Messages: 18
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Serikali inafanya nini kuhusu wizi katika posta nchini Tanzania? Hata barua za kawaida zinaibiwa na kufunguliwa na wafanyakazi wa posta.

  Nimewaandikia ndugu zangu mara nyingi na, kila mmoja wao, wamesema barua pamoja na picha nilizowatumia hazikuwafikia. Na wote wameniambia nisithubutu kuwatumia kitu chochote kupitia posta nchini Tanzania. Na mmoja wao amesema wananchi wengi wanasema itakuwa ni vizuri posta zikifungwa kwa sababu ya wizi huo ambao unaendelea kwa kasi.

  Malalamiko hayo yanatoka sehemu zote za Tanzania. Ndugu zangu niliowaandikia wanaishi sehemu mbali mbali - Dar es Salaam, Mtwara, Iringa, Mbozi, Mwanza, Bukoba, Tabora, na Arusha.

  Hakuna posta nchini ambayo haina wafanyakazi wanaoiba vitu mbali mbali - barua, vifurushi - vinavyotumwa kutoka n'gambo. Pia wana akili pungufu wanapofikiri kwamba kuna fedha katika barua hizo wanazozifungua.

  Labda wananchi wakigoma kutumia posta, hatua zitachukuliwa kupambana na wizi huo.

  Nimeishi n'gambo miaka michache (au mingi?) - zaidi ya kumi - na ni jambo la kukatisha tamaa kwa watu kama mimi tunaotaka kurudi nyumbani tunapoona serikali haifanyi chochote kurekebisha mambo - wizi, rushwa, mahongo, ufisadi na kadhalika.

  Tutajengaje taifa letu? Kama Mwalimu alivyosema, "Tanzania itajengwa na wenye moyo."

  Haitajengwa na wezi. Haitajengwa na wala rushwa au mahongo, na haitajengwa na mafisadi. Wamejaa serikalini na katika kila wizara na idara na sehemu mbali mbali kazini.

  Halafu kuna viongozi wanashangaa kwa nini wananchi wengi hawataki kurudi nyumbani? Si Tanzania tu bali nchi zote katika bara letu.
   
 2. D

  Darwin JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kileleni sio wafanyakazi wote wa posta ni wezi.
  Mimi ninachoona nikwamba kuna mtu aliwahi kukuibia mzigo wako wakati mmoja na akapata kile ulichotuma kwahio akiona tu kifurushi au barua inayotoka nchi fulani na jina lako wewe mtumaji basi anajua kwamba ataiba tena. Kumbuka kwamba pia barua zote zinazokwenda mikoani nazinatoka nje zinapitia Dar. Hii kama kuna mwizi analijua jina lako Dar akiona barua tu au mzigo wenye jina lako atauiba na hautafika mikoani.

  Siwezi nikaamini kwamba posta zote Tanzania ni wezi wa barua na vifurushi.

  Ushauri ni kwamba jaribu kutuma mizigo yako kutumia register, inakua rahisi kufuatilia mzigo wako ulipotelea wapi.
   
 3. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #3
  Dec 25, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Lakini hizi case ni typical, wengi sana wanaotuma vifuruhushi hulalamika. I am one of the victims. There must be something wrong with the corporation. The staff may be either incompetent or fraudalent.
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kama ingekuwa ni wimbo ningeuita ni wa zamani sana. Nawashauri kitu pekee ambacho mtumie posta yetu ni ankara za utilities mbalimbali, kama simu, maji na umeme.

  Ukituma kitu kingine unakuwa na uhakika wa asilimia 95 kuwa kitapotea, asilimia 5 tu ndio kitafika.

  Kuna makampuni binafsi ingwa bado hayajaendelea vizuri lakini yana uhakika wa kufikisha vifurishi na barua kwa haraka na kwa usalama. Lakini ukipenda kuendelea kutumia hili shirika letu linaloelekea kuwa mufilis, basi endelea at your own risk.
   
 5. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mtalalamika weeee mwisho mtachoka, Sector zote Tanzania ndivyo hivyo anzia kwa Mtendaji wa kijiji anakula kesi ndogondogo kijijini, Hospitali unauziwa dawa au damu huna pesa kufa kivyako, Mkurugenzi fulani anaacha ofisi na kwenda kwenye Warsha ili apate per diem yake hata mara tano hiyohiyo warsha moja, Mahakamani ndio kabisaaa kotekote kumeoza jamani msiwaonee Posta tu,
   
 6. D

  Darwin JF-Expert Member

  #6
  Dec 25, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kuna ushauri wa register kama nilivyosema mwanzo.

  Nakumbuka kwenye miaka ya juzi postmaster mmoja alipandishwa joto na wazungu fulani waliokua wanatumiwa vifurushi vyao kutoka nje na kila wakati vilikua vinapotelea kwenye posta yake.

  Mbona alifanya uchunguzi mpaka akajulikana mwizi ni nani na akaachishwa kazi
   
 7. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #7
  Dec 25, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 135
  Nimefanya kazi posta kwa muda wa miaka miwili hadi nilipokuja UK kwa masomo. Ningeweza kutoa maoni ambayo wadau wengi wametoa kama ningekua sina knowledge yoyote ya postal industry. Lakini kwa kuwa nimefanya kazi huko na sasa ninaishi ughaibuni kama ambavyo majority ya watoa hoja kuhusu suala hili, naamini maoni yangu yatakua na uzito kidogo.

  Watanzania wengi walioko ughaibuni wanakuwa wepesi kujump into conclusion kila mara mizigo yao inapopotea na kusema kuwa imeibiwa posta za nyumbani. Unaona wazi kuwa kuna fikra kuwa parcels/barua haziwezi kuibiwa katika posta za ‘wazungu', kama kuna wizi wowote wanaona ni lazima utafanyika nyumbani. Hii si sahihi hata kidogo, kama kuna wizi posta zetu za nyumbani ni wa scale ndogo sana. Last year niliona kwenye news (TV and papers) sio chini ya mara moja wafanyakazi wa posta za UK wakiwa matatani kwa wizi.

  Kingine ambacho wengi hawaelewi ni kwamba mashirika ya posta duniani husafirisha mizigo yao kwa kutumia vyombo mbalimbali vya usafiri, ndege in particular kama ni international mails/parcels. Kinachofanyika hapa ni kwamba wafanyakazi wa Posta watakwenda na furushi lao la barua na parcels na kuliacha mikononi mwa shirika la ndege ambalo nalo litaiacha mizigo hiyo mikononi mwa Laguage handling companies zinazo operate kwenye airports- naomba ieleweke pia kwamba kuna mianya ya wizi au upotevu katika mtiririko huu. Mwaka jana kuna CCCTV footage moja ilionekana nchi nzima hapa UK kwenye vituo mbali mbali vya TV, kuliwekwa kamera ya siri kwenye changing room baada ya tatizo la wizi kukithiri na wahusika walikamatwa.

  Kunakuwa na matatizo mengi ya upotevu na wizi wa mizigo pale ambapo mzigo wenye barua na parcels unapita in transit, nikimaanisha mzigo huo unapandishwa ndege zaidi ya moja. Kama ni US utatoka huko uliko, utashushwa na kupandishwa New York, kama ndege ni Emirates zoezi hilo litafanyika tena Dubai then ndo unapandishwa ndege ya mwisho. Ni jambo la kawaida sana, kwa mfano, wafanyakazi wa language handling companies kufanya makosa na kuupeleka mzigo wa Tanzania Taiwan na utakapofika huko itategemea umefikia mikononi mwa nani.

  Kuhusu uchelewesho, sina proof na hili ila nahisi pia wenzetu wa posta za nchi zilizoendelea wanazipa priority parcels/barua za kwao na zile zinazokwenda kwenye nchi zilizoendelea, wanadeal na za nchi maskini mwishoni. That is kama kuna ndege inakwenda Dubai toka New York na nafasi ni ndogo, mizigo ya UK , Germany, etc itapewa first priority na kama kuna kanafasi kadogo kakibaki baadhi ya mizigo inayokwenda Tanzania na Togo yaweza pakiwa. Hii inawezekana, lakini ni hisia zangu tu. Najua utakua unajiuliza- vipi kuhusu uchelewesho wa ndani? Ni wazi kwamba shirika la Posta bado halijawa na usafiri wa uhakika. Magari machahe ya posta yana operates katika routes za Dar- Iringa-Mbeya, Dar-Moshi- Arusha, Dar-Korogwe- Tanga, sina hakika kama kumekuwa na routes mpya tangu nimeondoka. Barua za route hizi huwa zinasafirishwa usiku wa siku zinapopokelewa. Kule ambako magari ya Posta hayafiki- usafiri wa ndege, mabasi na trains hutumika na vyombo vyoote hivyo vina matatizo yake na ukijumlisha matatizo ya mifumo yetu ya usafiri kwa ujumla-ni kawaida kusikia abiria wa traini au basi wamekwama njiani kwa siku tatu au zaidi, au majambazi wamepora abiria na mizigo ikiwemo ile ya posta kwenye basi Fulani.

  Naomba ieleweke kwamba wafanyakazi wa posta za nyumbani wanafanya kazi nzuri kwenye mazingira magumu na tunakuwa hatuwatendei haki kama kila mara tutakuwa tukiwalaumu kila kunapotokea wizi au upotevu wa vifurushi na naona its immoral kila mara kucompare na mazingira tunayoishi sasa huku ughaibuni, kwanini tunasahau tulikotoka? Tusiwe wepesi kumlaumu muhudumu kwenye restaurant chakula kinapokuwa kibaya wakati yeye kakileta mezani tu, mbona mpishi hatumgusi?

  Nawasilisha kwenu wadau- siwakilishi shirika la posta katika maoni yangu, nachangia tu kama wengine. Merry Christmas to you all, akhsanteni.
   
 8. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #8
  Dec 25, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  ok, KKN-hatukatai kwamba matatizo ya wizi hayatokei nchi za wenzetu. Tofauti ni kwamba wenzentu huyafanyia kazi haya matatizo. Sasa wewe mwenyewe umetueleza jinsi ambavyo wafanyakazi wa posta UK walivyofukuzwa kazi baada ya kugundulika wameiba. Lakini kwetu kwanza tayari umeshakana kwamba wanaiba, sasa hapo mtachukua hatua kweli?

  On a bigger pciture, ni rahisi sana kuhalalisha makosa yetu kwa kutolea mifano ya nchi zilizoendelea. Ni vizuri tukasisitiza hapa kwamba hakuna anayekataa kwamba wenzetu hawana matatizo. Tofauti iliyopo ni kwamba, wakati wenzetu wakifanya bidii ya kutatua matatizo kila yatokeapo, sisi hufanya bidii ya kuyaficha kwa kuyasokomeza mnvunguni mwa kitanda ili yasionekane.

  Sasa tazama tayari mwenzetu unafanya jitihada kubwa, tena kwa kutumia rangi ya blue katika maandishi yako, kuonyesha kwamba wafanyakazi wa posta yetu hawaibi. Sasa hivi ukirudi na masters yako hapo ukabidhiwa u-MD wa shirika la posta ndiyo tutegemee mabadiliko? Au ndiyo utakuwa unatumia uzoefu wako wa kuishi UK kuonyesha kwamba hata kwa wazungu matatizo ya kupotea kwa vifurushi yapo??!! it is incredible!
   
 9. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #9
  Dec 25, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Tukisubiri wateja wote wa posta wafanye kama hawa wazungu huu wizi hamtaukomesha!
   
 10. K

  Kileleni Member

  #10
  Dec 25, 2008
  Joined: Dec 24, 2008
  Messages: 18
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mbona watu wengi sana wanalalamika? Na wanaishi nchi mbali mbali.

  Kuna Watanzania wanaoishi Uingereza, Canada, USA, Australia na hata South Africa ambao ninawafahamu na ninawasiliana nao. Wao pia wanalalamika kwamba vifurushi vyao vinaibiwa. Hata barua zao zinaibiwa. Wametuma barua na vifurushi kwa ndugu zao na marafiki zao sehemu mbali mbali za Tanzania mara nyingi.

  Kwahiyo haiwezekani kwamba ni mtu mmoja tu au watu wachache pale posta Dar - ambako barua zote zinapitia kabla ya kwenda mikoani, pamoja na vifurushi - ambao wanaiba tunavyotuma kwa sababu wanayajua majina yetu aua wanautambua mwandiko wa kila mtumaji.

  Miaka minne iliyopita, nilmwandikia post master, Dar, kulalamika. Nilimpa pia anwani yangu ya email lakini hakunijibu.

  Nikawapigia simu ndugu zangu Dar na walisema hawashangai kuhusu wizi huo na kutojibiwa na post master. Conclusion? Theft is tolerated, condoned and even encouraged, and nothing is done about it.

  Unasema labda niki register vifurushi, hata barua, itakuwa rahisi kufwatilia vifurushi na kuonyesha wapi vilipotea au wapi viliibiwa. Vitafwatiliwa na nani? Wafanyakazi wa posta, na wakaguzi wao, ambao wanapuuza malalamiko yetu?

  Mimi si mtu wa kwanza kulalamika kwao. Kuna wananchi walionitangulia na hawakufanikikwa, hawakufika popote - they got nowhere!

  This is a very, very serious problem. In fact , it amounts to a national crisis. Na bila shaka hata investors kutoka n'gambo wameibiwa vifurushi vyao. Why not? Mwizi ni mwizi.

  Vifurushi na barua kutoka nchi za Ulaya na zingine zilizoendelea ni prime target. Lakini hata vinavyotoka nchi zingine viko hatarini kuibiwa. Ndiyo maana mwanzoni nilisema hata South Africa. Ingawa nchi hiyo haijaendelea kama zile za Ulaya na North America, vifurushi vinavyotumwa, pamoja na barua, kutoka nchi hiyo vinaibiwa pia kwa sababu wezi katika posta wanadhani kuna valuable items au hata fedha.

  This is just part of the culture of impunity our leaders - more than anybody else - have nurtured through the years which is going to sink us as a nation.

  Ndiyo maana nimesema it's a national crisis, wizi wa posta being one of the most prominent features of this problem.
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Dec 25, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Unayosema kama ka nsungu yanawezekana sana kama parcel inasafiri kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine. lakini kuna wizi na uharibifu wa vitu ambavyo vinasfirishwa within the country. Hili linatokeaje?
   
 12. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #12
  Dec 25, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Kana kasungu Ameongelea facts ya kwamba tulio wengi tunachukulia hawa watu weupe sio wezi ni wezi sana tena sana.

  Pia naungana na Mwl Kitila kwamba kuna kau jinga fulani kametukaa kuidhinisha upumbavu kwa kuangalia hawa watu weupe eti kwa vile wamefanya vile ama hivi ama kuwatumia wao kama reference point ya kila kitu.
   
 13. K

  Kileleni Member

  #13
  Dec 25, 2008
  Joined: Dec 24, 2008
  Messages: 18
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Si vifurushi kutoka n'gambo tu vinavyoibiwa ingawa ni prime target vikitoka nchi zilizoendelea. Hata vinavyotumwa within Tanzania vinaibiwa. And nothing is done about it.

  Unazangumzia wazungu na nchi zao - jiuluze kwanini wazalendo wengi wameamua kuishi katika nchi hizo badala ya kurudi nyumbani: Tanzania au nchi zingine za Kiafrika. Haimanishi kwamba nchi za Ulaya na zingine za wazungu kama Merikani hazina wizi au matatizo mengine lakini ukifaninisha na nchi zetu, tofauti ni day and night.

  Just face it.
   
 14. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #14
  Dec 25, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 135
  Kitila ninachotaka kusema ni kwa kifupi ni kwamba tusikimbilie kulaumu Shirika letu la Posta kabla hata hatujajua mzigo umepotelea wapi. Wengi wetu tukiskia mzigo umepotea tunaanza kuwamwagia lawama ndugu zetu wakati kumbe mzigo wako unaweza kuwa umeibiwa hapohapo Southampton unapoishi au Gatwick! Na sio kila mara mzigo usipokufikia unakuwa umeibiwa, kuna uwezekano ukapotea ie being delivered at the wrong destination.
  Juhudi za kudhibiti wizi zipo, pale GPO (Posta Mpya) ni moja ya sehemu chache sana Dar ambako kumefungwa mtambo wa kisasa wa CCTV, matukio yote yanarikodiwa, na kama ungekuwa umewahi kuingia sorting room ya pale ungeona ni jinsi gani layout yake inavyofanya wizi uwe mgumu.
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  Dec 25, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Huu wizi katika Posta upo na hasa kwa vifurushi na barua toka nje. Cha ajabu ni kwamba unapotuma vifurushi ndani ya Tanzania yenyewe wizi ni mdogo sana ama hakuna kabisa. Hivi karibuni nilishawishika sana na usalama wa posta za Tz na ni baada ya kukutana na wafanyabiashara wengi katika posta ya Kijangwani Unguja wakituma vifurushi kwa mafungu, bila wasiwasi wowote. Tena kama haitoshi wengi wao walikuwa wakifunga vifurushi hivyo ndani ya posta hiyo.

  Sasa hii inatoa picha gani? kwamba ni vifurushi tu vinavyotoka ng'ambo ambavyo vinashawishi wafanyakazi wa posta kuwa wadokozi?
   
 16. K

  Kileleni Member

  #16
  Dec 25, 2008
  Joined: Dec 24, 2008
  Messages: 18
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tukisema kwamba nchi za wazungu zinapambana na wizi kuliko nchi zetu za Kiafrika, inamaanisha kwamba tunawasifu wazungu kwa sababu ni wazungu au tuna acknowledge jitihada na bidii yao kuliko yetu?

  Umesikia huko Uingereza watu wa kila rangi wakisema kwamba 95 per cent vifurushi vyao vinaibiwa posta? Au barua zao zinaibiwa posta kama Tanzania? And even if they are, nothing is done about it?

  Botswana ni nchi ya Kiafrika, Wafrika weusi. Mbona inasifiwa na Wafrika weusi kama sisi kwa jitihada yao kimaendeleo na kupammbana na ufisadi? Ni nchi ya kizungu - na ndiyo maana inasifiwa na Wafrika ambao ni weusi?

  Haimanishi kwamba hawana matatizo hayo nchini mwao kule Botswana, lakini linganisha jitihada yao na ya viongozi wetu kupambana na wizi na ufisadi. Pia jiulize mwenyewe kwa nini Wafrika wengi kutoka nchi mbali mbali katika bara letu - pamoja na Tanzania - wamehamia Botswana au Namibia.

  Pia jiuluze kwanini Watanzania wengi pamoja na Wafrika wengine wameamua kuishi - au baada ya kumaliza masomo wemeamua kubaki - katika nchi za Ulaya, Merikani na nchi zingine za Magharibu au za aina ya Magharibi kama Australia, badala ya kurudi nyumbani kama maisha katika nchi hizo ni magumu kuliko maisha katika nchi zetu. Nani amewalazimisha kuishi katika nchi hizo? Wazungu - au rotten leadership katika nchi zetu?

  Truth is a bitter pill to swallow. But probably that's the only kind of medicine we need to start doing something ili taifa letu liendelee.
   
 17. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #17
  Dec 25, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Changamoto
  Kwanini vifurushi vinavyotoka TZ kwenda uingereza haviibiwi?
   
 18. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 135
  Ushauri wangu wa kitaalamu kwenu ni kama ifuatavyo:

  Ni muhimu kuandika anuani sahihi za mtumaji na mtumiwa katika barua/ kifurushi ili kuondoa uchelewesho usio wa lazima kwa kuwa inapotokea anuani imekosewa mwenye sanduku la posta anaweza kuandika try P.O Box………. (nina maana anuani nyingine ambayo yeye anaweza kudhani kuwa huenda inaendana na yake kwa kufikiria kuwa mtumaji anaweza kuwa amekosea). Danadana kama hiyo inaweza kuendelea kwa barua kutoka sanduku moja hadi nyingine na nyingine hupotea kwa mtindo huo. Barua kama hiyo inapoingia kwenye sanduku la barua ambalo anayelifungua sanduku hilo si mwaminifu anaweza kuichana na kuitupa au kuchukua mali zilizopo.

  Pamoja na anwani sahihi- nyaraka na vifurushi vinavyotumwa kupitia vya EMS ziandikwe physical address (jina la mtaa na nambari ya nyumba) pamoja na simu ya mtumiwa ili kurahisisha usambazaji.

  Vitu vyenye thamani vitumwe kwa njia ya EMS au kwa kusajiliwa (registered) au kukatiwa bima (insurance) ili kudhibiti usalama wake na pia kurahisisha ufuatiliaji.

  Aidha ni muhimu kuhakikisha kuwa kifurushi au parcel kinafungwa vizuri (properly packed) ili kisipasuke wakati kinasafirishwa. Ni muhimu kufunga vizuri kwa sababu usafirishaji wa barua, nyaraka na vifurushi kutoka nje ya nchi hususan Ulaya, Marekani, Asia, n.k hushughulikiwa na makampuni mbalimbali kabla ya kufikishwa Posta ya Tanzania.

  Ni vyema zaidi kwa mtumiwa kuwa na sanduku lake binafsi la barua ili kuweza kudhibiti barua ziingiazo katika sanduku lake. Gharama ya sanduku binafsi la kupokelea barua kwa mwaka ni sh. 12,000/- kwa Ofisi Kuu ya Posta Dar es Salaam, sh. 9,600/- kwa ofisi za Posta zilizoko miji mikuu, sh. 7,200/-kwa Ofisi za Posta Wakala (Franchised Post Offices) na zile zilizoko wilayani na sh. 1200/- kwa ofisi za Posta zilizoko vijijini. Uwezekano wa mzigo kupotea au kuibiwa ni mkubwa kama unatumia address ya taasisi, kijiji au jirani.

  Kwa yeyote mwenye tatizo kuhusu masuala ya Posta namba zao za simu ni +255 22 2118280 Ext: 336, 637 na 642 au 2121591, Fax: +255 22 2113081J, Email: customer.care@posta.co.tz. Ongea na Mrs Kanuti au Mrs Bujiku.
   
 19. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #19
  Dec 25, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145

  KKN,

  hivi katika posta zetu kuna CCTV katika maeneo yote sensitive katika kusimamia mizigo? Pili, nahisi hili suala linachangiwa pia na hukosefu wa incentives katika hawa wafanyakazi. Vilevile wadokozi hawawezi kukosekana lakini natumaini posta itajijenga na kuondoa hii dhana kwa kuboresha miundombinu ya kiusalama kama CCTV.

  Mimi nafagilia hawa posta kwa kitu kimoja, mizigo inayokwenda ulaya hususani vifurushi vinafika mapema na salama.
   
 20. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #20
  Dec 25, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama una uhakika na hili, mimi binafsi kuna parcel nilitumiwa toka bongo na sijaipata hadi leo na kwenye system za Royal Mail inaonekana kwamba ilikuwa delivered kwenye address yangu, bado nafuatilia!
   
Loading...